Neno "DEAR" linatumika vibaya au ni Ushamba wangu

Kwa miaka ya hivi karibuni matumizi ya neno dear yameongezeka sana, zamani ukimuita mtu dear maana yake kuna mapenzi kati yenu

Kumuita mtu "mpendwa" ina maana mna mahusiano ya kimapenzi?

Waingereza wenyewe wenye lugha yao, neno "dear" hulitumia kwa mtu yeyote pasipo kujali uhusiano wa kimapenzi...
 
Kumuita mtu "mpendwa" ina maana mna mahusiano ya kimapenzi?

Waingereza wenyewe wenye lugha yao, neno "dear" hulitumia kwa mtu yeyote pasipo kujali uhusiano wa kimapenzi...
Umeshasema waingereza. We are not
 
Mtu yoyote akikuita dear ni sawa? Seriously? Kama ni me kuna tatizo mahali
 
Uko sahihi kabisa sio kila mtu utamuita Dear

Mwanaume kwa mwanaume ni No hata kama ni mteja

Dogo fundi anakuita Dear, sio sawa labda wewe umuite Dear ktk hali ya kumbembeleza

Kifupi Dear inasehemu yake ya kutumika
Asante kwa kunielewa mkuu. Kuna wanaume humu wanaitana dear na wanaona sawa. Ina ukakasi kwa upande wangu
 
Nimemuambia mimi na wewe tumezeeka.
Ukiona hivyo situmii neno dear zaidi ya kwenye friendly letter au nikimuandikia ndugu.
Binti yangu ananiita Lovely Dad au Lovely father kwenye mail. Mimi namuita dear daughter (au jina lake).
Kwa mtoto wako au wazazi ni sawa kabisa
 
Dear imekaa kinafiki sana
Tunalitumia kwenye ma email huko
Ila kuliko mpenzi wangu aniite dear bora aniite mbwa
 
Umeshasema waingereza. We are not

Maana halisi ya neno kisarufi katika lugha hubakia vilevile pasipo kujali watumiaji wa lugha husika...

Neno "dear" litabaki kuwa na maana ile ile kwa kuzingatia matumizi yale yale kwa wazungumzaji toka asili zote ulimwenguni...
 
Dada, unaonyesha ww maisha yako ni ya makasiriko sana, mbona unazingatia mambo madogo madogo hvy?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…