NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

Ungeweka na kaushahidi ka picha tuone namna ulivyozungukwa na nyumba za ibada [emoji4]
 
Pole sana ndugu yangu,hawa jamaa wanakera sana. Mie moja ya sifa ya kiwanja cha kujenga ni kutokuwa karibu na makanisa au misikiti. Huwa sipendi kelele kabisaa nikipumzika
 
Pole sana ndugu yangu,hawa jamaa wanakera sana. Mie moja ya sifa ya kiwanja cha kujenga ni kutokuwa karibu na makanisa au misikiti. Huwa sipendi kelele kabisaa nikipumzika
Asante mkuu. Hawa watu wanatusumbua sana aisee
 
Waumini karibu wote wanamiliki simu. Alarm zipo kwenye kila simu. Wawe wanaset hizo alarm kwenye simu zao muda ukifika zinalia na kuwaamsha kwenda ibadani badala ya kutumia maspika yanayochafua hewa mtaa mzima.
Hili la Waumini kuweka Alarm kwenye simu zao au Kuamshana kwa kipigiana simu inapofika muda wa ibada ni jambo la MUHIMU SANA kwa Waislam na Wakristo pia

Hakuna sababu ya kuwapigia kelele na kuwanyima usingizi na utulivu wengine ambao yamkini sio waimini wa dini hizo

Hivi kuamshana kwa Alarm au kwa kupigiana simu ni Dhambi???

Msaada tafadhali
 
Inabidi wawe wastaarabu, wawe wanapigiana simu na kuweka alarm. Wanatusumbua sana hawa viumbe aisee!
 
Hii nchi hivi sasa imevaa chupi kichwani, NEMC wanajitahidi sana ila watu jamii ya Chalamila na Makala ndiyo shida kubwa, mbaya zaidi mamlaka ya uteuzi inawachekea badala ya kuwakemea
 
hakuna mtu yoyote ataweza kupiga marufuku adhana nyinyi mliee humu mitandaoni mpaka mfe
 
hakuna mtu yoyote ataweza kupiga marufuku adhana nyinyi mliee humu mitandaoni mpaka mfe
KKKT wameonesha nia. Na nyie kuweni wastaarabu, tuondoleeni maspika misikitini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…