NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

Hata mimi NEMC nashangaa kwanini wanachukua muda mrefu kuweka utaraibu wakati ni suala la kutamka tu na kumaliza kazi. Wawaelekeze wenzetu wawe wanatumia alarm kuwambusha muda wa ibada unapofika badala ya kutupigia mikelele yao kila alfajiri tunashindwa kulala.
Mkuu alfajiri ni mda wa dakika mbili ila kuna wale wanapiga kelele usiku mzima au zile speaker za wauza dawa na mitumba

Yaani kuna kelele hazivumiliki na kama wakisema wadhibiti adhana wataomba na kengengele za jumapili zipigwe marufuku
Naona Ibada ziwepo ila sio zile za karaha

NEMC hawana meno na sio hao tu hata mahakama na kila sehemu sheria ni ngumu kuzifuata
 
Hata mimi NEMC nawashangaa kwanini wanachukua muda mrefu kuweka utaraibu wakati ni suala la kutamka tu na kumaliza kazi. Wawaelekeze wenzetu wawe wanatumia alarm kuwambusha muda wa ibada unapofika badala ya kutupigia mikelele yao kila alfajiri tunashindwa kulala.
Shauri hiyo alama iweje???
 
sheria zipo lakini serikali inaogopa kuwagusa hawa jamaa maana wanapenda shari hatari.
 
uonyesha chuki kabisa yaani😅😅,Kuna kumbi za starehe kibao watu hawana time kila mtu na maisha yake...Hata majirani watu wanapiga mziki kivyao.

Kuna vibes la vibanda umiza hata uwanja wa taifa kila mtu na starehe yake.

Tatizo lako unatokea kijijinj sana siwez kukulaumu.
 
Hapa mtaani,Kigamboni kwa Steven kuna hili kanisa hatujawahi kulala jamani, Wanapiga mziki mkubwa na kukemea mapepo hadi saa 12 alfajir na wanaona wako tu
Kanisa gani hilo mkuu? Kama ni la kilokole hama hapo. Walokole nao wakiamua kusali wanasali 24/7 hata hawakumbuki kwenda kufanya kazi za maendeleo. Wanaambiwa kila kitu watakipata kutoka kwa Mungu kama ile mana ambayo Mungu aliwateremshia wana wa Israel.
 
Mmeona muziki wa baa umekula kibano mnataka na nyumba za zifungiwe shangwe na ibada zao za kupaza sauti? Hapo mjipange hajatokea wa kuzima shughuli za ibada huko. NEMC wakashughulike na uchafuzi wa mazingira kwingine, kwenye nyumba za ibada watachemka. Kwanza watu wa ibada zingine wamewaelewa na wanachukua tahadhari kabla ya NEMC kuwaibukia wameamua kwa hekima na busara ya kiungu kupunguza sauti ya maspika yao ili wasiwe kikwazo kwa wengine. Hao wengine inategemea wana hekima na busara gani kupunguza kelele za sauti za maspika yao. Ni suala la hekima tu kutii mamlaka
 
uonyesha chuki kabisa yaani😅😅,Kuna kumbi za starehe kibao watu hawana time kila mtu na maisha yake...Hata majirani watu wanapiga mziki kivyao.

Kuna vibes la vibanda umiza hata uwanja wa taifa kila mtu na starehe yake.

Tatizo lako unatokea kijijinj sana siwez kukulaumu.
Wala sio mimi mkuu.....ni NEMC ndiyo walioahidi kukomesha kero hizi lakini naona kama wanachelewa kuja. Kelele zimezidi sana hapa mtaani watu hatulali wala kushinda kwa utulivu. Ni kero mwanzo, mwisho!
 
sheria zipo lakini serikali inaogopa kuwagusa hawa jamaa maana wanapenda shari hatari.
Sio ukorofi bali Sala zilikuwepo miaka yote na hakuna sheria inasema adhana marufuku
Kwa hilo la ibada haliwezi kupigwa marufuku, hilo kila mmoja anajua

Wengi wanaamka mapema sana na kwenda kutafuta riziki alfajiri kwa hiyo kuamshwa ni sawa tu

Kama kelele zinakatazwa basi zianze na bar zinazotoa sauti mpaka mtaa wa pili tena usiku na mchana

Kuna kelele zisizokuwa na ukomo
 
Shauri hiyo alama iweje???
Waumini karibu wote wanamiliki simu. Alarm zipo kwenye kila simu. Wawe wanaset hizo alarm kwenye simu zao muda ukifika zinalia na kuwaamsha kwenda ibadani badala ya kutumia maspika yanayochafua hewa mtaa mzima.
 
Mkuu wakat unajenga mitaa hyo uliyakuta hayo makanisa au makinisa yalikukuta ww!!tuanziee hapo
Hayakuwepo, yamenikuta mkuu. Mpaka natamani kuuza nyumba nihame hapa lakini bado sijapata mteja. Ukipata mteja mwenye 80M nishtulie aje anunue hii nyumba mm nihame mkoa, hata ikibidi nirudi kijijini kabisa.
 
Hayo makanisa yanayokesha dawa ni kuwanunulia spika kubwa na kuwawekea singeli.

Kuna wakati wa kila kitu, Mungu hakusema twende kanisani kila siku.
Alitoa siku 1 tu ya kumuabudu
 
Mmeona muziki wa baa umekula kibano mnataka na nyumba za zifungiwe shangwe na ibada zao za kupaza sauti? Hapo mjipange hajatokea wa kuzima shughuli za ibada huko. NEMC wakashughulike na uchafuzi wa mazingira kwingine, kwenye nyumba za ibada watachemka. Kwanza watu wa ibada zingine wamewaelewa na wanachukua tahadhari kabla ya NEMC kuwaibukia wameamua kwa hekima na busara ya kiungu kupunguza sauti ya maspika yao ili wasiwe kikwazo kwa wengine. Hao wengine inategemea wana hekima na busara gani kupunguza kelele za sauti za maspika yao. Ni suala la hekima tu kutii mamlaka
Mkuu inabidi uwekwe utaratibu kwa nyumba zote. Waelekezwe haya maspika waliyotundika juu ya paa wayashushe wayaingize ndani ya nyumba ya ibada. Waumini wapo ndani haya maspika waliyoweka nje ya kazi gani?
 
kama kitu hakikuhusu basi ukae kimya ,hata magari yanapiga kelele...
Mkuu magari yanapita barabarani hayaji kwenye makazi ya watu. Sisi tunaongelea hizi kelele zilizopo kwenye makazi ya watu.
 
Back
Top Bottom