Kwa faida yako pamoja na wapumbavu wengine acha nitoe ufafanuzi. Ili mtu ashiriki mashindani ya Olympic lazima awe amefikisha vigezo vilivyowekwa na kamati ya olimpiki ya dunia. Kwa mfano ili mwanariadha ashiriki mbio za Marathon kwenye olimpiki 2024 lazima awe ameshiriki kwenye mashindano yanayotambulika na shirikisho la riadha duniani kati ya 30th December, 2022 na June 2024 na awe amekimbia kwa muda usiozidi masaa 2:08:10, hapo ndo utaona kwenye hicho kigezo ni watanzania wawili tu walioweza kufanya hivyo. Hata kama serikali ingekuwa na nia ya kupeleka wachezaji 1000 isingewezekana kama hao wachezaji hawana rekodi zozote zinazotambulika kimataifa kwenye michezo wanayoshiriki. China yenye watu zaidi ya bilioni 1 imefanikiwa kupeleka wanariadha watatu tu kwenye marathon. USA na utajiri wake imefanikiwa kupeleka wanariadha wawili tu wa marathon.
Badala ya kumlaumu waziri Ndumbaro walaumu BMT, TFF, AT na vyama vingine vya michezo kwa kushindwa kuwasaidia wachezaji kushiriki mashindano makubwa yanayotambulika ili kupata vigezo vya kushiriki olimpiki. Kwa mfano hizi marathon nyingi zinazofanyika ni kama takataka kwasababu hazitambuliki na shirikisho la riadha duniani. Kilimanjaro marathon peke yake ndo inatambulika.