NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

NEMC wamedhamiria kuua baishara ya baa na sanaa kwa ujumla. Baa itaendeshwa vipi bila muziki? Liquid Bar wamezuiwa kupiga muziki

Mkuu huyu Maza anataka kufanya "Nanny State".
Enzi ya Nyerere bendi zilipiga muziki open bar ...ni Bayankata majogooo mpaka Lyamba

Wapiwapi Chang'ombe Bar......burudani Ijumaaa Jumamosi Jpili

Ndekuleee Njatanjata Msondongoma Sikindeee Paselepaa KumbaKumba....VangaVanga ....Kamanyola....KimbungaJKT....
 
Ungekuwa pengine .wanafunzi wa chuo na unakaa mtaa wenye baa kaq hiyo na unahitaji utulivu wa kujisomea nadhani ungepongeza zuio hilo,hata mimi nalipongeza NEMC sio wapumbavu mpaka wachukue hatua hiyo na ni sehemu ya majukumu yao.Naona umeamua kulaani ukiwa umeegamia upande mmoja.Je ulifanya utafiti hata kidogo kujua ni kwasababu gani wamefungiwa kupiga mziki?
 
Dawa ni kwenda kufungua Cornerpub Chamwino karibu na Ikulu ili tuwe tunakutana pale na Mziki mpaka asubuhi.
 
NEMC wako sahihi. Moto sasa uelekee makanisani. Kelele ni mbaya
 
Twambie sheria inataka bar zikae wapi? Na kwa sheria hipi? Kwanini imeanza leo? Bar zimeanza kupiga muziki leo?
Acha ujinga! Unapokwenda

halmashauri kuomba kiwanja kwa ajili ya ujenzi unaonyeshwa wazi maeneo ya makazi, makazi na biashara, biashara viwanda nk. Na kila eneo lina masharti yake hivyo ni jukumu lako kuchagua.

Majibu kwa maswali yako:

i) Bar zinatakiwa zikae maeneo ya makazi na biashara kwa masharti ya Mipango miji.

ii) Sheria za makazi za Mipango miji na mazingira ndizo hasa zinazohusika.

iii) Sheria zimeanza kutumika muda mrefu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi na wadau kwa ujumla. Hivi sasa serikali imejiridhisha kuwa elimu imetolewa vya kutosha na hivyo kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaokaidi.

iv) Bar zimeanza kupiga muziki zamani hata kabla hujazaliwa lakini si kigezo cha kuendelea kuvunja sheria na kukera wengine.

Majibu yako ndiyo hayo
 
Waweke viwango vilivyoruhusiwa kisheria(Decibel) ,usiangalie upande mmoja ,angalia pia upande wa wagonjwa ambao hawahitaji makelele.
 
Inashangaza unalilia kelele, bar nyingi zimewekwa katikati ya makazi ya watu. Kuna magonjwa yasiyotaka mishtuko, kuna watu kwenye kelele hawalali. Kuna wanafunzi wanahitaji kujisomea.

Mbaya zaidi hizi bar wengine wamewekeana karibu, kwa maana hiyo wanashindana nani muziki wake utasikika zaidi. Wafikirie na watu wengine wanaoishi jirani. Wafanye utaratibu muziki uwe wa wastani usiokera wengine.
Bar kuwepo makazi ya watu hakuna ubaya, tatizo ni miziki.

Mbona Mbezi Makonde kuna Bar EB25 haina kelele, Triple 7
 
Cha kushangaza makanisa yanayopiga kelele ni mengi kuliko bar
Waraka wa nemc unawahusu hata nyumba za ibada isipokuwa katika miito ya ibada, kengele na adhana tu.
 
Polepole mwishowe watasema Pombe haramu kwa sasa wanaanza na Mziki sasa hivi mnaambiwa ni MEMC baadae mtajua ni BAKWATA.
 
Rais Samia kupitia NEMC umeaamua kuuwa baishara za watu na kuuwa biashara za watu ni sawa na kuuwa watu kabisa!

