Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) ULIOFANYIKA SEPTEMBA, 2026
UTANGULIZI
Katika Mkutano wake wa 173 uliofanyika tarehe 02 Novemba, 2026 katika ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania zilizopo Dar es Salaam, Baraza la Mitihani liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika Septemba, 2026.
USAJILI NA MAHUDHURIO
Jumla ya watahiniwa 1,168,718 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi wakiwemo Wasichana 637,214 (54.52%) na Wavulana 531,504 (45.48%). Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wenye mahitaji maalum walikuwa 4,921 sawa na asilimia 0.42.
Kati ya watahiniwa 1,168,718 waliosajiliwa, watahiniwa 1,139,318 sawa na asilimia 97.48 walifanya Mtihani wakiwemo Wasichana 624,976 (98.08%) na Wavulana 514,342 (96.77%). Aidha, Watahiniwa 29,400 (2.52%) hawakufanya Mtihani, wakiwemo Wavulana 17,162 (3.23%) na Wasichana 12,238 (1.92%).
MATOKEO
Ufaulu wa Jumla
Jumla ya watahiniwa 970,876 sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa 1,139,273 wenye matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2026 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C. Mwaka 2025 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia.81.80. Hivyo, ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 3.42. Ufaulu kwa kuzingatia jinsi unaonesha kuwa, Wavulana ni 443,254 sawa na asilimia 86.18 na Wasichana ni 527,622 sawa na asilimia 84.43. Mwaka 2025 Wasichana waliofaulu walikuwa asilimia 81.21 na Wavulana waliofaulu walikuwa asilimia 82.51. Hivyo, ufaulu wa Wasichana umeongezeka kwa asilimia 3.22 na ufaulu wa Wavulana umeongezeka kwa asilimia 3.67.
Kuhusu ubora wa ufaulu, watahiniwa 429,667 sawa na asilimia 37.72 wamepata madaraja ya A na B ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.82 ikilinganishwa na mwaka 2025.
Ubora wa ufaulu kwa Wasichana umeongezeka kwa asilimia 0.56, ambapo mwaka 2026 umefikia asilimia 34.27 ikilinganishwa na asilimia 33.71 mwaka 2025.
Kwa upande wa Wavulana, ubora wa ufaulu nao umeongezeka kwa asilimia 1.17 hadi asilimia 41.90 ikilinganishwa na asilimia 40.73 mwaka 2025.
Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja mbalimbali umeainishwa katika Jedwali Na.1.
Jedwali Na.1: Ufaulu wa Jumla
Idadi ya Shule katika Makundi ya Umahiri
Kati ya shule 20,010 zilizofanya PSLE 2026, shule 12,914 (64.54%) zimepata wastani wa Daraja la C (utepe wa Njano) ikilinganishwa na madaraja mengine ya ufaulu. Shule zilizopata wastani wa madaraja ya A na B (Utepe wa Kijani) zimeongezeka kwa asilimia 0.01 kutoka shule 5,503 (28.32%) mwaka 2025 hadi kufikia shule 5,670 (28.33%) mwaka 2026. Aidha, shule zilizopata wastani wa Daraja la A-C zimeongezeka kwa asilimia 1.66 ambapo mwaka 2026 ni shule 18,584 (92.87%) ikilinganishwa na shule 17,727 (11.21%) katika mwaka 2025.Mchanganuo wa idadi ya shule katika Makundi ya Umahiri umebainishwa katika Jedwali Na. 2.
Jedwali Na. 2: Idadi ya Shule katika Makundi ya Umahiri kwa Mwaka 2026
ikilinganishwa na Mwaka 2025Ufaulu wa Watahiniwa Kimasomo
Masomo ya Lugha
Ufaulu wa somo la Kiswahili mwaka 2026 ni asilimia 93.13 ukiwa umeongezeka kwa asilimia 5.56 ikilinganishwa na mwaka 2025, Wasichana waliofaulu ni asilimia 93.61 na Wavulana ni asilimia 92.56.
Kwa upande wa somo la English Language ufaulu ni asilimia 50.50 ambao umeongezeka kwa asilimia 0.39 ikilinganishwa na mwaka 2025. Wasichana waliofaulu ni asilimia 50.71 na Wavulana ni asilimia 50.23.
Kwa kuzingatia ubora wa ufaulu, somo la Kiswahili limeonesha ongezeko la watahiniwa waliopata madaraja ya A na B hadi kufikia asilimia 73.81 ikilinganishwa na asilimia 59.65 mwaka 2025. Katika somo la English Language ubora wa ufaulu umeongezeka kwa watahiniwa waliopata madaraja ya A na B hadi kufikia asilimia 22.56 kutoka asilimia 20.95 mwaka 2025.
