Ndugu zangu vijana, UKIMWI unatafuna watu na sio wanyama

Yaani afadhali hata sasa hivi wagonjwa hawaugui na kukonda kama zamani...kwa mtu aliyewahi ishi au kumuona mgonjwa wa ukimwi aliyepitia dalili zote hakika atakuwa na adabu kama mbwa....mateso waliyokuwa wanapata huwezi elezea.
Mkuu mbwa ana adabu? Em unganisha adabu ya mbwa na hili swala la ukimwi
 
Halafu huwaga wakigundua wameambukizana mdudu na ndoa inaishiaga hapo hapo[emoji134][emoji134]....

Yaaan we ukishaona mifarakano ndoani ujue kimenuka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kwasasa ukiendekeza ngono lazima utaukwaa maana watu walioathirika especially w/me wanaambukiza sana mademu hovyo na hawa dada zetu wakishaona mtu ana hela hawajali status yake ya afya wao twende tu ili mradi apate pesa akadamshi awaringie mashostito wenzake.
 
Nina condition moja wanaita INNATE RESISTANCE TO HIV(IRH) hii inatokana na mimi kukosa receptor protein ijulikanayo kama CCR5-delta 32 kwenye seli hai nyeupe ambayo ndo huwa inatumika kama kihisishi cha magonjwa na pia ndiyo njia ambayo HIV anatumia kuingia ndani ya seli hai nyeupe na kuzidhuru mimi kutokuwa nayo ina maana hakuna njia ya kirusi kuingia ndani ya seli hai nyeupe hivyo napata virusi kwa muda kisha vinaondoka pindi seli zikimaliza mzunguko wake .Kiufupi HIV HANIDHURU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Screenshot_20190405-225950~2.jpeg
    32.8 KB · Views: 20
  • Screenshot_20190405-225950~2.jpeg
    32.8 KB · Views: 21
  • Screenshot_20190405-225950~2.jpeg
    32.8 KB · Views: 21
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…