Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Bado hatukuelewi.Ipo siku watu kama nyie mtasema polisi iache kuangaika na panya road uswazi kwa hoja za kwamba kwanza ni watoto waliokulia huko huko kwa ivyo ni matatizo ya malezi ya ovyo huko wacha yawakute.
Halafu hayo maeneo yenu nyumba zenu zinawalinzi wa security companies tena mnawalipa kwa mishahara inayotokana na kodi hizo hizo za hao wa uswazi mnaodai panya road ni tatizo la malezi yao.
Hakuna serikali makini itakayo kubali aina ya ubia NHC inayotaka kufanya duniani si business model ya shirika lolote la nyumba duniani, na uwezi kuweka mfano wa mtu mwingine yeyote aliefanya icho kitu.
Ni hivi hilo jambo sio rahisi morally ndio maana hakuna serikali yoyote itakayo support labda ya Tanzania tu.
Hakuna shida kubomoa baadhi ya nyumba lakini hekima ni kuwatafutia wapangaji sehemu kwanza, ivyo ndivyo watu wanafanya mambo ata kama hayapo kwenye sheria za nchi; it’s canon law.
Only in 1920’s watu walikuwa wanaweza fanya hayo mambo kwa ethics za leo ata hizo central control economies kama China awawezi fanya ivyo; it’s just immoral.
Wewe unapinga ubia wa NHC au unapinga wapangaji waliokuwa wanaokaa kwenye nyumba za NHC kuondolewa kwenye hizo nyumba bila kufidiwa mahali pengine pa kukaa? Ama unapinga yote mawili?
Ufafanuzi tuliotoa hapa ni kuwa, mpangaji hapaswi kuingilia uhuru wa mwenye nyumba. Wapangaji wa NHC hawana haki wala mamlaka ya kuipangia NHC namna ya kufanya ubia wa shughuli zake za upangaji.
Pili, kisheria upangaji sio jambo la kudumu milele. Muda wa kupanga ukiisha, mpangaji ana haki ya kuondoka na mmiliki ana haki ya kuchukua nyumba yake. NHC wameamua kuchukua nyumba zao baada ya muda wa wapangaji wake kwisha kisheria. Hakuna kosa wala tatizo hapo.
Wapangaji wa NHC watafute mahali pengine pa kwenda kukaa, walishapewa taarifa mapema kuwa upangaji wao utakoma mara moja, mara tu mikataba yao itakapokwisha. Nyumba za kupangisha zimejaa tele mitaani, hakuna uhaba wa nyumba za kupangisha Dar. Ni pesa yako tu.