6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
1. Iran kuna wayahudi hakuna anaewagusa.Kwa hiyo akijiuzulu magaidi wataacha nia yao ya kuwaangamiza wayahudi?!
2. Palestina kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
3. Jordan kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
4. Syria kuna wayahudi hakuna anaewagusa.
5. Lebanon na nchi nyingine nyingi za eneo hilo kuna wayahudi na hakuna anaewagusa.
Hivyo hata hao kina Netanyahu na genge lake wakifuata mipaka ile ile iliyowekwa na Umoja wa Mataifa kati yake na Wapalestina hakuna mtu atakaewagusa. Ila wakiendelea kuvamia maeneo ya wenzao kuwafukuza katika nyumba zao, kujenga katika ardhi za wenzao huko ukingo wa magharibi, basi watakuwa wanatafuta wenyewe ugomvi na hivyo wataendelea kupambana tu.
Ni kama vile serikali ilivyowatoa wamasai katika ardhi zao kwa nguvu, kila mtu ukiwemo wewe ulilalamika. Sasa kwanini na wenyewe wapalestina wakitolewa kwa nguvu wasilalamike. Cha ajabu wakilalamika wanakamatwa, wakiandamana wanapigwa risasi. Sasa haki hapo iko wapi? Kwanini waisrael wasiridhike na mipaka iliyowekwa ili kuondoa mivutano isiyokuwa na lazima. Bunduki na vifungo kwa wadai haki zao haviwezi kuwa suluhisho la kudumu. Maana kuna siku wale mnaowapiga bunduki na kuwafunga watachoka na kuamua liwalo na liwe, hivyo kuleta maafa pande zote wanyanyasaji na wanyanyaswaji.
Nina imani hata wewe unajua mateso yote wanayopitia wapalestina kule ukingo wa magharibi, sema tu itikadi fulani inakufanya ujifanye huyafahamu. Kila siku, kabla hata ya October 7 Israel imekuwa ikikatazwa na Umoja wa mataifa na sometimes hata Marekani yenyewe kuwa wasitumie nguvu kujenga katika maeneo ambayo sio halali wao kujenga, lakini wanakaidi kwa kuona hakuna mtu wa kuwafanya kitu.