Ndugu zangu wa Morogoro, mshawahi jiuliza kwanini ndege za Air Tanzania hazifiki kwenu?

Kwa sasa watz na waafrica tujikite kwenye train zaidi ya ndege ...treni za kisasa kwa usafiri wa ndani ni muhimu sana kuliko ndege ...badala ya kujenga airport tujenge terminal za sgr za kisasa kama ya dar es salaam...viwanja vya ndege viwe ni usafiri wa dharulu na usafiri wa kimataifa tu ...pia nauliza yale mabehewa ya gorofa ya sgr ndiyo yametelekezwa yapate kutu?πŸ™„πŸ™„πŸ™„ hatu sikii chochote kuyahusu.
 
Acha kamba jeshi la Tanzania hili la waponda kokoto halina uwezo wa kutungua ndege yeyote ile
 
Treni au road ndio mpango mzima. Kijiografia tu tz huwezi Jenga airport kila mkoa. Hapo kwenye mabehewa tuwaachie wizara ya uchukuzi.. wanajua wenyewe kinachoendelea
 
Hairuhusiwi hizo kukatiza anga ya Kijiji cha ngerengere... Na hizo ni special case kwa ruhusa au kibali maalum kutokana na uwepo wa mbuga za mikumi n.k.
Kuna morogoro airstrip iliyopo karibu ya ngerengere, nayo imezuiliwa lakini kuna kipindi huko nyuma auric air walikuwa wakifanya safari kufikia hapo.
 
Usinipangie cha kuandika au kusema humu, nitatumia uhuru wa kujieleza mwenyewe ninavyoona sawa na matakwa yangu.
Unakuja kuomba nini ?
Sikuelewi, wewe huingilii imani za watu?, au unataka ushahidi ?
Na kwenye elimu, nimesoma kukuzidi wewe, nina uhakika huo na kwa kuwa umeuliza , labda ujieleze wewe una elimu gani kunishinda mimi?
 
Unaongelea utadhani hiki kiinchi kina uwezo hata wa kutungua ndege za kivita kama labda tuseme Sukhoi 30 za Uganda zilizotengenezwa miaka ya 1980,
Unaongelea makombora ya masafa marefu yaani sijakuelewa unataka kusema leo bongo tuna uwezo wa kuipiga Sudan kutokea ngerengere πŸ˜‚



Ngoja sasa nikuonyeshe huko unakosema ni restricted area, unaona hio Flight runway, ilijengwa na kufunguliwa na mjeshi mwenyewe Kikwete, labda niwapongeze kwa ukubwa wa runway lakini hawana ndege za maana kulingana na hio runway


Haya turudi kwenye huo usiri unaoungelea, hivi unajua kuna vindege gani vimepaki hapo, ni vi chengdu J7 na Shenyang J6 utadhani ni mbayuwayu wametua πŸ˜‚
Haya nazooma sasa naenda huko restricted area na kukutana na hivi vidudu

Kujifanya wanakataza ndege zingine kupita hapo, ni ujinga ambapo mwenye atakaeamua kwa uwezo wa kijeshi au pia ndege za abiria zenye kuruka anga ya mbali ambayo hatuna uwezo wa kijeshi kuzitungua zinapita tu hapo, hakuna cha maana sana hapo
Ni kama vile kuandika maandisha ya USIKOJOE HAPA kwenye ukuta, wakati watu wanapita na kukojoa kila siku
 
Sema nini... Nlichojifunza kutoka kwako ni kama hutaki kujifunza na kujua mambo yanavyoenda kwenye hii dunia. Upo kimhemko sana.
 
Imenibidi nipitie comment zake kwenye baadhi ya nyuzi kwa kweli hayuko sawa nimeamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…