Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Ndugu zama zimebadilika, mazingira yamebadilia na maisha yamebadilika. NHC ya zama hizo ya sera za kijamaa ilishakufa kitambo sana. Watanzania hatuhitaji tena kuwa na NHC ya kutujengea nyumba walalahoi maana NHC haiokoti pesa, tunataka NHC ya kusaka pesa za matajiri wanaotaka kuishi sehemu chache specho, ili hizo pesa tukajengee madarasa, zahanati, vyoo vya shule nk.

Watanzania walalahoi huenda tuko karibu milioni 40, sasa NHC itajenga nyumba ngapi ili sote tukae?
 
Afu mpangaji anajiita mnyonge
Wakuambiea wajenge hawataki
 
Kwani hizo nyumba ni mali ya mchechu au ni za umma, hao matajiri kwa nini wasiende kujenga huko boko na bunju..
 
Hii operation mbona ni ya nchi nzima mkuu?
Lengo lake ni kuondoa majengo ya kizamani yanayo milikiwa na NHC, City Centres nchi nzima na ku replace na mapya ya kisasa yenye kuendana mandhali ya kisasa na eneo husika, kama gorofa ndefu zaidi.

By the way the man is my Role Model.
 
Kwani hizo nyumba ni mali ya mchechu au ni za umma, hao matajiri kwa nini wasiende kujenga huko boko na bunju..
Kwa urahisi mngehama tu
Mana sijui mtamshinda NHC/Mchechu kwa hoja gani

Wewe mpangaji ndo ukajenge Bunju
Hapo NHC ni kwako?
Bunju kwa R.O.I ipi?
 
Kwa hiyo malengo ya NHC yamebadilika kuwa shirika la kuwajengea matajiri nyumba......kwani matajiri wana shida katika kujenga nyumba zao wenyewe hadi NHC ianze kuwajengea.
 
Hapo hakuna cha mikataba inasemaje, shirika linakusanya kodi kwa nini lisikarabati na kujenga nyumba badala ya kutaka kuwapa matajiri hizo nyumba kwa kisingizio cha kuingia ubia, yanajengwa mazingira ya upigaji na rushwa nono nono.​
Kwa mfano halisi unaweza kukuta, Kodi inayokusanywa na NHC kwenye jengo moja chakavu lillopo prime area labda ni wastani wa shilingi laki tano kwa mwezi (kwa miaka mitatu: 500,000 x 12 x 3 = 18milioni) wakati gharama za maintenance kwa mwezi ni wastani wa shilingi laki tatu (kwa miaka mitatu: 300,000 × 12 x 3 = 10.8milioni), na kulifanyia ukarabati muhimu hilo jengo (kama kupiga rangi, sewage system, umeme, vitasa, milango, vioo, madirisha, sakafu) kila baada ya miaka mitatu ni shilingi milioni 20. Sasa piga mahesabu.
Mapato: 18milioni
Maintenance+Ukarabati: 30.8milioni
Hasara: 10.8milioni

Kwanini NHC isiwaze uwekezaji wenye ubia katika mazingira hayo?
 
Wewe ni mpangaji tu, hupaswi kumpangia mwenye nyumba nini cha kufanya kwenye nyumba zake.

Kama NHC wameamua kuingia ubia na watu wengine ili kuvunja hizo nyumba ili wajenge kitu kingine, wewe mpangaji unakuhusu nini?

Kama unaona NHC wanakuzingua si uhame tu, kwanini ung'anganie hapo hapo kama kwako hapo?
 
Katiba baba achana na Nehemia. Mkiambiwa katiba mnaona watu ni wasaliti. Tulia wembe ukate
 
Kwa hiyo malengo ya NHC yamebadilika kuwa shirika la kuwajengea matajiri nyumba......kwani matajiri wana shida katika kujenga nyumba zao wenyewe hadi NHC ianze kuwajengea.
NHC haijawahi kuwa na sera ya kuwapangisha wanyonge (maskini), sera zao za zamani zilikuwa kutoa huduma kwa watanzania wote na sio kufanya biashara, kwa sasa sera zao zimejikita kufanya biashara na watu wote.

Matajiri hawana shida ya kujengewa nyumba na NHC, wao wana shida ya kufanya biashara na NHC katika sekta ya makazi. Matajiri wana pesa (lakini hawana maeneo prime) na NHC hawana pesa (lakini wana maeneo Prime), lakini wote wawili wanataka kufanya biashara. Nini kitatokea? Watakaa mezani na kufanya deals, mwisho wa siku maisha yanakwenda.
 
Mkuu, watu wanajitoa ufahamu tu na huenda wengine ni machawa wanatumika, hapo kuna uonevu ulio wazi ili kuwanufaisha wajanja wachache. Kuwasemea wanaoonewa siyo lazima kwamba sisi ni wapangaji kwenye hizo nyumba, wengine tunaishi kwenye nyumba zetu lakini hatupendi watu wa hali ya chini waonewe.
 
Bora zivunjwe, muhame mkajenge zenu.
Mmejisahau sana nyinyi wapangaji wa Upanga. Hela zenu mnanywea bia, hamjengi. Mkifa, watoto wenu watarithi nini?
 
Kinachofuata ni kuhamisha walimu woote wa SUA, Mzumbe na UDSM. Nyumba ziwe mabweni ya wanafunzi. Walimu wote 'wanapaswa' kuwa na nyumba zao katika umri huu.
Hizi nyumba za chuo zinafanya wengi wanabweteka. Wanastaafu wanaenda tena kupanga.
Kuanzia sasa nyumba za staff wa vyuo inatakiwa wakae wanafunzi wa Masters na phD.
Walimu wakajenge zao.
 
Halafu watu wa aina hii kesho watatatea kwa nguvu zote bunge la ulaya likitunga uongo serikali imetoa wananchi kwenye njia ya bomba la EACOP na kuweka ushahidi sio kweli wamelipwa fidia na kujengewa nyumba kuonyesha ethical credentials za serikali mbele ya mabeberu. Bila ya kuelewa morally hakuna tofauti na hiki wanachotaka kufanya NHC ni kitu hiko hiko na kina stahili equal treatment kwa wapangaji wao.

Nilichojifunza kwa watetezi wa hii sera ya NHC awafahamu right of occupancy ya mikataba ya NHC au public housing yoyote duniani. Wao wanadhani tenants agreement za public housing ni sawa na nyumba za kupanga mitaani. So awawezi ona mfanano wa kuwa treat sawa wapangaji wa NHC na raia waliofidiwa njia ya bomba ni kitu sawa.

Watu wanaongea bila ya kuzingatia mikataba ya NHC si ajabu ata huyo mkurugenzi mwenyewe aelewi rationale ya mikataba yao ni sheria zilizopo kuhusu uendeshwaji wa hilo shirika ndio maana kumtoa Mbowe billicanas ilikuwa mbinde pamoja na madeni aliyokuwa nayo.

Tofauti ni kwamba Mbowe ana hela na public influence ya ku challenge watanzania wengi hawana hizo resources wala mbinu za ku mobilise support and fight their course.
 
Wivu wa kitoto unakusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…