Nehemia Mchechu bila ya ‘speed governor’ ni tatizo. Ndugu zangu wa mitaa ya ‘Al Muntazir’ Upanga mjipange

Bado hatukuelewi.
Wewe unapinga ubia wa NHC au unapinga wapangaji waliokuwa wanaokaa kwenye nyumba za NHC kuondolewa kwenye hizo nyumba bila kufidiwa mahali pengine pa kukaa? Ama unapinga yote mawili?

Ufafanuzi tuliotoa hapa ni kuwa, mpangaji hapaswi kuingilia uhuru wa mwenye nyumba. Wapangaji wa NHC hawana haki wala mamlaka ya kuipangia NHC namna ya kufanya ubia wa shughuli zake za upangaji.

Pili, kisheria upangaji sio jambo la kudumu milele. Muda wa kupanga ukiisha, mpangaji ana haki ya kuondoka na mmiliki ana haki ya kuchukua nyumba yake. NHC wameamua kuchukua nyumba zao baada ya muda wa wapangaji wake kwisha kisheria. Hakuna kosa wala tatizo hapo.

Wapangaji wa NHC watafute mahali pengine pa kwenda kukaa, walishapewa taarifa mapema kuwa upangaji wao utakoma mara moja, mara tu mikataba yao itakapokwisha. Nyumba za kupangisha zimejaa tele mitaani, hakuna uhaba wa nyumba za kupangisha Dar. Ni pesa yako tu.
 
Unajua kwanini for the most part nilikuwa nakwepa hoja zako huna tofauti na Kobello kwenye uelewa wa NHC contracts.

Mfano unazungumzia sijui NHC rent za wapangaji ndogo (rent upanga na mjini ni karibu 1 million a month nyumba nyingi) na wao wakigharamia sijui ABC so wanapata hasara kwenye maintanance ya majengo. Kukusaidia tu kwenye rent za NHC unalipa na service charges so zile gharama ulizokuwa unaongelea zinalipwa na wapangaji sio NHC.

Mikataba inawekwa for short term leases tena utaratibu huo kauleta Nehemia na wala haukuwa standard kama ilivyokuwa kabla yake ambapo ilikuwa mkienda wote mnapewa muda sawa. Alipokuja yeye nyumba A inaweza pewa ten year lease renewal nyumba B block hiyo akienda anapewa 5 years; baadae akaja na maximum ya 3 years or 5 years but renewal has never been an issue to existing tenants.

So mabadiliko mengi unayo yaona kayaleta Nehemia from day 1 kwenye kuwaweka wapangaji roho juu kila uchao.

Kitu cha pili kufanya kabla ata ajafikiria kuongeza nyumba maeneo mapya akaanza kuzunguka prime areas kutafuta nyumba za kubomoa hizo zama za JK kama nilivyo elezea waziri husika akazuia kwa arguments za haki ya makazi ya kuishi kwa kila mtu. .

So hili swala la ubia sasa hivi wanampachikia tena raisi Samia kwa madai ya kuenzi sera zake za PPP, kwani PPP ya NHC lazima iwe mijini tu kwenye prime areas ya mikoa ya Tanzania. Kwanza hilo ndio lengo number moja ya NHC kutafuta maximum profits.

Worst wanavunja hawana hela ya kujenga wao wenyewe, hakuna independent valuation nani kafanya tathmini ya jengo ata moja sure kuna maeneo wana majengo pamoja na ardhi thamani yake inaweza kuwa billioni 10 na kama kanuni zao mwekezaji kujenga inabidi iwe 4 times ya kile kilicho kuwa awali that’s a 40 billion investment ya PPP hizo rent return zake zitakuwaje au ni watu wangapi Tanzania wenye hela hizo za kuchezea.

Ni hivi ili zoezi lote limekaa ki fisadi na kwenye kutekeleza hiyo adhma wapo tayari kuumiza watu huku wakisingizia kutekeleza sera ya raisi.

Good Morning
 
Huyo ndio Kikwete wanayemfagilia kwa shangwe baada ya kufanya yao na hatimae kuwa historia.

Ngoja remote iendelee kufanya yake mkuu!

Magufuli alisema
"Iko siku mtanikumbuka"
 
Let the market forces decide. Hao wakaazi wa Upanga hawawezi kwenda Chànika
 
Msechu ni banker
Anachokifanya ni uwekezaji.

Ili kumuongoza vyema ni kupitia sheria itakayoelekeza aina ya uwekezaji na namna yabkuwekeza kwa kulinda nankujali watu wa hali zote.

Kule Keko flats kuna balaa si dogo. Na jamaa karudi basi wataondolewa wale
 
Una uhakika kwamba kuna ubiya wowote kati ya NHC na hao tycoons.
Kumbuka mchechu ameletwa kimkakati Tu 😀 hapa NHC na msoga jazzy band.
Isije ikawa Hawa ma tycoons Wana taka kujenga ma bagaroh yao ya kuishii na family zao Tu 😀🤣
 
Kitu hujui uwe una tulia. Hata TANESCO wana nyumba za Staffs. Polisi, hivyo hivyo kwa Rais Ikulu. Hivyo hivyo kwa vyuo. Lecturers au Staffs, waki kosa nyumba una mlipa House Allowance kila mwezi kwenye mshahara wake. Mfano inaweza kuwa 15% au 20% ya mshahara wake kila mwezi. Mfano: Professor mwenye mshahara wa Tshs 5m ×0.15= 750,000 kwa mwezi. Ila ukimpatia nyumba chuoni halipwi hiyo. Ina kuwa 0.00. Chuo kina punguza gharama kwa kujenga nyumba na kurahisisha utendaji kazi kwa watu mhimu na ma afisa.
 
