Ndege ndogo inatumia dk 10 mpaka 15 Morogoro to Dar. Lakini mchakato wa kuifikia Airport ya Dar, kwa wakazi wa Dar pamoja na utaratibu wa check-in unaweza kuchukua zaidi masaa mawili. Changanya bei kubwa ya usafiri wa ndege, na kutofuata ratiba au kutokuwa punctual kwa airlines zetu na abiria wake, utaona kuwa hicho kiwanja kikijengwa HAKITALIPA kwakuwa na idadi ndogo ya abiria. Abiria wengi wata-prefer kutumia njia nyingine za usafiri.
Miaka 100 ijayo kama nchi itakuwa imeendelea sana na abiria wapo wa kutosha wataweza kuwa na viwanja hata kama ni hapo Kibaha, Bagamoyo au Morogoro mjini au hata Morogoro kusini maeneo ya Mahenge (karibia 500 km from Dar) au Malinyi (karibu 600km from Dar).
Ni masuala zaidi ya kiuchumi (Returns on investments) na uwezo wa kiuchumi wa nchi ndio vyaweza kufanya tujenge viwanja kila mkoa au la.