Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Pole mrembo...yasikuathiri. Cha msingi puuzia maneno utakaoletewa. Usiongeze neno kwa yale yatakayoletwa kwako na wala usijenge uadui kwa maneno yatakayoletwa kwako na nduguzo.

Kama uliweza kuwaleta pamoja watu waliotengana miaka 20 basi unaweza kuwaleta pamoja shangazi na baba zako.
 
Wasamehe,lakini wakitaka kuja tena waishie mlangoni,wasiingie tena ndani,


Wakati wewe uko bize unapambana na umasikini,ukiamini ndio adui yako,
Wao wako bize wakipambana na wewe,wakiamini wewe ndio adui yao,
Jitenge nao mbali,fanya mambo yako.
 
Pole mkuu kuna ndugu jau sana nina experience inaendana na yako nakuelewa vzuri. Me washajaribu hadi kunitenganisha na familia yangu kimkakati kabisa, washasema sana sitatotoboa Mungu si Asumani sahv napigwa vizinga hatari na kusomewa mashtaka ya watoto wao eti niwasaidie kuwashauri.

Ndo ile nakuheshimu sana na kama una shida ntakusaidia kama naweza ila tofauti na hapo tutaonana misibani na kwenye sherehe, funga vioo. Plus kuna mtu apo kasema usiulize wala kutaka kujua wanakusemaje, yes 100%.. what u dont know, can't hurt yo feelings.
 
Watu kama wewe huwa hawana maisha marefu bro... Anytime anything can happen!!!
Mzee wangu aliwahi nipa somo kwamba "watu wa aina tatu huwa hawana maisha marefu hapa dunian...... Kuwa mwelevu kweny kundi la wajinga (wewe upo hapa), migogoro ya ardhi na mwsho kabisa akasema kutembea na mke wa mtu


Anyway kuwa makini bro... Allah akutangulie🚶🚶
 
Simama na Mungu wako maana Mungu anasema waheshimu na kuwajali wazazi wako upate pepo ya mbinguni
 
Tunajua ulilelewa na single Mama sikia wewe kijana kwanza kabisa Ndugu zako wako sahihi kabisa wanapigania chakwao, damu yao, mtoto wao, usipambane nao, si shangazi zako hao lazima una tabia za kimama mama, sio bure, ndio mnapitia changamoto lakini tuliza akili fanya kazi kwa bidii wawezeshe hata kidogo shangazi zako, acha umama mama hapa unalia lia unakimbia majukumu, kua mwanaume wa kiafrika, changamoto ameumbiwa binadamu unalia lia nini acha umama mama.
 
Asante sana mkuu kwa Ushauri.

Ubarikiwe sana
 
Hakuna shida mkuu tuko pamoja🥂
 
pole ndugu yangu, silaha ya kwanza kabisa puuzia hayo yoote.
fanya kama hamna kilichopo kibaya kati ya wewe na ndugu zako, zidisha wema na tahadhari kwa wote, Focus kwenye issue zako mengingine yatapita kama yalivyo kuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…