Pesa ya ruzuku Kwa Chama kikubwa haiwezi kutosha kufanya kila kitu. Kuna kazi za kuutangaza Chama Kwenye mitandao ,kutumia vyombo vya habari ,magari ya safari ,kulipa wafanyakazi na safari zao ndani na nje ya nchi.
Kwa hiyo kujenga majengo ni jambo kubwa sana . Nadhani hujui kuwa CCM ilipokua inajenga ofisi kila Kijiji ,Kata ,Wilaya ,mkoa na Taifa walichangishwa mpaka wanafunzi mashuleni wakati huo ni Chama kimoja na serikali ilikua yao . Leo kutaka ACT au CuF ilingane na CCM kimiundimbinu ni mbingu na ardhi .
Kwa Sasa Tunataka tupate watanzania Wenzetu wakatutungie SHERIA ndani ya Bunge sio watu kutoka Punjabu na Gujarati au Pakistani au Paris.
Kukaomalia maofisi badala ya kupata watu wenye uwezo ni kuimarisha CCM B .
Tutoke Huko kwenye mavyama ya Siasa tuwekeze kwenye watu wenye uwezo na maono Kwa Taifa hili. Tutumie Kodi zetu kusomesha WAKULIMA na wafugaji na wafanyabiashara nje ya nchi. Wajifunze wanavyofanya Wenzetu na sio kuwategemea . Hii nchi inapotezwa na wahuni kushirikiana na mabilionea wageni wanaotaka kupora na kwenda kuishi Dubai kwenye Jiji kubwa la mabilionea wa Dunia nzima . Hawana muda na watoto wa maskini kule Namanyere. Watawaachia mashimo na matetemeko makubwa ya ardhi kutokana na kuharibiwa Kwa mazingira na uchimbaji mkubwa wa madini ya chuma na kuyasomba kupeleka Ulaya na China . Hakuna nchi iliyokuwa inasafririsha malighafi za madini nje Kwa kiwango hicho. Kiwanda Cha chuma kilipaswa kijengwe Liganga na sio kupeleka malighafi nje ya nchi.
Pumbavu sana wahuni.