Uchaguzi 2020 NEC: Mawakala wataapishwa siku saba kabla ya uchaguzi

Uchaguzi 2020 NEC: Mawakala wataapishwa siku saba kabla ya uchaguzi

Sasa kama wanachadema wote ni waadilifu na wapo tayari kulipambania taifa hata kwa kuingia barabarani, inakuwaje mnakosa Imani juu ya mawakala wenu ambao nao Ni miongoni mwenu.?
Au ndo tukubaliane, mpo kwaajili yakutafuta shibe ili msife kwa unyafuzi?
Safari hii uzuri ni kwamba hata hawa watakaopenda kushibishwa akili zitawarudia watakapoona 'sunami' itakayowazoa hao waliowanunua.
Maana yake ni kwamba pamoja na kupata shibe, kazi watakayotakiwa kuifanya hawataifanya.

Itakula kwa hao waliowashibisha.

Umeelewa sasa?
 
Mtego niliouna apo: alisema mawakala wataapishwa na barua zao za kutambuliwa watazikuta kituo cha kupigia kura.... kwaio Wakala hatatoka nyumbani kwake na Utambulisho wowote bali ataukuta kwenye kituo cha kupigia kura...... Aminini mawaambia hapa ndipo ulipofichika mchezo mchafu.
Mtego huu hapa ni mbaya.

Natumaini CHADEMA na ACT watakataa upuuzi huu.
 
Vyama hasa CDM, baada tu ya kuapishwa hawa makawaka watageuka na kuwa na thamani kubwa mno...ni lazima wawe na timu ya kuwalinda..... !! Mawakala ndiyo uchaguzi wenyewe!!

Mawakala ndiyo ushindi wenyewe, huwezi kupewa ushindi kirahisi...lazima hujuma za kila aina pamoja na majaribu ya kiuchumi yatawapitia.
Eeeh! Sasa mtaongozaje nchi wakati mkiwa hamuaminiani?

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Tunamshukuru tume kwa kuendeleza na utaratibu mzuri wa uchaguzi wetu huu, ama kwa hakika uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki.
 
Eeeh! Sasa mtaongozaje nchi wakati mkiwa hamuaminiani?

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
mwambieni jamaa yenu aanze kuaga...roho ya kukataliwa inatembea naye mgogoni...ni mshahara wa hayo aliyoyafanya...
 
Siku saba kabla ya uchaguzi!

Muda mzuri wa kuwanunua 'wakala' wanaotafuta shibe.

Hatari kubwa kwa CHADEMA ipo hapa. Kuna mtego mahsusi umewekwa kuwanasa.
Mawakala wakikubali kuhujumu,wajue hiyo dhami haitawaacha salama.
Vitu vitatu vinavyowafanyaga mawakala kuhujumiwa kirahisi ni cha kwanza ni njaa na cha pili ni njaa na cha tatu ni njaa.nakumbuka kule Newala mawakala walipewa hela waemde kula chakula.waliporudi walikuta matokea yanajumlishwa.Najua yule aliyeshinda kipindi kile namkumbuka kwa jina moja alikuwa anaitwa Njwayo,atakuwa anaukumbuka huu mchezo.

mpango uwepo wa kuwasaidia chakula siku hiyo.wasipewe chakula cha msaada,kitawekewa vitu vitakavyowaletea uzubavu.Pili vyama wachague mawakala ambao wana stake ikiwa chama kitashinda.
 
Hivi ninyi mnaangaika na nini,mmekalia kuibiwa kuibiwa na ukiwa na akili za hivi ina maana unaenda na matokeo tiyali unayajua, hivyo unajiami,,nawataadhalisha Msije Anguka na presha
Kwani wizi CCM wameanza leo?
Haya niambie zile serikali za mitaa zipo kwa vile CCM ni watu waaminifu sana?

Nadhani nikuache tu kwa sababu unaonyesha wazi wewe ni kondoo tu hata kama hili hulijui!
 
Mawakala wakikubali kuhujumu,wajue hiyo dhami haitawaacha salama.
Vitu vitatu vinavyowafanyaga mawakala kuhujumiwa kirahisi ni cha kwanza ni njaa na cha pili ni njaa na cha tatu ni njaa.nakumbuka kule Newala mawakala walipewa hela waemde kula chakula.waliporudi walikuta matokea yanajumlishwa.Najua yule aliyeshinda kipindi kile namkumbuka kwa jina moja alikuwa anaitwa Njwayo,atakuwa anaukumbuka huu mchezo.

mpango uwepo wa kuwasaidia chakula siku hiyo.wasipewe chakula cha msaada,kitawekewa vitu vitakavyowaletea uzubavu.Pili vyama wachague mawakala ambao wana stake ikiwa chama kitashinda.
Mkuu, safari hii CHADEMA wanayo fursa nzuri sana ya kuukomesha ujinga huo.

CHADEMA ni lazima wawawekee semina hawa watu kabla au ndani ya hizo siku saba.

Wawaeleze hao mawakala kwamba baada ya uchaguzi huu, wengi wa hao mawakala ndio watakaokuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, kwa hiyo njaa yao itakayokuwa imetibiwa kwa mlo mmoja wa CCM sio kitu cha kushadadia.

Bila shaka wengi wa wakala hawa watakuwa wametokana na watu kama walimu na kada nyingine. Hawa wana uelewa wa kutosha na hawawezi kutupa mlo wa miaka mitano kwa mlo wa siku moja.

Jambo la muhimu ni CHADEMA kuwachambua wakala miongoni mwa wanachama wao na wapenzi wa chama hicho wanaoelewa uaminifu wao. Wasiparamie tu mamluki wa siku tatu toka CCM.
 
Safari hii uzuri ni kwamba hata hawa watakaopenda kushibishwa akili zitawarudia watakapoona 'sunami' itakayowazoa hao waliowanunua.
Maana yake ni kwamba pamoja na kupata shibe, kazi watakayotakiwa kuifanya hawataifanya.

Itakula kwa hao waliowashibisha.

Umeelewa sasa?
Unavyowasemea sasa, utafikiri uatakuwa kwenye ufahamu wao🤪.Chamsingi mkizidiwa hatutaki kusikia zile kelele zenu za kujitetea kuwa mmeibiwa kura.
 
Kwani wizi CCM wameanza leo?
Haya niambie zile serikali za mitaa zipo kwa vile CCM ni watu waaminifu sana?

Nadhani nikuache tu kwa sababu unaonyesha wazi wewe ni kondoo tu hata kama hili hulijui!
Naona hujaelewa nilicho andika
 
Hivi wakuu kwa nini Lissu alishikia bango sana mawakala waapishwe?
Sawa kiapo ni kiapo hata mashetani wanaotafuna pesa zetu bungeni mawaziri waliapa. Full usanii na mzaha kwa dini. Anyways na kisheria blaa blaa

Swali langu ni technically speaking Tundu Lissu aliona kuna nini hapa kwenye kuapisha???

Na je chaguzi za nyuma hakukua na kuapishwa?
Nahisi ni kwa sababu iwapo wakala hajaapishwa haruhusiwi kusimamia uchaguzi
 
Back
Top Bottom