NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

Sio ukorofi bali Sala zilikuwepo miaka yote na hakuna sheria inasema adhana marufuku...
Mkuu hatusemi nyumba ya ibada ifungwe bali tunashauri watumie busara kung'oa haya maspika waliyoweka nje wayaingize ndani. Waumini wapo ndani haya maspika yapo nje kwa kazi gani kama sio kuwapigia kelele wananchi wasiohusika na ibada yao?
 
Tatizo watu wa mazingira hawa wezi kuzunguka nchi nzima ilitakiwa wakuu wa wilaya mkoa kusimamia sheria hizo tatizo wakuu wa wilaya na mitaa hawa simamii sheria mfano Ifakara kuna tatizo la kelele kutoka kwenye kanisa lililopo umbali wa mita 5 kutoka msikiti ulipo hilo kanisa lina kelele sana waisilamu wameenda kwa mkuu wa wilaya alie hama ikashindikana kaletewa mkuu wa wilaya muingine nae hivio hivio wakaenda kwa .kuu wa mkoa aliehamia mkoa kagera kutoka Morogoro ikashindikana kwa ujumla hawa watu hawana uwezo wa kusimamia sheria hasa makanisa sijui kwa sababu ni waumini wa makanisa hayo
 
Hayo makanisa yanayokesha dawa ni kuwanunulia spika kubwa na kuwawekea singeli.

Kuna wakati wa kila kitu, Mungu hakusema twende kanisani kila siku.
Alitoa siku 1 tu ya kumuabudu
Kuna siku moja hapa mitaa ya nyumbani baa walikuwa wanapiga kelele, jamaa yangu mmoja kawasha lisabufa lake kaweka sauti hadi mwisho, mbona walikuja kuomba poo! Tangu siku hiyo wakawa na adabu wakapunguza kelele.
 
Mkuu magari yanapita barabarani hayaji kwenye makazi ya watu. Sisis tunaongelea hizi kelele zilizopo kwenye makazi ya watu.
😅😅😅yasitishe magari kwanza uchafuzi wa mazingira na kelele kibao.
 
Kuna siku moja hapa mitaa ya nyumbani baa walikuwa wanapiga kelele, jamaa yangu mmoja kawasha lisabufa lake kaweka sauti hadi mwisho, mbona walikuja kuomba poo! Tangu siku hiyo wakawa na adabu wakapunguza kelele.
Ndicho kinachotakiwa kifanyike, wafate uwaeleze.

Waandikie barua ipitishe kwa mjumbe awape.

Wapeleke Serikali za Mitaa.

Juhudi zote zikikwama wanunulie spika waelekezee muda wanapofanya ibada zao.

Mungu wetu ni wa utaratibu
 
Kwani magari yanapita wapi?
Yanapita barabarani mkuu. Lakini walau magari kelele inapita inaondoka kuliko hii ya maspika yanayolizwa mara 5 kwa siku. Watu hatupumui!
 
Kwahyo kuna nyumba nne za ibada zimeizunguka nyumba yako, ni maeneo gani unaishi ndugu mwandishi?
 
Kwahyo kuna nyumba nne za ibada zimeizunguka nyumba yako, ni maeneo gani unaishi ndugu mwandishi?
Ndio mkuu na kila moja imetundika spika 4 juu ya paa; jumla spika 16. Naishi maeneo ya Tandale.
 
Mkuu inabidi uwekwe utaratibu kwa nyumba zote. Waelekezwe haya maspika waliyotundika juu ya paa wayashushe wayaingize ndani ya nyumba ya ibada. Waumini wapo ndani haya maspika waliyoweka nje ya kazi gani?
hapa sina hoja
 
Ndio mkuu na kila moja imetundika spika 4 juu ya paa; jumla spika 16. Naishi maeneo ya Tandale.
Tandale sehemu gani kuna nyumba za ibada nne sehemu moja ndugu mwandishi? Mana mimi mwenyewe ni mkazi wa Tandale
 
Tandale sehemu gani kuna nyumba za ibada nne sehemu moja ndugu mwandishi? Mana mimi mwenyewe ni mkazi wa Tandale
Tandale kubwa; wewe unakaa Tandale ipi mkuu?
 
Tayari muda umefika; maspika yameanza kuunguruma tena......hadi kero!
 
Wewe unafikiri ikifika alfajiri hatutaki kulala? Kuimba kupokezana
 
Back
Top Bottom