Nesi aliyempokea Lissu Hospitalini anadai kuwa Antony Mtaka alimtukana 'Fala wewe' na akamuweka mahabusu siku tatu wakati ni Mgonjwa

Kwa hiyo mumekwisha okoka kwa sasa na uhai wa watu ni part na parcel ya chama chenu, si ndio au hapana?
 
Asante sana kwa video za Mheshimiwa Mtaka. Hata mimi mwenyewe naona ni kama kuna kutaka kumchafua na kumpaka matope.na ndio maana hata mimi nimesema namkubali sana na hata ukisema orodheshwa wakuu wa mikoa walau watatu wachapa kazi na wabunifu ,basi jina la Mheshimiwa Mtaka ni lazima liwepo katika Listi.

Nimezungumza hayo kwa kuwa najuwa ya kuwa uongo ukizunguka sana na kuenea pasipo kupata majibu unageuzwa kama ndio ukweli wenyewe hasa kwa watu wasiopenda kuangalia mambo kwa jicho la tatu. Nafikiri hata wewe mwenyewe Mheshimiwa Mayalla umekuwa ukizungumza juu ya jambo hilo katika baadhi ya makala zako.
 
Haya maisha ni ya kupita tu, miungu watu wana mwisho wao
 
Na rungu limeshawashukia ndiyo maana leo hii yule mwovu mkuu kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania yuko Jehannam anapokea kibano kwa uovu wake uliokithiri
Acha dhihaka zako ndugu yangu. Kwani ni nani ambaye hatakufa hapa Duniani. Ni nani wa kuishi milele.
 
Japo sijasoma ila uko vizurr
 
Kaka Kwa heshima Yako ungemuacha Mtaka hajibu na sio kumjibia.Mtaka hayuko Mbinguni anatakiwa kutupa ufafanuzi lakini tutalejea kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu je Fala ni tusi ama la.Kama Mwanadamu tuna makosa mengi ya kibinadamu hasa tunapotumia akili za wengine katika kiongoza au kufanya maamuzi.
 

Anachoongea sio anachomaanisha, huyo ni bonge la laghai.
 
Wakati JPM anamuapisha Kichere kuwa CAG alisema kuwa alimteua kuwa RAS mkoa wa Njombe kama adhabu. Kuhamishiwa Njombe ni adhabu. Njombe ni mkoa wa adhabu.


Ameendelea kueleza kuwa alitoa maelezo kwa wasaidizi wa Mheshimiwa Rais ambapo anaamini pengine ni katika maelezo yake yale ndio maana Mheshimiwa Mtaka alipewa kama adhabu kwa kupelekwa mkoani Njombe.
 
 
Yesu akawaambia " Hakuna aliye Mwema ila Mungu wa Mbinguni pekee"
 
Kwanza niambie unafahamu maana ya Neno Jemadari ?

Naona kama umelitumia sivyo.
Usipotoshe wasomaji.
Kabla ya kuendelea kujadili hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…