Pre GE2025 NEC yabadilishwa jina sasa kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuwape imani, mabadiliko ni mchakato. Kuanza tu kwa jina zuri inatosha kuanza kuwapa ujasiri hata wale maafisa wa tume.
 
Kwani Watanzania walikuwa na Tatizo na Jina la Tume au Mchakato mzima wa Uchaguzi? Maana kubadilisha jina bila kubadili mfumo mzima wa uendeshaji wa Tume hadi namna ya kuwapata Watendaji wa Tume Itakuwa tu sawa na Abdallah kumuita Dullah au Mohamed Kumuita Mudi a.k.a MO. HAPO HAKUNA UHURU BALI JINA LIMEBADILISHWA
 
Wananchi tunataka tume huru siyo kibadilisha jina kujiita huru wakati wasimamizi wakiwa wateule wa rais.Kwa mwendo Huu Hadi tutwangane makondendiyo muheshimu matakwa ya wanachi
 
1. Nani anateua wajumbe wa Tume hii?
2. Utaratibu wa kuwateua upoje?
3. Wanawajibika kwa nani?
 
Uhuru upi inayo hii tume??
Hata Korea kaskazini inaitwa Democratic peoples republic of korea πŸ˜„ 🀣 πŸ˜‚ πŸ˜†
 
Hivi majina ya walioomba kusimamia uchaguzi yameshatoka au bado yamekaliwa na Tume?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…