Netanyau atinga kambi ya Jeshi la Israel iliyopigwa na drone, aapa kuitandika Hezbollah bila huruma popote walipo Lebanon ikiwemo Beirut

Kwa hiyo akijiuzulu magaidi wataacha nia yao ya kuwaangamiza wayahudi?!
1. Iran kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
2. Palestina kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
3. Jordan kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
4. Syria kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
5. Lebanon na nchi nyingine nyingi za eneo hilo kuna wayahudi na hakuna anaewagusa.

Hivyo hata hao kina Netanyahu na genge lake wakifuata mipaka ile ile iliyowekwa na Umoja wa Mataifa kati yake na Wapalestina hakuna mtu atakaewagusa. Ila wakiendelea kuvamia maeneo ya wenzao kuwafukuza katika nyumba zao, kujenga katika ardhi za wenzao huko ukingo wa magharibi, basi watakuwa wanatafuta wenyewe ugomvi na hivyo wataendelea kupambana tu.

Ni kama vile serikali ilivyowatoa wamasai katika ardhi zao kwa nguvu, kila mtu ukiwemo wewe ulilalamika. Sasa kwanini na wenyewe wapalestina wakitolewa kwa nguvu wasilalamike. Cha ajabu wakilalamika wanakamatwa, wakiandamana wanapigwa risasi. Sasa haki hapo iko wapi? Kwanini waisrael wasiridhike na mipaka iliyowekwa ili kuondoa mivutano isiyokuwa na lazima. Bunduki na vifungo kwa wadai haki zao haviwezi kuwa suluhisho la kudumu. Maana kuna siku wale mnaowapiga bunduki na kuwafunga watachoka na kuamua liwalo na liwe, hivyo kuleta maafa pande zote wanyanyasaji na wanyanyaswaji.

Nina imani hata wewe unajua mateso yote wanayopitia wapalestina kule ukingo wa magharibi, sema tu itikadi fulani inakufanya ujifanye huyafahamu. Kila siku, kabla hata ya October 7 Israel imekuwa ikikatazwa na Umoja wa mataifa na sometimes hata Marekani yenyewe kuwa wasitumie nguvu kujenga katika maeneo ambayo sio halali wao kujenga, lakini wanakaidi kwa kuona hakuna mtu wa kuwafanya kitu.
 
Yeah. Watu wanashindwa kuelewa kwamba hao viongozi sio wao kwa majina binafsi (Personal interest) bali wanausimamia na kuzingatia Mfumo (System)uliopo. Kumbadilisha kiongozi hakuna Tija kwani awe yeyote yule atakayeshika hiyo nafasi lazima azingatie kanuni zilizopo.
 
Hakuna kiongozi wq isael aliyeleta maafa kwa israel kama netanyahu ,ni mbinafsi na hata viongozi waliopita wanamlaumu kwa kuweka maslahi yake ya kisiasa mbele kuliko ya watu wa israel, waziri wake wa vita gantz alijiuzulu baada ya kutofautiana nae hadharani ,na huyu wa sasa gallant pia anaendelea kumpinga hadharani kila siku hadi netanyahu anamtishia kumfukuza
Hadi sasa kapigana na mgambo wa hamas mwaka mzima hakuna alicho achieve, kaenda kumchokoza iran huku anajua kabisa nguvu hana ya kupigana na iran , anamtegemea marekani wqkati marekani hataki kujiingiza kwenye vita yupo kwenye uchaguzi sasa hivi, israel haijawahi kuwq na mpumbavu kama neyanyahu, ehud barak alimwambi asiende lebanon maana ni kutaka kuwaua wanajeshi wa idf bila ya sababu maana hakuna watakacho achieve ila kichwq nazi yule kaenda ,kasababisha hadi weqkness ya israel defence system imejulikana na dunia nzima ndio maana kasita kulipiza kisasi kwa iran ,kwa sasa hawezi kumgusa iran hadi defence system aliyotuma marekani ifike ama sivyo atachakazwa
 
Vikimaliza tuna uhakika kidogo boko haram na alshabab wa kenya na msumbiji watatulia
Hao yawezekana sasa hv wameshakuwa mobilised kwenda kuwasaidia ndugu katika Iamani. Kwa hiyo HAMAS, Hezbollah na Houths wakimalizika nao jamaa watakuwa wamemalizikia mumo humo ndani kwa ndani.
 