Wamasai wamepisha!? Huu ujinga tafuta wajinga wa kuwaambia.
 
Mayor Quimby Nitakujibu hapa hapa hoja zako zote.

Kwanza nimesema ueleweki unasimamia kipi katika hili la NHC. Wewe unapinga wapangaji kuondolewa au unakosoa utaratibu wa NHC kufanya ubia na wawekezaji?

Kuna tofauti kati ya service charges vs maintenance. Mimi sijazungumzia popote kuhusu service charges (ambazo ni jukumu la mpangaji kuzilipa), mimi nimezungumzia maintenance cost (jambo ambalo ni jukumu la NHC kama mmiliki wa jengo), kwa uchakavu wa majengo ya NHC ya zamani, maintenance yake ni kubwa.

Kama wapangaji wa NHC wanalipa kodi kubwa kulingana na uhitaji wa soko la nyumba lilivyo sasa, kwanini hao wapangaji wang'ang'anie kukaa kwenye hizo nyumba? Kwani ni lazima kukaa kwenye nyumba za NHC? Kwani hakuna watu wengine wanaopangisha nyumba? Kwanini sasa wajiite maskini, walalahoi wanaobaguliwa kwa vipato vyao kuwa vidogo? Ni mlalahoi gani anaweza kulipa kodi ya nyumba shilingi milioni moja kwa mwezi?

Mchechu ni Director General wa NHC, anachokifanya ndio NHC wamemtuma au kile NHC wanachokifanya ndicho ambacho wametumwa na Mchechu kukifanya, na kama anakosea basi aliyemuweka ndio ana wajibu wa kumuwajibisha. Hivyo huwezi kumlaumu Mchechu kwa kusimamia sera na miongozo ya NHC kuhusu sera ya ubia katika kujenga nyumba kwa sasa.

Kuhusu mikataba kuwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine, hilo sio jambo la ajabu au jipya katika issue za mikataba. Kila mpangaji wa NHC anapangishwa yeye binafsi katika nyumba mahsusi. Na mkataba huwa unaweza hata kuwa siri ya watu wawili tu, yaani mpangaji mmoja na NHC, huwezi kulazimisha mkataba wako na NHC ufanane na mkataba wa mtu mwingine na NHC. Katika mazingira ya kibepari, utofauti wa kimikataba ni jambo la kawaida sana.

Kuhusu utaratibu unaotumika na NHC kufanya ubia wa kujenga majengo mapya, hilo liko ndani ya mamlaka ya NHC, mpangaji wa NHC hahusiki nalo. Sote tunaweza kuhoji, kuukosoa au kuupinga kama watanzania wengine lakini sio kwa sababu sisi ni wapangaji tunaokwenda kuondolewa kwenye hizo nyumba mikataba yetu ikiisha.
 
Mfano, yale Maghorofa ya pale "faya". Naona ni aina fulani ya uchafu usiostahili kuwepo pale miaka hii aisee.
 
If he is your role model, it's obvious you wouldn't have said the otherwise.
 
Shirika likishakuwa linaendeshwa kiujanja ujanja hiyo mnayodai mikataba itakuwa inachezewa kila kukicha na hao wenye hela za rushwa.

Mathalani, mkataba wangu ukikaribia kuisha, naweza kunyimwa kuendelea kupanga kwa sababu za uongo na kweli, kisha kesho akapangishwa mwingine, kwa kuwa tu alitoa kitu kidogo ili mimi nitolewe na akae yeye.
 
Inawezekana vipi, mkataba wangu na wa jirani yangu tuliopanga apartments za aina moja utofautiane kwenye kiasi cha kodi tunacholipa!? Huoni huu utakuwa ndio mwanzo wa rushwa!? Kwamba mpangaji anaweza toa rushwa ili apewe nafuu kwenye kodi!? Hii haikubaliki.
 
NHC Kuna wengine hawalipi.
 
Mche
Wengi zilikuwa zao walidhulumiwa pili kwanini tusiwe na old town tubuni prime areas nyingine Nne je system ya maji chini????? Ect….
 
Dawa ni kumfungulia kesi mahakamani kupinga na hapo mengi ya huyu jamaa yataibuka
 
Kuhusu swali lako naongelea kitu gani hasa kwa wewe kutofautisha model ya uwekezaji wanayotaka kufanya na uhalali wa right occupancy kwa wapangaji kutotolewa kiholela (ni sawa na kuuliza unaongelea picha ya mwenge au Nyerere kwenye shilling, topic ni shillingi yenyewe so vyote ni kitu kimoja).

Ni hivi uwezi fanya investment dunia ya leo bila ya kuzingatia ‘corporate social responsibility’ bila ya hata kuwa na sheria huo ni wajibu wa kitaasisi dunia ya leo.

That is to say uwezi kutoa watu ovyo bila kuwa na mikakati ya re-housing hizo sio nyumba za kupanga kama zile za mtaani. Biashara kubwa zipo bound na ethics na as well kuna sheria za kuendesha shirika.

Moreover like I said before arguments zako ni za jumla nyumba za NHC kodi inakuwa set by several factors aina ya nyumba, square meter, eneo and so forth. So nyumba zinazofanana rent inatakiwa kuwa sawa.

Ni hivi kama unatetea huo uwekezaji na uozo wa NHC walau elewa hilo shirika linavyofanya kazi na taratibu za uwekezaji; personally leo nina homa kidogo vinginevyo ningetafuta sheria inayolinda right of occupancy kwa wapangaji wa NHC, hiyo sheria aiwahusu wapangaji wa private.

Enjoy ya weekend and stay blessed ila hiko wanachotaka kufanya NHC ni wrong in every way na hakuna serikali itaachia unyanyasaji au irresponsible approach ya shirika zaidi ya Tanzania.

Alamsiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…