Mh Rais wewe na wasaidizi wako mnakula raha kila siku na mko angani kila siku mnakula asali lakini sisi wananchi wengine burudani yetu ni muziki lakini mmeona tunafaidi sana ndio maana sasa mnaitumia NEMC kuhakikisha mnatupora hata hiki tulichobakiwa nacho!

Mh ukiwasikiliza baadhi ya wamiliki wa bar utagundua kabisa NEMC sasa hawana tofauti na TRA wanao funga biashara za watu…pia ni wazi kabisa hata wamiliki wenyewe hawajui kabisa hicho kipimo cha kelele badala yake wanashitukizwa na kuambiwa muziki umezidi kiwango hivyo wanafungiwa bar zao na biashara!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wanazifungua baadhi ya bar na kumbi kutokupiga muziki kabisa…kupitia EFM nimewasikia baadhi ya wamiliki wa bar wakieleza kwa uchungu jinsi ambavyo wameharibiwa biashara zao!

NEMC wamekwenda mbele zaidi wamezifungia kabisa baadhi ya bar kupiga muziki kabisa ikiwemo Liquid bar ya Dar.

Hivi kweli bar gani itaendeshwa bila muziki nchi hii? Mama Samia hawafanya biashara mnataka wakale wapi? Wataishi vipi?

Hivi kwanini mnataka kuigeuza nchi hii ni ya kidini?

Jamani pesa za serikali mnazitumbua peke yenu na hakuna anayewafanya chochote sasa mnatuzuia hata sisi kuburudika na muzuki? Mnataka tukaishi wapi?
we mshamba nenda kajifunze kwa wenzako waliostaarabika. Bila hata haya unakuja kuandika huu upumbavu? Huna adabu, starehe zako ziwe kero kwa wenzio na baada unaona ni sawa, ubinafsi wa kiwango huo? Kwa ufupi mkaheshimu haki za wenzenu na mkatii heria bila shuruti. Serikali imechelewa sana kuchukua hatua nawapongeza sana waendelee bila kukatishwa tamaa na mapoyoyo km haya. Haki yako inaishia pale inakoanzia haki ya mwenzako/wenzako.
 
Tena wafungiwe maisha kama hawatajirekebisha
Unapigaje mziki kama kichaa, sauti mtaa mzima
Wanaona mziki mkubwa ndio unauza pombe zaidi hawajui wanaathirika watu kwa kelele hizo na wengine wanashindwa hata kulala?

Tena waende mbali zaidi mpaka wenye mabasi waandikiwe barua za warning [emoji3544] kabisa maana ni madereva wavuta bangi na walevi wa gongo ndio wasumbufu zaidi

Weka mziki kwenye gari lako ila public services za nini?

Mhubiri nae anapiga kelele bila kujali nani anamsikiliza mradi apayuke tu

Huku nako machinga kaweka lispika kuanzia asubuhi mpaka jioni yeye ni kubadili batteries tu kelele mpaka tunakariri maneno

Kweli kutembea unayaona mengi
Upumbavu huu nchi zingine huwezi kusikia kabisa
Ukimya mpaka raha
 
Huna hoja.
Bar lazima waweke mziki wa juu?
Kama mnataka muziki wajuu jengeni bar nje ya mji pasipo makazi ya raia.

Wananchi pembezoni mwa bar wanateseka sana.
Katika hili niko na serikali

Wakati wanatoa kibari na kudai Kodi walikuwa hawajui kama hiyo bari ipo kwenye makazi ya watu
 
Nchi ina wajuaji wengi wanaonuka umasikini na wivu wa kutosha.

Wasichojua tunategemeana sana...

Unafunga bar Lakin TRA wanadai VAT returns ya 18% bado SDL na Takataka kibao...

Kelele kwa baa hapana., ila kwa maspika ya makanisa sawa..

Nchi ina mamlaka zaid ya 40 na zote zinasimamia kitu kimoja.

Wazue na makelele ya saa 11 alfajiri watu wakiwa wamelala
 
Back
Top Bottom