NEC yakabidhiwa magari 12 maandalizi Uchaguzi Mkuu

NEC yakabidhiwa magari 12 maandalizi Uchaguzi Mkuu

Joined
Apr 4, 2020
Posts
16
Reaction score
7
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amekabidhi magari 12 kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ni sehemu ya magari 20 yalionunuliwa na tume ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

1586157297044.png

​
Akizungumza mara baada ya kukabidhi magari hayo, leo Aprili 4,2020 Mhagama amesema Serikali itahakikisha kwamba NEC inawezeshwa kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na Sheria ili iweze kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki. “Kwetu sisi kama Serikali wajibu wetu wa kwanza ni kuhakikisha kwamba Tume haikwami katika kutekeleza majukumu yake, hata fedha zinazohitajika katika shughuli zote za uchaguzi zinatengwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali,” amesema Mhagama.

1586157315899.png
​

Mhagama ameipongeza NEC kwa weledi katika utendaji kazi na kusema kwamba msingi wa uhuru wa Tume uliowekwa na Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 utaendelea kuheshimiwa na Serikali.

1586157339778.png

1586157359448.png
​

“Nchi kama Malawi na nchi nyingine zinakuja kujifunza kwenye Tume hii, nakupongeza sana Mwenyekiti (wa Tume) na wafanyakazi wote. Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ametamka kwamba mwaka huu tuna uchaguzi na ametamka kwamba uchaguzi huo lazima uwe huru na haki. Magari haya 12 mmepata, mtapata magari mengine nane (8) na sio magari tu bali vifaa vyote vya uchaguzi vimeshafikia hatua nzuri ya manunuzi, fedha zimeshatengwa,” amesema Mhagama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa (NEC) Jaji Semistocles Kaijage ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa Tume ili iweze kutekeleza majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria


1586157383394.png

1586157399493.png
​
 
Mkuu Maendeleo Kwanza, safi sana kwa habari hii!. Hizi ndizo habari za kimaendeleo tunapaswa kusikia. Hapa NEC inajengewa uwezo na serikali yetu kwa capacity building.

NEC ambapo ni Tume huru ya uchaguzi, japo sio shirikishi, pia ijengewe uwezo kutoa elimu ya mpiga kura kwa umma. NEC kama NEC yenyewe tuu pekee yake, haiwezi, lazima i-team up na wadau wa utayarishaji wa vipindi na utangazaji ili kuwaelimisha Watanzania.

P
 
Mkuu Maendeleo Kwanza, safi sana kwa habari hii!. Hizi ndizo habari za kimaendeleo tunapaswa kusikia. Hapa NEC inajengewa uwezo na serikali yetu kwa capacity building. NEC ambapo ni Tume huru ya uchaguzi, japo sio shirikishi, pia ijengewe uwezo kutoa elimu ya mpiga kura kwa umma. NEC kama NEC yenyewe tuu pekee yake, haiwezi, lazima i team up na wadau wa utayarishaji wa vipindi na utangazaji ili kuwaelimisha Watanzania.

P
Hatutaki NEC iliyo huru kwenye makaratasi Bali inayofanya kazi kwa Uhuru na itapatikana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magari 20, Toyota Landcruiser za mkonga iwe ni habari ndogo!.
P
Vp kwani ilishindikana tu kutolewa taarifa fupi ikielezea hilo tukio?
Kulikuwa na umuhimu gani wa kukusanyika?Yale maelekezo ya ku-keep social distance at least one meter hayawahusu wao?
 
Back
Top Bottom