Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafikiri niwapuuzie tu mkuu.kuwaleta pamoja sidhani Kama itatokeaPole mrembo...yasikuathiri. Cha msingi puuzia maneno utakaoletewa. Usiongeze neno kwa yale yatakayoletwa kwako na wala usijenge uadui kwa maneno yatakayoletwa kwako na nduguzo.
Kama uliweza kuwaleta pamoja watu waliotengana miaka 20 basi unaweza kuwaleta pamoja shangazi na baba zako.
🥺🥺🥺🥺Wasamehe,lakini wakitaka kuja tena waishie mlangoni,wasiingie tena ndani,
Wakati wewe uko bize unapambana na umasikini,ukiamini ndio adui yako,
Wao wako bize wakipambana na wewe,wakiamini wewe ndio adui yao,
Jitenge nao mbali,fanya mambo yako.
Ukishagundua watu hawakusaidii chochote kwenye maisha usiangalie nyumaAsante sana D.nitalifanyia kazi
Asante sana.Pole mkuu kuna ndugu jau sana nina experience inaendana na yako nakuelewa vzuri. Me washajaribu hadi kunitenganisha na familia yangu kimkakati kabisa, washasema sana sitatotoboa Mungu si Asumani sahv napigwa vizinga hatari na kusomewa mashtaka ya watoto wao eti niwasaidie kuwashauri.
Ndo ile nakuheshimu sana na kama una shida ntakusaidia kama naweza ila tofauti na hapo tutaonana misibani na kwenye sherehe, funga vioo. Plus kuna mtu apo kasema usiulize wala kutaka kujua wanakusemaje, yes 100%.. what u dont know, can't hurt yo feelings.
I’m a woman mkuu.Watu kama wewe huwa hawana maisha marefu bro... Anytime anything can happen!!!
Mzee wangu aliwahi nipa somo kwamba "watu wa aina tatu huwa hawana maisha marefu hapa dunian...... Kuwa mwelevu kweny kundi la wajinga (wewe upo hapa), migogoro ya ardhi na mwsho kabisa akasema kutembea na mke wa mtu
Anyway kuwa makini bro... Allah akutangulie🚶🚶
Fungua vioo wewe😂Wasamehe halafu wafungie vioo!
Hii njia imefanya kazi kwangu.
Unaogopa vitisho vya akina Yezebeli walivyomtisha Elia Mtishbi?Asante sana.
Ninashukuru kwa ushuhuda pia
Kumbe wanakuombea, Mimi nikajua labda kuna mtu amekukata mkono au Miguu hapo lingekuwa suala lingine, ndugu yangu kuombewa mabaya siyo wewe peke yako unayepitia hiyo Hali.Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.
Mimi na familia yangu(baba, mama, kaka na wadogo zangu) hatukutoka kwenye familia ya yenye uwezo. Maisha tuliyokuwa tunayaishi tangu nikiwa mdogo binafsi nilikuwa siyapendi kabisa na niliapa mimi wala watoto wangu hatutakuja kuishi maisha maisha niliyoyaishi nikiwa mdogo na niliapa kuja kubadilisha historia ya wazazi wangu.
Kwa ufupi tu haikuwa kazi rahisi lakini Mungu ni mwema, nililoliomba kwa miaka mingi limefanikiwa kwa asilimia 92. Ndugu zetu kwa upande wa baba kwanzia baba wadogo, babu, mashangazi walikuwa hawatukubali wala kutuombea mema.
Walituhesabu sisi ni fungu la kukosa, maisha hayakuwa rahisi lakini Mungu mwingi wa rehema amenitumia mimi kubadilisha familia ili nizidi kuongeza Utukufu.
Nitaruka ruka kidogo ili kufikisha ujumbe maana ni ndefu sana, najua hii ni personal life lakini nimeamua kuileta huku sidhani Kama kuna ubaya.
Wazazi wangu walitengana kama miaka 20 na zaidi iliyopita kila mtu akaishi kivyake, hali ya utengano iliunyong’onyeza sana moyo wangu kuna wakati nilikuwa nikienda kumsalimia mama najikuta namkumbuka baba yangu (hapo sijui alipo), nikajiuliza ni kwanini ninaumia hivi juu ya utengano huu wa wazazi wangu, nikajisemea moyoni hapana mimi ndie ninaetakiwa kuirudisha hii familia pamoja tena.
Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka nilikuwa na maswali mengi sana nikajisemea moyoni badala hawa ndugu wamshukuru Mungu ndugu yao amerudi nyumbani wao wanaanza kumpiga vita.
Maisha yakaendelea wakati Niko endelea kufanya utaratibu na kuzungumza na wazee ili kama kuna mila zifanyike başı mama yetu arudi nyumbani.
Wakati baba yuko nyumbani ugomvi ukawa ni mwingi sana na mashangazi, mara leo limetokea hili kesho lile nikasema ngoja nikate mzizi wa fitna maana ilikuwa inaonekana kama mama angerudi başi Vita ingekuwa kubwa ikabidi nizungushe ukuta kote kupunguza maneno.
Nikajisemea mpaka mtu aje kugonga geti kuanzisha ugomvi basi atakuwa amedhamiria kweli.
Baada ya kumalizana na ujenzi wa ukuta nikamrudisha mama nyumbani so kwa sasa wa naishi kwa upendo na Amani ingawa majaribu ya upande wa ndugu wa baba hayana budi kuja lakini Mungu anamuepusha nayo.
Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!
Moyo wangu unavuja damu, koşa langu liko wapi? Ninastahili maombi mabaya namna hii? Moyo wangu unamajeraha.
Nimeifupisha naomba kuiwasilisha.
Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.