Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Usiwasikilize sana hao ndugu uchwara fanya unachoona sahihi kwako mkuu na c lazma Kila mtu akupende..

Mm na ndugu yangu Mzee alimsomesha Kwa tabu sana Kwa kuuza kahawa na ndizi kipindi hcho bb mkubwa kasepa ,Mzee Kuna kipindi alikosa kbs Hela ya kulipia malipo ya shulee akaamua kuuza na shamba lenyewe Ili bro asomee ,km unavyojua ndugu jamaa na marafiki walimsema sana Mzee na kumcheka ety anauza shamba kisa mtt asomee ss atakufa njaa maana Hana pakulima tenaa,,

Leo hii bro alishamaliza chuo na kujiajiri ktk fani ya engineering anapigaa Hela na kununua mashamba km yt wale wale ndugu wameanziasha maneno bro n jambazi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aiseee,hvyo ubinadamu n kazi mkuu ..
Mkuu hii ishu atanielewa mtu ambae imeshamkuta au kushuhudia kWa wapendwa wao,vinginevyo nitaonekana najimwambafai au natafuta attention 💔💔💔
 
Pole sana mamy, zidisha maombi na mapambano ya kiuchumi.
NB:kamwr usithubutu kuwekeza nguvu za kupambana nao.
 
Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka
Pole sana mkuu.
Huwa ni kawaida sana ndugu(wa kiafrika) wakikaa au kuishi eneo moja wanakuwa kama glasi kwenye sinia...vijimaneno na ugomvi mdogo mdogo huwa haviishi.

Suluhisho ni kumwomba Mungu aendelee kukubariki ujenge makazi ya familia yako mbali na hao ndugu wa baba yako.

Nb. Hao ndugu ni hazina muhimu sana kwako kwenye haya maisha. Waepuke kwenye madhaifu yao lakini katu usijitenge nao.
 
Utibeli ndio dawa pekee ya magonjwa Yote.
Dua mbaya ndio kichocheo cha mafanikio yako kwa muumba.

Achana nao. Wape Haki yao kwa kuwaweka kundi wanalostahili
 
Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.

Mimi na familia yangu(baba, mama, kaka na wadogo zangu) hatukutoka kwenye familia ya yenye uwezo. Maisha tuliyokuwa tunayaishi tangu nikiwa mdogo binafsi nilikuwa siyapendi kabisa na niliapa mimi wala watoto wangu hatutakuja kuishi maisha maisha niliyoyaishi nikiwa mdogo na niliapa kuja kubadilisha historia ya wazazi wangu.

Kwa ufupi tu haikuwa kazi rahisi lakini Mungu ni mwema, nililoliomba kwa miaka mingi limefanikiwa kwa asilimia 92. Ndugu zetu kwa upande wa baba kwanzia baba wadogo, babu, mashangazi walikuwa hawatukubali wala kutuombea mema.

Walituhesabu sisi ni fungu la kukosa, maisha hayakuwa rahisi lakini Mungu mwingi wa rehema amenitumia mimi kubadilisha familia ili nizidi kuongeza Utukufu.

Nitaruka ruka kidogo ili kufikisha ujumbe maana ni ndefu sana, najua hii ni personal life lakini nimeamua kuileta huku sidhani Kama kuna ubaya.

Wazazi wangu walitengana kama miaka 20 na zaidi iliyopita kila mtu akaishi kivyake, hali ya utengano iliunyong’onyeza sana moyo wangu kuna wakati nilikuwa nikienda kumsalimia mama najikuta namkumbuka baba yangu (hapo sijui alipo), nikajiuliza ni kwanini ninaumia hivi juu ya utengano huu wa wazazi wangu, nikajisemea moyoni hapana mimi ndie ninaetakiwa kuirudisha hii familia pamoja tena.

Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka nilikuwa na maswali mengi sana nikajisemea moyoni badala hawa ndugu wamshukuru Mungu ndugu yao amerudi nyumbani wao wanaanza kumpiga vita.

Maisha yakaendelea wakati Niko endelea kufanya utaratibu na kuzungumza na wazee ili kama kuna mila zifanyike başı mama yetu arudi nyumbani.

Wakati baba yuko nyumbani ugomvi ukawa ni mwingi sana na mashangazi, mara leo limetokea hili kesho lile nikasema ngoja nikate mzizi wa fitna maana ilikuwa inaonekana kama mama angerudi başi Vita ingekuwa kubwa ikabidi nizungushe ukuta kote kupunguza maneno.

Nikajisemea mpaka mtu aje kugonga geti kuanzisha ugomvi basi atakuwa amedhamiria kweli.

Baada ya kumalizana na ujenzi wa ukuta nikamrudisha mama nyumbani so kwa sasa wa naishi kwa upendo na Amani ingawa majaribu ya upande wa ndugu wa baba hayana budi kuja lakini Mungu anamuepusha nayo.

Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!

Moyo wangu unavuja damu, koşa langu liko wapi? Ninastahili maombi mabaya namna hii? Moyo wangu unamajeraha.

Nimeifupisha naomba kuiwasilisha.
Uli

Ulichokosea ni kujenga karibu na ndugu zake, unatakiwa ujenge mbali kabisa ambapo mtu mpaka apande daladala.
 
Watu kama wewe huwa hawana maisha marefu bro... Anytime anything can happen!!!
Mzee wangu aliwahi nipa somo kwamba "watu wa aina tatu huwa hawana maisha marefu hapa dunian...... Kuwa mwelevu kweny kundi la wajinga (wewe upo hapa), migogoro ya ardhi na mwsho kabisa akasema kutembea na mke wa mtu

Anyway kuwa makini bro... Allah akutangulie[emoji124][emoji124]
Mkuu hivi vitu ulivyo vi list sipingi

Personally nimeshuhudia kwenye jamii zetu hizi

Mungu atuongoze
 
Huyu kayakanyaga Mwenyewe kwa sababu ianonekana anapenda kurushiana nao maneno lazima wamvuruge tu. Mpaka anakuja humu washamvuruga abadirike aache kujibizana nao hiyo ndio last solution's
It possible!!!! aache maneno,

Akiacha kurushiana maneno, maneno yatakoma.

Mbinu za vita ni nyingi mojawapo ni kukaa Kimya.
 
Kabisa yani! Kama mimi huwa sitakagi maneno mengi wala kelele kabisa ikitokea suala la familia natulia bila kelele naact afu sina muda wa kupigizana kelele.

Cc Smart911
Siku maslahi yako ya kiguswa au vile vitu ambavyo ni worth kwako utajijua vizuri wewe ni mtu wa aina gani

Personally nilikuwa kama wewe before sijakutana na mambo ya hovyo na siblings
 
Siku hizi mambo ya baba mdogo sijui watto wa baba mkubwa, yanapotea kwenye familia nyingi sana

Imebaki familia ni baba,mama na ndugu wa kuzaliwa.

Hilu nazidi kuliona sehemu nyingi.
Bora ibaki tu hivyo mkuu kuliko kuwa na ndugu wanakufanyia mambo ya ajabu
 
Kabisa unajua familia iki extend conflict nazo zinaongezeka

Mwisho kama mtoto usipokuwa makini unaingia kwenye mkumbo huo wa ndugu wa wazazi.
Yeah ni kweli, unaweza jikuta umefanywa mbuzi wa kafala huelewi usimame upande upi..
 
Back
Top Bottom