Nelson Mandela alihalalisha uporwaji wa Ardhi ya Afrika Kusini kwa Boers halafu anaitwa Baba wa Afrika. Afrika tumerogwa na nani?

Nelson Mandela alihalalisha uporwaji wa Ardhi ya Afrika Kusini kwa Boers halafu anaitwa Baba wa Afrika. Afrika tumerogwa na nani?

Kuna watu wana akili za ajabu sana,wao hutaka maendeleo na mafanikio kwa kufa au kudhurika kwa wengine
Tarehe 20 Aprili 1964, akiwa na umri wa miaka 45, akiwa tayari anatumikia kifungo cha miaka 5, kilichoanza 1962, alisimama kizimbani katika kesi iliyojulikana kama kesi ya Rivonia, Mandela alikiri kuwa alikuwa mmoja wa waasisi wa Umkhoto we Sizwe na kuwa alihusika katika juhudi za ku sabotage utawala wa makaburu. Alisema hivyo akijua thika kuwa anaweza kuhumiwa kifo. Lakini aliwaambia makaburu kuwa yote tayari kufa kwa ajili ya imani yake. Akahumiwa kifungo cha maisha. Kwa miaka 18 ya kifungo hicho alipasuwa mawe, alilala kwenye sakafu na alikuwa kwenye selo isiyokuwa na choo. Na kwa muda wote huo hakutetereka katika imani yake. Mwaka 1985 Mandela alikataa ofa ya kuachiwa kutoka jela kwa sharti la kuacha shughuli za ukombozi. Alibaki jela mpaka 1990.
Alipotoka jela alikuta kuna mapambano makali kati ya ANC na Inkatha Freedom Party cha Chief Buthelezi. Mandela akamfanya Buthelezi Waziri wa Mambo ya Ndani. Na alimuachia nchi mara 22 kama acting President.
Ingawa alikuwa na uwezo wa kuendelea kuwa Rais, Mandela alikataa kugombea na mwaka 1999 akaachia urais.
Wakati viongozi wake wenzake wanakataa uwepo wa Ukimwi, Mandela alisema wazi kuwa mwanae alifariki kwa ukimwi!
Kwa kumshutumu Mandela kwa kuwauza watu wake, kunaonyesha wazi msivyoijua historia ya huo uafrika mnaojifanya kuutetea.

Amandla...
 
Mleta mada na watu wa namna yako ni wapuuzi sana, Kwahiyo mulitaka SA iwe kama Zimbabwe?
Acha upuuzi wako wewe mbilikimo wa akili..

Harakati za kudai ukombozi huko South Afrika zilikuwa ni za kumtoa jela Mandela kwa gharama ya damu na ardhi ya watu wake?

Angola,Msumbiji na Nchi zingine zilidai haki yao ya Ardhi badala ya uhuru wa bendera kama wa South Africa na Zimbabwe..

Zimbabwe imefeli kwa sababu hawakudai haki sawia wakati Mugabe anapewa uhuru wa bendera kama Mandela ,so walivyokuja kunyakua kwa nguvu ndio wameharibikiwa ila wangenyakua from bugging wala wasingekuwepo walipo sasa.
 
Mugabe aliwanyang'anya ardhi wakoloni na kuwapa waafrika wenzake. Idi Amin aliwanyang'anya wahindi biashara zao akawapa waafrika wenzake na akawafukuza nchini. Sasa hivi wazimbabwe wako tayari kuishi maisha duni Afrika ya Kusini kuliko kubaki kwao. Museveni alipoingia madarakani aliwaangukia wahindi waliofukuzwa ili warudi na waendeshe mashamba na biashara zilizoporwa. Sisi wenyewe tuliwanyang'anya nyumba na biashara za wahindi lakini mwisho wa siku tukawarudishia kimya kimya.
Mandela anastahili heshima anayopewa.

Amandla...
Unasema hivyo sababu unaweza kununua kiwanja dar es sallam au arusha au mwanza ai mikocheni ili mradi pesa yako. Wenzio weusi huko SA hawaruhusu hata kudhuru fukwe za miji wanayoishi makaburu.
 
