Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Huyu kayakanyaga Mwenyewe kwa sababu ianonekana anapenda kurushiana nao maneno lazima wamvuruge tu. Mpaka anakuja humu washamvuruga abadirike aache kujibizana nao hiyo ndio last solution's
Kabisa yani! Kama mimi huwa sitakagi maneno mengi wala kelele kabisa ikitokea suala la familia natulia bila kelele naact afu sina muda wa kupigizana kelele.


Cc Smart911
 
Habari ya wakati huu JF members, nina imani mnaendelea salama. Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba kushare japo kidogo hili swala ninalolipitia.

Mimi na familia yangu(baba, mama, kaka na wadogo zangu) hatukutoka kwenye familia ya yenye uwezo. Maisha tuliyokuwa tunayaishi tangu nikiwa mdogo binafsi nilikuwa siyapendi kabisa na niliapa mimi wala watoto wangu hatutakuja kuishi maisha maisha niliyoyaishi nikiwa mdogo na niliapa kuja kubadilisha historia ya wazazi wangu.

Kwa ufupi tu haikuwa kazi rahisi lakini Mungu ni mwema, nililoliomba kwa miaka mingi limefanikiwa kwa asilimia 92. Ndugu zetu kwa upande wa baba kwanzia baba wadogo, babu, mashangazi walikuwa hawatukubali wala kutuombea mema.

Walituhesabu sisi ni fungu la kukosa, maisha hayakuwa rahisi lakini Mungu mwingi wa rehema amenitumia mimi kubadilisha familia ili nizidi kuongeza Utukufu.

Nitaruka ruka kidogo ili kufikisha ujumbe maana ni ndefu sana, najua hii ni personal life lakini nimeamua kuileta huku sidhani Kama kuna ubaya.

Wazazi wangu walitengana kama miaka 20 na zaidi iliyopita kila mtu akaishi kivyake, hali ya utengano iliunyong’onyeza sana moyo wangu kuna wakati nilikuwa nikienda kumsalimia mama najikuta namkumbuka baba yangu (hapo sijui alipo), nikajiuliza ni kwanini ninaumia hivi juu ya utengano huu wa wazazi wangu, nikajisemea moyoni hapana mimi ndie ninaetakiwa kuirudisha hii familia pamoja tena.

Mungu alivyomwingi wa rehema akanibariki nikafanikiwa kujenga kijumba kidogo kwa ajili ya wazazi wangu (nikamrudisha kwanza baba nyumbani) baada ya baba kurudi vita vya ndugu vikaibuka nilikuwa na maswali mengi sana nikajisemea moyoni badala hawa ndugu wamshukuru Mungu ndugu yao amerudi nyumbani wao wanaanza kumpiga vita.

Maisha yakaendelea wakati Niko endelea kufanya utaratibu na kuzungumza na wazee ili kama kuna mila zifanyike başı mama yetu arudi nyumbani.

Wakati baba yuko nyumbani ugomvi ukawa ni mwingi sana na mashangazi, mara leo limetokea hili kesho lile nikasema ngoja nikate mzizi wa fitna maana ilikuwa inaonekana kama mama angerudi başi Vita ingekuwa kubwa ikabidi nizungushe ukuta kote kupunguza maneno.

Nikajisemea mpaka mtu aje kugonga geti kuanzisha ugomvi basi atakuwa amedhamiria kweli.

Baada ya kumalizana na ujenzi wa ukuta nikamrudisha mama nyumbani so kwa sasa wa naishi kwa upendo na Amani ingawa majaribu ya upande wa ndugu wa baba hayana budi kuja lakini Mungu anamuepusha nayo.

Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!

Moyo wangu unavuja damu, koşa langu liko wapi? Ninastahili maombi mabaya namna hii? Moyo wangu unamajeraha.

Nimeifupisha naomba kuiwasilisha.
Muamini Mungu na mtegemee yeye pekee ili akuvushe kwenye hii Vita.
 
Mkuu nilikuwa ninasubiria comment yako sana.

Ninakushukuru mno.
Nitafanya kilichosahihi.ubarikiwe🫶🫶🫶


Uki -Practice utafanikiwa kuwa na Amani Sana na familia na ukoo wako wataishi vizuri Sana.

Hiyo hali Kama yako wanapitia watu wengi , Ila unabidi kujua huwezi kuondoa Giza kwa kuweka Giza.

Hivyo ili uondoe Giza unabidi wewe kuwa mwanga.

Ukiwa positive Sana utaanza kupata Kitu kinaitwa Enlightenment macho ya yatafunguka Sana na kuanza kuona badala ya kutazama.


Kila MTU ni muhimu ,God never make no Junk and God never made a poor

Hivyo usijitenge na watu Ila watenganishe watu na siri zako

Play low key maintain be a commoner vaa vizuri pendeza Ila usipende kutaka kila MTU ajue Una nini au unamiliki nini.

Na elewa umasikini wa uchumi unatokana na
Umasikini wa fikra
Umasikini wa roho na baadae hufata umasikini wa fedha.

So don't hate anybody and Enjoy ur life to the fullest
 
Uki -Practice utafanikiwa kuwa na Amani Sana na familia na ukoo wako wataishi vizuri Sana.

Hiyo hali Kama yako wanapitia watu wengi , Ila unabidi kujua huwezi kuondoa Giza kwa kuweka Giza.

Hivyo ili uondoe Giza unabidi wewe kuwa mwanga.

Ukiwa positive Sana utaanza kupata Kitu kinaitwa Enlightenment macho ya yatafunguka Sana na kuanza kuona badala ya kutazama.


Kila MTU ni muhimu ,God never make no Junk and God never made a poor

Hivyo usijitenge na watu Ila watenganishe watu na siri zako

Play low key maintain be a commoner vaa vizuri pendeza Ila usipende kutaka kila MTU ajue Una nini au unamiliki nini.

Na elewa umasikini wa uchumi unatokana na
Umasikini wa fikra
Umasikini wa roho na baadae hufata umasikini wa fedha.

So don't hate anybody and Enjoy ur life to the fullest
😁😁😁

Asante kwa ushauri mkuu🫶

Sio Tajiri wala sina cha maana zaidi ya kujichanga tu.

😁😁hashtaglowkey
 
Wewe ni dhahabu, ishi nao kwa akili.Tumia mdaa mwingi kufikilia mambo Yako ya familia Yako! Ndugu zako ni wazazi wako na wanao!
 
Usiwasikilize sana hao ndugu uchwara fanya unachoona sahihi kwako mkuu na c lazma Kila mtu akupende..

Mm na ndugu yangu Mzee alimsomesha Kwa tabu sana Kwa kuuza kahawa na ndizi kipindi hcho bb mkubwa kasepa ,Mzee Kuna kipindi alikosa kbs Hela ya kulipia malipo ya shulee akaamua kuuza na shamba lenyewe Ili bro asomee ,km unavyojua ndugu jamaa na marafiki walimsema sana Mzee na kumcheka ety anauza shamba kisa mtt asomee ss atakufa njaa maana Hana pakulima tenaa,,

Leo hii bro alishamaliza chuo na kujiajiri ktk fani ya engineering anapigaa Hela na kununua mashamba km yt wale wale ndugu wameanziasha maneno bro n jambazi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aiseee,hvyo ubinadamu n kazi mkuu ..
 
Back
Top Bottom