NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba 2019. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 3.78

Huo mtihani ulitungwa huko kanda ya ziwa! Yaani ni Graiyaki sijui, Mara, Shinyanga, Geita, Kagera! Lengo ni kumfurahisha baba mwenye nyumba au?
Unasikia bingwa, hayo matokeo hasa hiyo shule namba 1 kwa maoni yangu kuna sarakasi.
wawachukue hao watoto wote leo wawape mtihani mwingine utaona ukweli, mtihani utungwe na kufungiwa ndani pamoja na watunzi hadi siku wanapofanya watahiniwa.

Kanda ya ziwa kuna vurugu sana ya udanganyifu iwe kurudia mitihani kwa jina jingine n.k.
Kagera ni kawaida yake lakin

Haya ni matokeo ya mwaka Jana tazama kagera ilivyokawaida yake.

Tena mwaka huu imeshuka
Maana 2017 na 2018 ilikuwa ya kwanza
FB_IMG_15685370365574361.jpeg
 
Unasikia bingwa, hayo matokeo hasa hiyo shule namba 1 kwa maoni yangu kuna sarakasi.
wawachukue hao watoto wote leo wawape mtihani mwingine utaona ukweli, mtihani utungwe na kufungiwa ndani pamoja na watunzi hadi siku wanapofanya watahiniwa.

Kanda ya ziwa kuna vurugu sana ya udanganyifu iwe kurudia mitihani kwa jina jingine n.k.
Nakuhakikishia hiyo shule ya kwanza itakuumbua ..naijua watoto wanajua mpaka wanakera..hao walio top ten hata ukiwapigia simu usiku huu wafanye mtihani nina hakika watakuumbua vibaya mno
 
NECTA imetangaza Matokeo ya Darasa la Saba 2019 na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanya udanganyifu
*****

Baraza la Mtihani la Taifa (Necta) limesema katika Mtihani wa Darasa la saba uliofanyika Septemba 11, 2019 wamebaini walimu Wakuu, Wasimamizi na walinzi walihusika kufanya udanganyifu

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati akitangaza matokeo ya darasa la saba na kueleza kuwa katika kikao kilichokaa leo tayari wameshazitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie hatua waliohusika na udanganyifu huo. Ambapo kwa sasa udanganyifu kwa ujumla umepungua ambapo mwaka 2011 ulikuwa 9,736 na mwaka huu umefikia 900.

Amesema kuwa katika matokeo hayo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu, matokeo ya jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asilikia 3.78.

"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.

Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.

Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.

Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.

Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.

Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha.
Kwa Kifupi HALMASHAURI ZOTE /JIMBO YA WAPINZANI YAMEONGOZA KWA UFAULU HUKU JIMBO LA CHATO, LA NDUGAI, LA MAJALIWA, LA SAMIA ANAPOTOKA, LA SIRRO, LA MZEE WA TISS /MWANGA, hayapo, hii inaonyesha jinsi Mungu anavyozidi kumuumbua Jiwe na sera zake za kugawa watu , eti hapeleki maendeleo majimbo ya upinzani as if hizo hela anatoa mfukoni, tena si ajabu hayo majimbo ndio yanakusanya zaidi kuliko hayo ya CCM, oka okay Tatizo ushamba
 
Tulizoea ufaulu wa watoto wawili au watano kwenye shule kwenda sekondari le mnatuambia asilimia hizo??? Je wasiojua kusoma na kuandika ni wangapi na mtawajuaje ikiwa tumeambiwa mpaka F. 5 wapo wasiojua kusoma na kuandika? Sawa hiyo? haaaaata.
Kwasasa kuanzia chekechea hadi kidato cha 4 ni elimu msingi. Ndio maana unaona wanafaulu tu ili wengi waipate elimu hiyo. Kigezo cha kujiunga sekondari ni kujua kusoma na kuandika Kiswahili.

Wasiojua kusoma na kuandika wapo na ukiwauliza walifauli vipi, wala hawana hiyana. Majibu yao ni "tulishade au tulionyeshwa majibu".

