Siku saba kabla ya uchaguzi!
Muda mzuri wa kuwanunua 'wakala' wanaotafuta shibe.
Hatari kubwa kwa CHADEMA ipo hapa. Kuna mtego mahsusi umewekwa kuwanasa.
Kwa mtazamo wa kibinadamu, hii inaonekana kuwa hatari ya kweli..
Lakini, kama hatima ya mwisho wa CCM na Magufuli wao imeshasainiwa na abebaye hatima ya kila kitu, na kila mtu...
Then, hakuna kinachoweza kuzuia hilo kutokea..
Hebu rudisha tafakari yako nyuma kidogo hadi uchaguzi mkuu wa 2015..
Kila mtu mawazo yake na imani yake aliiweka kwa Edward Lowassa au Bernard Membe, kwamba mmojawapo ndiye angeweza kuwa mgombea urais - CCM badala ya Magufuli..
Lakini ktk hali isiyotarajiwa hao wote "nature" ikawatupa kando. John Pombe Magufuli bila hata kuelewa haya mambo yamekuwaje, akawa mgombea Urais kupitia CCM na akawa Rais wa JMT 2015 - 2020
Pointi yangu hapa ni kuwa, kilichokwisha kuamuliwa ktk ulimwengu wa roho, hakuna kinachoweza kuzuia kisitokee ktk ulimwengu wa mwili pamoja na jitihada nyingi za kibinadamu kuzuia..!!
Kama upinzani umeshaamuliwa kuchukua uongozi wa nchi hii dhidi ya CCM na Magufuli, itakuwa hivyo hakuna kitakachozuia bila kujali nini kinafanyika kuzuia hilo.!