Ndugu zangu wa Morogoro, mshawahi jiuliza kwanini ndege za Air Tanzania hazifiki kwenu?

Haina noma ... Lakini unaona hii scheduled flight ya ndege ya air Tanzania inatoka dar kwenda kigoma hapa? Kwanini isikatize straight hapo kwenye anga ya Morogoro? ๐Ÿ˜ฌ๐Ÿ˜ฌ. Inapita pembeni pembeni kama mwizi... Mbona isikatize straight hapo kwenye anga ya ngerengere Airbase?. Tafuta kujua mambo ya dunia hii
 
Air Force base gani unaongelea? ya zile ndege za mrusi enzi za Soviet Union๐Ÿ˜, morogoro kubwa sana inaweza ikawa na Air Force na airport for civilian bila matatizo technology ya sasa inaruhusu, story yako ni chai
Sijasema hakuwezi kuwa na airport za ndege za civilian. Maana tayari Morogoro Kuna uwanja mdogo ule wa vumbi .. na zinatua ndege za kitalii sanasana. Na hapo Kuna kuwa na special permit inayotolewa na TCAA. na hata kama zinatua hapo Morogoro ,haziwezi katiza hapo ngerengere airspace.. umenielewa mdau?
 
Air Force base gani unaongelea? ya zile ndege za mrusi enzi za Soviet Union๐Ÿ˜, morogoro kubwa sana inaweza ikawa na Air Force na airport for civilian bila matatizo technology ya sasa inaruhusu, story yako ni chai
Nilivyomuelewa ni wilaya ya morogoro hiyo ndo restricted. Kwa maana morogoro mjini na morogoro vijijin kupita ngerengere. Ila kuhusu mahenge, gairo, malinyi sidhani kama anazungumzia huko
 
Hii haina mashiko, embu jenga hoja ya maana.

Mbona Singida, Manyara, na mikoa mingine hakuna hizo bases za jeshi na bado ndege za abiria hazitui huko?
Ha ha ha ha labda ngoja tumsubiri huyu msingida wa tai ya Taifa kama ataweza. Maana kila siku anatoa boko tuu hana jipya anakuwa kama empty box
 
Kwa hiyo ndege yetu tena, ikipita juu ya ngerengere itatunguliwa ๐Ÿ˜‚
Au watapiga picha ๐Ÿ˜‚umeshawahi kupanda ndege ukapiga picha chini, na kupata picha nzuri zaidi ya hii ya google maps inaonyesha mpaka mabweni yao ya kulala?



 
Reactions: Tui
Hoja yako angalau ina mashiko
viwanja vya ndege sio km vituo vya bus!
Ndege ndogo inatumia dk 10 mpaka 15 Morogoro to Dar. Lakini mchakato wa kuifikia Airport ya Dar, kwa wakazi wa Dar pamoja na utaratibu wa check-in unaweza kuchukua zaidi masaa mawili. Changanya bei kubwa ya usafiri wa ndege, na kutofuata ratiba au kutokuwa punctual kwa airlines zetu na abiria wake, utaona kuwa hicho kiwanja kikijengwa HAKITALIPA kwakuwa na idadi ndogo ya abiria. Abiria wengi wata-prefer kutumia njia nyingine za usafiri.
Miaka 100 ijayo kama nchi itakuwa imeendelea sana na abiria wapo wa kutosha wataweza kuwa na viwanja hata kama ni hapo Kibaha, Bagamoyo au Morogoro mjini au hata Morogoro kusini maeneo ya Mahenge (karibia 500 km from Dar) au Malinyi (karibu 600km from Dar).

Ni masuala zaidi ya kiuchumi (Returns on investments) na uwezo wa kiuchumi wa nchi ndio vyaweza kufanya tujenge viwanja kila mkoa au la.
 
Chai

Sasa kama ndege ndogo zinatuwa.

Si tayari usafiri wa Anga upo huko?
Jamaa kaandika kama vile kwenye anga letu vitu vinavyolindwa ni hiyo Ngerengere base tu. Ndege zinapita juu ya magogoni Dar na mtumba Dodoma halafu kwa Morogoro usingizie hako kakituo ka jeshi?
 
Waruguru watarusha ngumiiii...Kuna jamaa Jana mtu wa mlorogoro (morogoro) anabishaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