NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

100%
 
Sasa baa na sanaa vikiangamia kuna ubaya gani? Vyote ni vitu vya haramu acha viangamie. Ni sawa kabisa.
 
Nasikia watu wakisema Tanzania ina mapori mengi sana, wafanyabiashara wa Bar kama hawawezi kudhibiti kelele za muziki na walevi wahamishie Bar zao huko maporini mbali na makazi ya watu.
Na nyie mtaamia hukohuko ili mkilewa msiteseke kufika nyumbani bado litakua kosa tena

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
  • A good move.
  • Bado makanisa na misikiti.
  • Kwa idadi hii ya watu na ukuaji wake, bila udhibiti itaonekana kama kambi ya vichaa
 
watu wenye akili yakuona mbaali. tumeshabain nini kimelegwa kufutwa

1. Makanisa. mengi saana yamelegwa kufugwa. hiii ikimaanisha kwamba nchi hiii itakuwa nadin. roman, usabato na uisilam tuu katk nchii.

2. wamelenga kudhooofisha raia ili iwe rahisi. kutawala. coz raia wanatakiwa kuwa masikin. watawaliwe kirahis

3. wamelenga hasa watu wanaotoka Kanda ya ziwa, na kati waondolewe kwenye system kabisaa. Ili watu. wapwani na waisilam ndo watamalaki kati nchi

4. teuzi zijazo. wakristo wataondolewa saana kwenye nafasi nyeti. hii nikampeni. nadhani yakugauza nchi hiii kuwa ya kiislam watanzania tuamke. nchi inaenda kugawanye nakusambalatishwa kidin. mtakumbuka. tumeshamalizana
 

Mtoa mada yuko subjective na si objective.
 
Mto mada umekosea sana.

Tambua haya
1. Nini maana ya noise pollution (Uchafuzi wa Sauti) na athari zake
2. Sheria inasema nini juu kiwango cha Sauti kinachotakiwa zaliswa katika au kutoka eneo fulani (Makazi, Sehemu za Biashara na Sehemu za Viwanda) kwa wakati fulani (usiku au mchana)
3. Wazalishaji wa sauti ni kina nani? (Bar, Makanisa, Magari, majumbani n.k)
4. Waathirika ni Akina nani (watoto, wazee, wasiokunywa pombe, wanafunzi n.k)
5. Nini wazalisha sauti wanatakiwa kufanya (funga sound proof)

Serikari haijawafungia kisa haitakiwa wafanye biashara, imewafungia sababu wameshindwa funga sound proof na wanazalisha kiwango cha sauti kisichotakikana na sheria.

Serikari haitafungia Bar tu itafungia hata makanisa na nadhani huu ni mwanzo tu.

Pia kumbuka Bar wanaenda wanywa pombe.. wakishakunywa wanapata tatizo la kusikia (hearing loss) hivyo wataanza ongea kwa sauti na watataka mziki wa juu. Wakirudi majumbani mwao wamelewa hata huo mziki unapigwa Bar ya jirani hawausikii tena.

Sasa fikiria mtoto, bibi, mwanafunzi mgonjwa n.k asiyekunywa ambaye ubongo wake uko active masaa yote anaumia vipi na sauti.

Ukija kwa makanisa, wale nao shida sana maana nao hawatofautiani na walevi. Wakishapandishana Mizuki basi nao ugeuka viumbe wa ajabu wasiowajari wenzao. Hupiga makelele, mziki juu. So serikari iko sahihi kabisa kufungia bar na makanisa yanayozalisha uchafu wa sauti.

Fanya rejeo la sheria linasemaje hapa
 

Attachments

Tuvumiliane angalau tufikie uchumi WA juu WA kati, kelele zipo Kila mahali na zote kwa sababu ya njaa
 
NEMC safi sana, narudia kusema Safi sana. Naiomba tu Serikali na wanasiasa msije kuleta siasa katika jambo jema kama hili, maana hii nchi unaweza kusikia mwanasiasa au Mbunge anaanza kutafuta Kiki kwa kukosoa huu uthubutu wa NEMC. Naomba Mhe Spika akitokea mbunge kuanza kuleta siasa za kukwamisha juhudi za NEMC ita askari wamtoe nje ya Bunge.

Nimekumbuka jinsi siasa zilivyotaka kukwamisha suala la kuwaondoa wamachinga barabarani. Leo hii angalau miji inaonekana tofauti na ilivyokuwa unakuta nyanya zimepangwa barabarani na chips zinauzwa katikati ya Round About.

Neno la leo :
Mama yetu amekuja na Baraka nchi hii hadi Yanga imeingia nusu fainali
 
Wanaokunywa Pombe zanzibar si Waislamu, wamehusianaje na shehe?
Wacha zako wewe.
 
Zanzibar wao hunywa pombe wakiwa wamejifungia vyumbani kwa kumuogopa shehe, sisi hapa Tanganyika tunakula Gambe na Mziki na shehe mwenyewe anajumuika.
Wanaokunywa Pombe zanzibar si Waislamu, wamehusianaje na shehe?
Wacha zako wewe.
 
Mkuu tusiingize siasa kila jambo.
Muziki wa juu unatesa sana raia karibu na bar.
Unasababisha hadi presha kwa wazee.

Hebu fikiri una mgonjwa ndani halafu muziki uko juu hadi kuta za nyumba zatetema
Au una mtoto mchanga. Mziki unadunda hadi mtoto anataka kutokwa roho. Mtoto anakua kwenye zile kelele, mwisho Wa siku ubongo haujengeki. Tunaishia kuwa na chokora na vibaka wengi kumbe ni watoto walioathirika bongo zao.
Shuleni wanataka watoto wafanye vizuri. How? Wakati mtoto akili haiko sawa?!
 
 
Ujengewe sanamu lako mrembo
 
Sauti yoyote, iwe ya muziki, hotuba, au hata mazungumzo baina ya watu, ikizidi kiwango fulani inaashiria ukosefu wa akili nzuri au uwendawazimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…