Uko sahihi! hawezekaniSidhani kama kuna ukweli hapa😆😆😆😆 computer inasaisha ya darasa la saba tu huko mbele haiwezi na ikiweza itatoa ufaulu usio sahihi😁
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko sahihi! hawezekaniSidhani kama kuna ukweli hapa😆😆😆😆 computer inasaisha ya darasa la saba tu huko mbele haiwezi na ikiweza itatoa ufaulu usio sahihi😁
Atafaulu?
St francisWapi mkuu
St Francis au
A level Canossa?
Hongereni sana mliofaulu ,pia pongezi kwa Canossa,Mzumbe na Ilboru.NECTA wameandika matokeo ya Kidato cha nne na Upimaji wa kidato cha cha Pili na Darasa la Nne 2021, yatatangazwa hivi punde kaa tayari ndio mida hii.
All the best Comrades, see you at the top.
=====
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2020 yakionyesha kuwa asilimia 85 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu.
Kwa mujibu wa Necta iliyotangaza matokeo hayo leo Ijumaa Januari 15, 2021 kupitia kwa katibu mtendaji wake, Dk Charles Msonde, watahiniwa 434,654 walifanya mtihani huo na 373, 958 wamefaulu katika madaraja mbalimbali. Dk Msonde amesema kwa matokeo hayo kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 5.19.
Katika mtihani huo Paul Luziga wa sekondari ya Pandahill iliyoko Mbeya amekuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa.
Orodha ya walioongoza kitaifa kidato cha nne
1. Paul Luziga - Panda Hill
2. Justina Gerald - Canossa.
3. Timothy Segu - Mzumbe
4. Isaya Rukamya - Feza Boys
5. Ashraf Ally - Ilboru
6. Samson Mwakabage - Jude
7. Derick Mushi - Ilboru
8. Layla Atokwete - Canossa
9. Innocent Joseph - Mzumbe
10. Lunargrace Celestine - Canossa.
Shule bora kitaifa ni Peaceland Secondary School kutoka Mwanza
Mikoa 3 iliyofanya vizuri:
Dar es Salaam
Lindi
Arusha
Link ya matokeo kamili![]()
https://matokeo.necta.go.tz/csee2020/csee.htm
=====
MATOKEO KIDATO CHA NNE 2020: NECTA YASEMA UFAULU UMEONGEZEKA KWA 5.19%
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde, amesema Watahiniwa wa Shule 373,958 (85.84%) kati ya 434,654 waliofanya Mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne 2020 wamefaulu
Ameeleza kuwa, idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 5.19 ikilinganishwa na matokeo ya Mitihani ya mwaka 2019 ambapo Watahiniwa waliofaulu walikuwa 340,914 (80.65%)
Amesema Wasichana 193, 672 sawa na 85.44% wamefaulu Mitihani hiyo huku Wavulana wakiwa 182,086 sawa na 86.27%. Watahiniwa wapatao 490,213 walisajiliwa kufanya Mitihani hiyo
Labda wa kudangaHivi mtu anapata A zote hizo dah.. kweli tunatofautiana... Ngoja nirudi form four Marian girls nnaeza kua TO
Hakunaga mtoto mwenye akili anaesoma Ayo ma shule wanaiba paper tuAaaaah ouk sawaah, but kwa A level mpeleke St Mary's mazinde Tanga, au Marian girls, uwezo ukizidi kidogo mpeleke Feza girls.
Labda wa kudanga
Asante sanaDarasa la nne matokeo haya »»» https://matokeo.necta.go.tz/sfna2020/sfna.htm
Mkuu wa kitangaza ya kidato Cha pili naomba unitagBaraza la mitihani la taifa (NECTA).
Leo Tarehe 15-01-2021 litatangaza matokeo ya kidato cha pili, nne na darasa la nne ya mwaka 2020/2021
darasa la nne mkuu, link
Syllabus
Wakati dogo wangu ana pne ya 11 huko kusini vijijini.Mwenye point 9 ndio wa mwisho [emoji3][emoji3][emoji3][emoji23]
Utakuwaje TO huku kuandika neno NAWEZA hujui?.
Neno Kua maana yake ni kuongezeka, to grow, while kuwa ni kuwepo au to be.
Hebu tujifunze kuzungumza na kuandika kwa usahihi.
Uhakika ni daraja la kwanza hadi la tatu la alama 22. Hapo nazungumzia kidato cha tano kwenye Shule za Serikali. Kwenye shule nyinginezo ni hadi daraja la nne la alama 28. Huo ni uelewa wangu Mkuu.Mkuu saidia kama unauelewa kwenda form 5
From form 4:
Cut off point ni ngapi?
Au matokeo yaweje?