NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

Asante sana Mkuu kwa kuwa mkweli.
 
DARUBINI

Ukiangalia nje ya box hili jambo kuna KITU

Hivi hivi kwa macho ya UNYONGE huwezi ona......
 
Acha upotoshaji usimuusishe Rais na makosa ya wafanyabiashara wa bar wasiozingatia sheria za Baraza la mazingira (NEMC) kwa kuwa yeye ni Mwiislamu wala hana hizo habari za bar kufungiwa labda aone kwenye tv, unakumbuka ile issue ya Mufti kutaka mali za Waisilamu zirejeshwe Rais Samia akamjibu siwezi kuzirejesha hizo mali kwa kuwa mliziuza wenyewe kihalali, kama angekuwa mdini angefanya kama alivyotaka Mufti kwakuwa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo anayo ila kwa kuwa anaheshimu utawala wa sheria akakataa kumsikiliza Mufti.
 
Leo wanafungia Mziki kesho watafungia Pombe kwa madai kuwa ni haramu.
 
kwahyo unataka kufananisha adhana ya dakika 2 na makelele ya walevi mpaka usiku wa manane, mkuu una uhakika umekula mlo kamili mchana?.
Tena adhana ni hatari kwa afya, wanatumia honi spika inasikika hadi kilomita 3, inashtua kuliko hadi muziki wowote
 
Acha kutia HURUMA, sheria ivunjwe kisa wakale wap!?
 
huku Mkuu umaskini ndo MTAJI




Na kweli mkuu
Kama wakitokea wabunge 20 wenye msimamo mmoja waadilifu (sidhani kama wapo)
Labda baada ya miaka
Lakini mtu mmoja kuwanyoosha watamlia timing tu na kummaliza

Kweli umasikini mtaji
 
This comment should be laminated.
 
Ukiona operation nzito inatekelezwa na Nemc basi juwa sauti hiyo ilitoka Baraza la Mawaziri ama kwenye chumba cha mwenye Nyumba🤐
 
Fuateni masharti acha kelele zisizo na msingi.
 
Hilo ni jambo jema sana NEMC wanafanya, wakumbuke na kelele za stendi za magari, wahubiri kwenye magari na nyumba za kidini zinazojengwa kiholela pia.
Hapo ndio ntaamini wako serious
 
Subirini PRESS CONFERENCE ya Waziri mwenye dhamana. Kukanusha. Maana wapiga kura watakula wapi bila mikelele?
 
Hatutaki makelele kwenye makazi ya watu,
 
Nemc kazeni uzi, walevi hawaendi kunywa muziki wanakunywa pombe, kama wanashida na muziki siku hizi kila mtu ana muziki, TV na kila burudani kiganjani mwake, mambo ya kulazimishana kusikiliza muziki majumbani mwetu yamepitwa na wakati
 
Huna hoja.

Bar lazima waweke mziki wa juu?

Kama mnataka muziki wajuu jengeni bar nje ya mji pasipo makazi ya raia.

Wananchi pembezoni mwa bar wanateseka sana.

Katika hili niko na serikali
Vipi Makanisa yaliyo bize siku zote
 

Ni kama hauna hoja zaidi ya majungu na taarifa za kupika.

NEMC mpaka wamefikia hatua ya kufunga bar washazunguka sana kutoa elimu sehemu mbalimbali.

Uko na wateja wako ndani ya bar hapo hapo lakini unafungulia mziki usikike mtaa wa tatu ili iweje?

Acheni upuuzi lazima tufike mahala kama nchi tusitaarabike sio kupigiana makelele kila sehemu
 
Naomba kujua kama umejenga baa nje ya mji na raia wakaja kujenga hukohuko hapo kosa ni la nani?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…