Nesi aliyempokea Lissu Hospitalini anadai kuwa Antony Mtaka alimtukana 'Fala wewe' na akamuweka mahabusu siku tatu wakati ni Mgonjwa

Brother hii dalili ya Uchawa kwa heshima yako hii haikustahili,

Natural Justice,
 
Ndg lukasi

Tayari unaandaliwa utaratibu murwaaa wakumtimbisha mtaka kotini , tusubirie
Sawa japo ukumbuke ya kuwa mlalamikaji anatakiwa kuwa na ushahidi usioacha shaka ya aina yoyote ile. Mahakama haipokei ushahidi wa maneno tupu bila ushahidi wenye mashiko.
 
Lucas mbona unamkaanga Mtaka mwana ccm mwenzako? Mtakatana mapanga safari hii
 
haha sahihi kabisa hata bashite analijua hilo.
 
Lucas mbona unamkaanga Mtaka mwana ccm mwenzako? Mtakatana mapanga safari hii
Hapana ndugu yangu wala simkaangi bali nina mashaka na ukweli wa tuhuma zilizoelekezwa kwake na yule Nesi.ndio maana nikatamani kama angeweza kutoa neno la kukanusha au kuelezea juu ya tuhuma zile.

Humu jukwaani tuna Mheshimiwa Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambaye ni mfano wa kuigwa na aambaye huwa anatolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoibuka katika jamii hata mitandaoni pia.

Kwa hiyo naamini Mheshimiwa Anton Mtaka anaweza kufanya kama afanyavyo waziri wetu Mheshimiwa Dorothy Gwajima. Unajuwa video ile Inaendelea kuzunguka mitandaoni na watu ni wepesi wa kuamini ikiwa haitakanushwa au kutolewa majibu.
 
Nikisema hapa kizimkazi hana muda na watanganyika ona alishindwa nn yy kumckiliza? Tena ni mwanamke mwenzie!! Huyu kizimkazi hakuna anacho weza zaidi y kuteua na kutengua TU. Watanganyika tujipange sana kuhusu kizimkazi.
Na bado hata sikilizwa kwa uongozi w kizimkazi ila ingekua kwenda nje kuombaomba misaada yuko vzr au kuuza mali za watanganyika Yuko POA MNO.




KAZI ni kipimo cha UTU
 
Anasema kwa sasa anahitaji msaada wa kisheria ili aweze kufungua kesi mahakamani.ambapo amemuomba Lissu amsaidie kufungua kesi mahakamani.
Kesi kisa kuitwa fala au kufukuzwa kazi au kutolipwa mafao ama ni kipi hasa?

BTW: Hizo lugha kwa hawa miungu watu ni kawaida sana sitoshangaa ikiwa ni tuhuma ya kweli.

Mtaka is overrated,kuna takwimu zozote za huo uchapakazi kuanzia Simiyu hadi huko alipo sasa?
 
Anasema Anahitaji msaada wa kisheria kuhusiana na kufukuzwa kwake kazi kwa kosa la utoro.wakati yeye anadai kuwa alikuwa ni mgonjwa na anayobarua ya madaktari kutoka muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
 
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais wetu.sihitaji hata kukujibu kwa kuwa umekosa adabu kabisa kwa Rais. Rais wa nchi usifananishe na mtu wa kawaida.kwanini usingeuliza kwa lugha ya staha na adabu ili uweze kujibiwa kuliko kuandika kwakutumia lugha chafu,ya kejeli na dharau?
 
Wewe unamjua kwasababu umemwona kazini, sisi tuliokua na kuishi nae tunajua mengi zaidi yako.
 
Ni kweli uongo ukisemwa sana, na kuachwa ukarudiwa rudiwa, hugeuka ukweli, lakini sio uongo wa kijinga!. Dawa ya uongo wa kijinga ni kuupuuzia tuu, utajifia wenyewe!. Mfano shetani kakupitia, ukapita na dada zetu wale wa ile biashara, kisha akataka pesa zaidi na wawe huna, akaamua kukuchafua kwa kusema hujafanyiwa sunna!, vipi wewe ili kukanusha, utafungua zipu kuonyesha kuwa sii kweli?. Vitu vingine vya kujinga mno ni vya kupuuzwa tuu!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…