Masomo ya Sayansi Jamii
Ufaulu wa somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi mwaka 2026 ni asilimia 76.53 na ufaulu wa somo la Uraia na Maadili ni asilimia 90.12. Ufaulu wa Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi umeongezeka kwa asilimia 6.24 ikilinganishwa na mwaka 2025 na katika somo la Uraia na Maadili ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.75. Kwa kuzingatia jinsia, Wasichana waliofaulu katika somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi ni asilimia 74.53 na Wavulana waliofaulu ni asilimia 78.97. Katika somo la Uraia na Maadili, Wasichana waliofaulu ni asilimia 89.96 ikilinganishwa na Wavulana ambao ufaulu wao ni asilimia 90.31.Kwa ubora wa ufaulu, somo la Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi limeonesha ongezeko la watahiniwa waliopata madaraja ya A na B kutoka asilimia 27.87 mwaka 2025 hadi asilimia 36.53 mwaka 2026. Hata hivyo, katika somo la Uraia na Maadili kumekuwa na kushuka kwa ufaulu wa watahiniwa waliopata madaraja hayo mawili kutoka asilimia 56.68 mwaka 2025 hadi asilimia 54.00 mwaka 2026.
Masomo ya Hisabati na Sayansi
Ufaulu wa somo la Hisabati mwaka 2026 ni asilimia 62.56 ukiwa umeongezeka kwa asilimia 5.90 ikilinganishwa na mwaka 2025. Wasichana waliofaulu ni asilimia 60.27 na Wavulana ni asilimia 65.34. Ufaulu wa somo la Sayansi na Teknolojia mwaka 2026 ni asilimia 80.34 ukiwa umeshuka kwa asilimia 4.09 ikilinganishwa na mwaka 2025. Katika somo hili, Wasichana waliofaulu ni asilimia 76.25 na Wavulana waliofaulu ni asilimia 85.31.Kuhusu ubora wa ufaulu, somo la Sayansi na Teknolojia limeonesha kushuka kwa watahiniwa waliopata madaraja ya A na B hadi asilimia 33.60 kutoka asilimia 48.14 mwaka 2025. Katika somo la Hisabati ubora wa ufaulu umeongezeka hadi kufikia asilimia 32.47 kutoka asilimia 21.92 mwaka 2025.
Mchanganuo wa ufaulu wa watahiniwa katika masomo mbalimbali ni kama ilivyooneshwa kwenye Jedwali Na. 3.
Jedwali Na. 3: Asilimia ya Ufaulu kwa Watahiniwa
katika Masomo MbalimbaliMATOKEO YALIYOZUILIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 371 waliougua hivyo kushindwa kufanya Mtihani kwa idadi kubwa ya masomo au masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kurudia kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2027 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.MATOKEO YALIYOFUTWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya watahiniwa;26 ambao walibainika kufanya udanganyifu katika Mtihani,
05 walioandika lugha ya matusi katika skripti zao.
Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(i) na
(j) cha Sheria cha Baraza la Mitihani Sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za Mwaka 2016.
PONGEZI ZA BARAZA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri/Manispaa/Jiji, Wakuu wa Shule, Wasimamizi na Wasahihishaji wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2026 kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kutekeleza jukumu la Uendeshaji wa Mtihani huo. Aidha, Baraza linawapongeza watahiniwa wote waliofanya Mtihani kwa kuwa na utulivu na kuzingatia taratibu za mitihani katika kipindi chote cha Uendeshaji wa Mtihani.UTOAJI WA MATOKEO
Matokeo ya Kumaliza Elimu ya Msingi yalikuwa yakitolewa na kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani yakionesha namba na jina la mtahiniwa. Hata hivyo, kwa kuzingatia Kanuni na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, matokeo yatatolewa bila kuwa na majina ya watahiniwa. Namba za mtihani zitatumika kutambua matokeo ya kila mtahiniwa. Hivyo, mtahiniwa atakayesahau namba ya mtihani, mzazi/mlezi anashauriwa kuwasiliana na Mkuu wa Shule ambayo alifanyia Mtihani ili kupata matokeo yake.UPATIKANAJI WA MATOKEO
Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2026 uliofanyika Septemba, 2026 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:www.necta.go.tz,
www.moe.go.tz
www.tamisemi.go.tz,
Baraza la Mitihani la Tanzania litawasilisha Matokeo haya kwenye Mamlaka zinazohusika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa Kujiunga na Elimu ya Sekondari.
Prof. Said A. Mohamed KATIBU MTENDAJI 03/11/2026