Kwahiyo hapo mlokele unajiona umetoa elimu kubwa na maana sana kwa mustakabali wa taifa
Mlikimbia shule mnatapatapa humu walokole mnashida sana
Mdogo wang siyo kwamba najifanya natoa Elimu... ACHA Sasa nikupe Elimu basic kabisa tena Bure mdogo wangu.. Iko hivi... Nadhani umeshasikia kitu kuhusiana na
matumizi ya ardhi isn't it? ππ
Kwamba najua ushasikia eneo fulani la ardhi limetengwa kwa ajili ya kilimo tu, au ardhi fulani ni kwa ajili ya kujenga nyumba za makazi ya watu au ardhi fulani imetengwa kwa ajili ya kujenga shule , hospitali,soko n.k. Sasa mdogo wangu na anga hili unaloliona juu ya kichwa chako limepangiwa matumizi hivyo hivyo ,mdogo wangu.
Sasa nataka nikupe somo ... Anga hili unaloliona limegawanyika kwa madaraja tofauti kulingana na matumizi . Matumizi gani? ππ
Mdogo wangu ni matumizi ya usafiri wa Anga... Of course Sitaki kwenda deep hapa ....
Sasa Kuna anga maalum ya kurusha ki drone chako cha kufanya content creation kama Millard ayo
Kuna anga maalum kwa ajili ya shughuli ya ndege za kibiashara (air Tanzania, Kenya airways n.k) ambayo huitwa commercial au general airspace.
Kuna anga ni maalum kwa ajili ya shughuli za satellite , makombora ya masafa marefu n.k.
Na Kuna anga kwa ajili ya shughuli maalum mfano za kijeshi , ikulu n.k.. Ambayo huitwa restricted airspace.
Sasa mdogo wangu restricted airspace ni zipi?
Ni zile anga zinazozunguka Maeneo maalum mfano jeshini, ikulu ya rais au Maeneo ambapo Kuna viwanda vya nyuklia n.k
Anga hizi ambazo ni Restricted huwezi Kuta hata siku moja ndege ya abiria au drone imeruka Maeneo hayo pasipo ruhusa maalum.. nadhani umenielewa mdogo wa gu ...Sitaki kwenda deep sana najua hupendelei kusoma makitu marefu.
Sasa turudi kwenye hoja..
Anga ya Morogoro tayari hii ni Eneo restricted.. ndege yotote isiyohusiana na jeshi la anga la tz haiwezi pita bila ruhusa.. ikipita bila ruhusa basi inatunguliwa dakika sifuri mdogo wangππ.
Atleast nimekupa la mwanga kidogo mdogo wangu π