Pre GE2025 NEC yabadilishwa jina sasa kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Msemaji wa serikali anawatangazia "Utumiaji wa jina" ni kama ana sisitiza maagizo/maelekezo ya gazeti la serikali yaanze kuzingatiwa. Kwamba kuanzia tarehe hiyo Ijumaa Aprili 12, 2024, machapisho yote ya Serikali na Taasisi zake, yawe yanatumia Tume huru ya uchaguzi badala ya NEC.
 
Ni kama kusema CCM imebadili jina na kuitwa Chama Cha Mapinduzi.
 
Asante sana kwa taarifa hii, mimi ni miongoni mwa Watanzania tuliopendekeza NEC iitwe Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=lqufL6e34DyB2Gjr
P
 
Uhuru wake upo wapi wakati hadi taarifa na maamuzi yake yanatolewa na Msemaji wa Serikali? Kujizungumzia tu imeshindwa halafu wanadanganya watu kuwa ni Tume Huru?

Halafu watu walitaraji kusikia kubadilika kwa watendaji wa tume husika na jinsi watakavyopatikana. Siyo huo upuuzi wao.
 
Ni habari njema kwa wapinzani. Kwa miaka mingi wamekuwa wakililia tume huru ya uchaguzi na sasa kilio chao kimesikika.
 
Mdogo mdogo tutafika...kama Ngamia vile kichwa kinaanza ingia mwisho mabega kisha mwili mzima... kwa kubadili jina tu ni ishara kuwa mambo yanogile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…