Rais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!
Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!
Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu Pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!
NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!
NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya Dar.
Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?
Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?
Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?
Mto mada umekosea sana.
Tambua haya
1. Nini maana ya noise pollution (Uchafuzi wa Sauti) na athari zake
2. Sheria inasema nini juu kiwango cha Sauti kinachotakiwa zaliswa katika au kutoka eneo fulani (Makazi, Sehemu za Biashara na Sehemu za Viwanda) kwa wakati fulani (usiku au mchana)
3. Wazalishaji wa sauti ni kina nani? (Bar, Makanisa, Magari, majumbani n.k)
4. Waathirika ni Akina nani (watoto, wazee, wasiokunywa pombe, wanafunzi n.k)
5. Nini wazalisha sauti wanatakiwa kufanya (funga sound proof)
Serikari haijawafungia kisa haitakiwa wafanye biashara, imewafungia sababu wameshindwa funga sound proof na wanazalisha kiwango cha sauti kisichotakikana na sheria.
Serikari haitafungia Bar tu itafungia hata makanisa na nadhani huu ni mwanzo tu.
Pia kumbuka Bar wanaenda wanywa pombe.. wakishakunywa wanapata tatizo la kusikia (hearing loss) hivyo wataanza ongea kwa sauti na watataka mziki wa juu. Wakirudi majumbani mwao wamelewa hata huo mziki unapigwa Bar ya jirani hawausikii tena.
Sasa fikiria mtoto, bibi, mwanafunzi mgonjwa n.k asiyekunywa ambaye ubongo wake uko active masaa yote anaumia vipi na sauti.
Ukija kwa makanisa, wale nao shida sana maana nao hawatofautiani na walevi. Wakishapandishana Mizuki basi nao ugeuka viumbe wa ajabu wasiowajari wenzao. Hupiga makelele, mziki juu. So serikari iko sahihi kabisa kufungia bar na makanisa yanayozalisha uchafu wa sauti.
Fanya rejeo la sheria linasemaje hapa