Mental case.

Kwamba israel inapigwa? [emoji23]
 
Hao yawezekana sasa hv wameshakuwa mobilised kwenda kuwasaidia ndugu katika Iamani. Kwa hiyo HAMAS, Hezbollah na Houths wakimalizika nao jamaa watakuwa wamemalizikia mumo humo ndani kwa ndani.
Vikosi kwa sasa vimeenda kusaidia huko.....ndo maana huku Africa wamepumzika kidogo.........ashinde atakaeshinda ila hawa jamaa wapunguzwe
 
Ameshachanganyikiwa ni mwehu huyu!

Alishalipua kwa kupiga makombora wafu makaburi ya Beirut analipi tena la kufanya na la kusema!?
Hivi inakuwa ni kuchanganyikiwa kama adui akikimbilia makaburini eti asibutuliwe ila aachwe kwa kuwa yupo makaburini?
 
Vikosi kwa sasa vimeenda kusaidia huko.....ndo maana huku Africa wamepumzika kidogo.........ashinde atakaeshinda ila hawa jamaa wapunguzwe
Inaonekana kama kura ya ushindi inakwenda kwa Israeli. Tusubiri tuone.
 
Kaanza kula viapo tena ,,hichi sijui ni kiapo cha ngapi
 
Ayatollah hajasema nchi za kiislam ziungane kupigania dini ya kiislam.
Bali nchi za kiislam ziungane kutetea waislam.
Je hapo kuna mfanano mkuu!?
 
Ayatollah hajasema nchi za kiislam ziungane kupigania dini ya kiislam.
Bali nchi za kiislam ziungane kutetea waislam.
Je hapo kuna mfanano mkuu!?
 
Ayatollah hajasema nchi za kiislam ziungane kupigania dini ya kiislam.
Bali nchi za kiislam ziungane kutetea waislam.
Je hapo kuna mfanano mkuu!?
Ni Waislam gani watakaotetewa mkuu?
Mbona kote Lebanon, Gaza wapo Wakristo, Wayahudi, Waislam hata dini za Jadi? Kama Waislam wakijibagua kwa mtindo huo, mwishoni mwa vita itakuwaje?
Ingelifaa waseme nchi za kiislam ziungane kutetea Haki.
 
Ni Waislam gani watakaotetewa mkuu?
Mbona kote Lebanon, Gaza wapo Wakristo, Wayahudi, Waislam hata dini za Jadi? Kama Waislam wakijibagua mwishoni mwa vita itakuwaje?
Ingelifaa waseme nchi za kiislam ziungane kutetea Haki.
Ameongea kauli hiyo kwasababu mashariki ya kati majority ni waislam kuliko dini nyingine.
Ila haimaanishi kuwa dini zingine wametengwa laa hasha kaka.
 
Ameongea kauli hiyo kwasababu mashariki ya kati majority ni waislam kuliko dini nyingine.
Ila haimaanishi kuwa dini zingine wametengwa laa hasha kaka.
Ni dhana inayoonekana kutenga Raia wa eneo husika na kumbuka mti wa mbuyu huanza kama mchicha, lakini baadya ni mti mkubwa sana. Kwa mantiki hiyo hako kaneno kanaonekana kadogo kwa sasa ila huko mbeleni inaweza kuja kuwa ni hoja ngumu kubwa tena itakayoweza kuzaa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ni bora ikaachwa hata kama ni hoja ya majority.
 
Ikiwa hivyo atazitembea kambi nyingi. Hii nyingine imebamizwa Haifa:


View: https://www.youtube.com/live/h1J8TmxaDcY?si=eaELDQPir2TbIrEv
 
Hii comment yako hadi wenzako watakua wanakushangaa. Mmeshaanza kusahau vipigo vilivyowafanya mumpigie kelele watu wanakufa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…