NECTA yatangaza Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka mwaka 2017

NECTA yatangaza Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2018. Ufaulu waongezeka kwa asilimia 4.96 kutoka mwaka 2017

Hapo lazima watusue yani mtihani full machagulio ebu fikilia mtoto anapewa swali hili

Raisi wa kwanza wa tanganyika alikua ni nyere_______
A: ra
B: re
C: ri
D: ro
Inasikitisha sana. Pia kiukweli mkuu kwa uandishi wako na wewe inaonekana ni zao la mfumo ule ule wa elimu unaokosolewa. Maneno kama yani, ebu, fikilia, raisi, tanganyika, nyerere....
 
Naamini sio kwa KUMFURAHISHA MTU bali ni uhalisia
 
IMG-20181023-WA0021.jpeg
 
Haya ndio matunda ya Dkt. Athumani Kihamia aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambaye sasa ni Mkurugezni wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hivi kwanini Chadema inawapiga sana vita wachapa kazi kama huyu Dkt. Kihamia?
Kweli namba hazidanganyi. Hongera zikufikie huko uliko Dk. Kihamia endelea kufanya kazi kwa bidii watu wataangalia matokea sio maneno ya wanasiasa. Hongera sana
 
Kweli namba hazidanganyi. Hongera zikufikie huko uliko Dk. Kihamia endelea kufanya kazi kwa bidii watu wataangalia matokea sio maneno ya wanasiasa. Hongera sana
Kweli wanasiasa wanaongopa ila namba haziongopi
 
Baraza la Mitihani NECTA limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi (darasa la saba) ambapo matokeo yanaonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.96% tofaiti na ufaulu wa 2017 ambao ulikuwa asilimia 72.76%

Dk. Charles Msonde amesema katika tathmini ya awali kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.9% ikilinganishwa na 2017, amesema pia kiwango cha ufaulu wa somo la Kiingereza uko chini sana tofauti na masomo mengine

Baraza la Mitihani nchini limewafutia matokeo watahiniwa 357, waliobainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani iliyofanyika mwaka huu 2018

"Baraza limezuia kutoka matokeo ya watahiniwa zaidi 100 kutokana na kuugua kipindi cha mtihani na kuwapa fursa ya kufanya mtihani huo mwaka 2019" Dk. Charles Msonde

Jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 wamefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wasichana ni 382,830 sawa na 77.12% na wavulana ni 350,273 sawa na 78.38%

Takwimu zinaonyesha ufaulu katika masomo ya Kiingereza, Maarifa ya jamii, Hisabati na Sayansi umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 ikilinganishwa na mwaka uliopita

Wakati huo huo, ufaulu katika somo la Kiswahili umeshuka kwa asilimia 1.44

View attachment 908258
View attachment 908259
View attachment 908260
View attachment 908261
View attachment 908262

Kuona matokeo hayo | Fungua link zifuatazo

http://41.59.85.99/psle/psle.htm

https://www.necta.go.tz/results/2018/psle/psle.htm
Kila la heri waliofaulu,kwa waliofail hamjafail maisha,standard seven wapo hata bungeni,Msukuma and Lusinde ni mifano hai
 
Kagera bado utabaki kuwa mkoa Wa vichwa hata tuongee vipi!! Wameingiza Shule NNE kwenye kumi bora
 
Naona siku hizi wanafunzi hawafeli kabisaaa....naona ufaulu wa wastani wa A. Kweli hii elimu bure. Kipaumbele kwa sasa wafike kidato cha 4
 
Back
Top Bottom