Duh kwa ambavyo nimekua namkubali Mandela, mngesubiri kizazi chetu kiondoke kabla kuanza kumsema...
Wengi wanamkubali kwa hisia tu. Mandela aliyeingia jela si mandela aliyetoka jela.

Sawa na mbowe aliyetoka ikulu si mbowe aliyeingia ikulu.
 
Mugabe aliwanyang'anya ardhi wakoloni na kuwapa waafrika wenzake. Idi Amin aliwanyang'anya wahindi biashara zao akawapa waafrika wenzake na akawafukuza nchini. Sasa hivi wazimbabwe wako tayari kuishi maisha duni Afrika ya Kusini kuliko kubaki kwao. Museveni alipoingia madarakani aliwaangukia wahindi waliofukuzwa ili warudi na waendeshe mashamba na biashara zilizoporwa. Sisi wenyewe tuliwanyang'anya nyumba na biashara za wahindi lakini mwisho wa siku tukawarudishia kimya kimya.
Mandela anastahili heshima anayopewa.

Amandla...
Hujamalizia mwambie hao viongoz wote waliopora mashamba na Mali za wazungu walikuwa na mwisho mbaya Sana
 
Kabla ya kumlaumu mtu hata kama waona una haki jaribu hata kidogo kuvaa uhusika au viatu vya huyo unaayemlaumu then ndio uendelee kumlaumu..
~Anonymous
 
Usikimbilie kutukana jibu hoja,uchawa wako Kwa Samia anakutoa ufahamu unatukana kila anayemkosoa.
Rotten mind,kuna hoja gani hapo?

Anzisha hiyo mnayoita mada tutakuja kujibu,hapa tuko kwenye mada ya Mandela aliyewauza watu wake Ili atoke jela.
 
Habari hizi zina fikirisha Sana.

Mara kadhaa nimekuwa nawaza Sana na nakosa majibu muhimu.

(1) Mandela aliifanyia nini Afrika kuzidi akina Nyerere mpaka jina lake lionekane lipo ju zaida ya wengine??

(2) Mandela alikubali vipi kuona wazungu wamegawana aridhi na rasilimali asili za Nchi hiyo? Ambapo mpaka sasa waafrika wengi maisha yao ni mabovu kuliko wazungu.
 
Hakuna rais mpigania Uhuru mpumbavu kama Mandela. Yes you read it correctly.
Mugabe did the same. Akajirekebisha 2007. Wakamwekea vikwazo. Yule Mandela akapewa birthday London FiFa World Cup ili aendelee kuwaacha wazungu.

It will take bloodshed for black South Africans to regain their land which they lost since 1652.

After 50 yrs from now, drunkard will be urinating on Mandela's grave.
Too harsh...

Miaka 27 gerezani sio kitu kidogo, isitoshe baada yake wamepita marais weusi kama 3, kwanini hawajapigania hiyo ardhi?.....ilikuwa lazima kazi zote azifanye peke yake ?

Kwanini yeye ndiye awe wakubeba lawama ?
 
Ilikuaje akawauza wenzio from all such sufferings?

Narudia tena kuna waliokufa kwa ajili ya harakati ,kwa nini auze Nchi Ili tuu atoke jela?
Alikuuzia wewe? Kama nia ilikuwa ni kutoka jela angetoka 1985 lakini alikataa. Alitoka 1990 baada ya De Klerk kukubali utawala wa walio wengi.
Muwe na adabu.

Amandla....
 
Kwa wakati ule alikuwa sahihi kwani hata angekomaa wazungu wakaacha ardhi bado wangeweza kumkwamisha kama yaliyotokea Zimbabwe.
Ila Sasa nadhani ni muda muafaka wa kuwa na mazungumzo ya kitaifa ili wazungu waachie baadhi ya ardhi wapewe weusi japo hii rangi yetu sidhani kama wataifanyia lolote.
 
Back
Top Bottom