Walimu wakiliongelea wanaambiwa wajitahidi tu hadi wafike kidato cha nne, maana kidato cha2 anahidaji D mbili tu kuvuka. Na akifeli mara ya kwanza mara ya pili anapitishwa tu. Wakifika kidato cha4 ndio 0 za kutosha zinamwagika hapo.
 
Well said...sasa mtu ukiongea ukweli utaonekana ni tatizo na kama upo kwenye system wanakutema kabisa...siasaaa...twende tu
Elimu ya Tanzania inauliwa na siasa. Watoto wanafaulishwa ili shule zifanye biashara. Wanafaulishwa ili mradi waende mbele
 
Heko simiyu, wasukuma tuna akili nyingi mno, ni suala la muda tu kabla hatujawa vipanga wa karne
Acha ushamba wa "wasukuma" na vitu kama hivyo zaidi ya hapo hizi shule ni za watu wote hivyo unaweza kukuta aliyefanya vizuri akawa Mwenye asili ya Kagera, Kilimanjaro, Kigoma nk
 
Acha ushamba wa "wasukuma" na vitu kama hivyo zaidi ya hapo hizi shule ni za watu wote hivyo unaweza kukuta aliyefanya vizuri akawa Mwenye asili ya Kagera, Kilimanjaro, Kigoma nk
Soma vizuri hayo matokeo kali.o wewe, kwahiyo shule zote za huo mkoa wanatoka watu wa mikoa tofauti? unafikiri kwa kutumia nini?
 
Kanda ya ziwa tuko vizuri, tunawakilisha hata huku Western hongereni sana ndugu zangu
👏👏
Acha ushamba wa kikanda hauna manufa, encourage watu wako wawe na maendeleo ya kweli na kujitegemea ndio kutawasaidia wawe na upeo mkubwa wa kutambua mazingira yao na changamoto zilizopo
 
Soma vizuri hayo matokeo kali.o wewe, kwahiyo shule zote za huo mkoa wanatoka watu wa mikoa tofauti? unafikiri kwa kutumia nini?
Ok tuchukulie "ni wasukuma" je kuna wafanya kuwa ni bora zaidi kuliko jamii zingine?? % ngapi wana shule zilizo bora?? % ngapi wana nyumba zilizo bora?? % ngapi wana nguvu za kiuchumi vs jamii zingine % wana biashara au viwanda vinavyo eleweka
 
Wanafunzi kumi bora wote kanda ya ziwa

Shule kumi bora zote kutoka kanda ya ziwa

Mikoa ya kanda ya ziwa imeingia top ten

Wale wa kule milimani vipi naona mnapotea kwenye ramani

Chanzo mwananchiView attachment 1234189
Hapa pia
Hivi tuko ktk mashindano ya kanda hii dhidi ya kanda nyingine???
Tuwaache watoto washindane bila kuwa na itikadi ya ukanda, hata kama mwingine alikunyanyasa, kukudharau nk dawa ni kufanya kilicho bora ktk jamii bila kuonyesha dharau au mashindano kwa wengine
 
Ok tuchukulie "ni wasukuma" je kuna wafanya kuwa ni bora zaidi kuliko jamii zingine?? % ngapi wana shule zilizo bora?? % ngapi wana nyumba zilizo bora?? % ngapi wana nguvu za kiuchumi vs jamii zingine % wana biashara au viwanda vinavyo eleweka
Ni suala la muda kabla hatuja take over, huyu mmoja tu anafanya mambo makubwa Tanzania
 
Hivi tuko ktk mashindano ya kanda hii dhidi ya kanda nyingine???
Tuwaache watoto washindane bila kuwa na itikadi ya ukanda, hata kama mwingine alikunyanyasa, kukudharau nk dawa ni kufanya kilicho bora ktk jamii bila kuonyesha dharau au mashindano kwa wengine
Kwenu zenji nini
 
Back
Top Bottom