6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Nafikiri wewe ndo watu wanakushangaa. Kwani kati ya Iran na Israel ni wapi watu wanahaha kila siku kukwepa makombora?Hii comment yako hadi wenzako watakua wanakushangaa. Mmeshaanza kusahau vipigo vilivyowafanya mumpigie kelele watu wanakufa sana
Ushawahi kusikia Iran watu wanakimbilia chini ya mahandaki kukwepa makombora? Lakini Israel kila siku watu wanakimbilia chini ya mahandaki. Yani hakuna anaeijua kesho yake. Leo ikipita salama, basi kesho wanashambuliwa. Kesho ikipita salama basi keshokutwa wanashambuliwa. Wakipumzishwa na Hamas wanapigwa na Hezbulah, wakipumzishwa na Hezbulah wanapigwa na Houth ya Yemen.
Ndomaana wenye akili tunashauri kuwa Netanyahu aombe suluhu ya kumaliza vita. Kwani kupambana na nchi iliyokuwekea makundi mpakani kwako yakutwange kila siku ni kazi nzito. Hapo aumiae ni Israel. Iran haina cha kupoteza kwani kwao ni salama.
Hapo Ayatollah kashika mpini, na Netanyahu kashika makali. Wakivutana yeye (Netanyahu) ndo atachanika mikono. Iran kwao hata baruti ya kibiriti haijawahi kupigwa. Watu wanalala na kuamka salama.