New Force/ Golden Deer acheni uhuni kwa mizigo ya abiria

New Force/ Golden Deer acheni uhuni kwa mizigo ya abiria

Latra wapo na ilo swala hawawezi fatilia. Bus zinaamua zenyewe ulipe shillingi ngapi. Bei atakayojisikia mkatisha tiketi kukucharge ndjo iyo utatoa
 

Attachments

Pole sana ,kusafirisha mizigo Kwa basi ni changamoto sana Nchi hii
 
Ana haki ya kutoa dukuduku lake na kuwaonya wengine wachukue tahadhari kabla ya hatari.

Makampuni ya usafirishaji yanatakiwa kuacha ubabaishaji. Scandinavia waliweza nyie mnashindwa nini?

DHL wanawezaje?
Wanatumia kutokuwepo kwa mpinzani
 
Kuna siku nilisafirisha mzigo uzito wa kg15 una kaupana 90X50 ila nikaambiwa elfu 60 nikaomba sababu hakuna nikawauliza gunia la maindi la kilo 100 tunalipa 30000 itakuwaje haka kamzigo.

Mabasi yana tatizo kwenye wafanyakazi wake sio uongozi wa juu
Hii shughuli alitakiwa ifanya Posta
 
Hapa TCRA wamezembea, wao ndio wanaotoa leseni za kusafirisha mizigo. Mizigo inasafirishwa kutokana na uzito wake. Sio kutokana na thamani yake.

Mkuu una maana 10kg usafiri ya sukari, dhahabu au almasi zitakuwa na gharama Ile Ile? Kiuhalisia thamani ya mzigo haiwezi kuepukwa kwenye kufahamu gharama za kusafirisha vitu kwa watu serious.
 
Mkuu una maana 10kg usafiri ya sukari, dhahabu au almasi zitakuwa na gharama Ile Ile? Kiuhalisia thamani ya mzigo haiwezi kuepukwa kwenye kufahamu gharama za kusafirisha Kwa watu serious.
Mkuu almasi ya milioni kumi utaisafirisha na basi?
Mizigo yenye thamani kubwa hata kwenye ndege utatakiwa uikatie bima kwa kipindi cha safari, labda iwe ndege yako mwenyewe.

Mwenye basi atakayekubali basi lake lisafirishe almasi kienyeji kwa kutoza 10% ya value ya mzigo, anajitakia kufilisika.
 
Ana haki ya kutoa dukuduku lake na kuwaonya wengine wachukue tahadhari kabla ya hatari.

Makampuni ya usafirishaji yanatakiwa kuacha ubabaishaji. Scandinavia waliweza nyie mnashindwa nini?

DHL wanawezaje?
Mkuu hao Scandinavia kwani leo wanasema je?
 
Mkuu almasi ya milioni kumi utaisafirisha na basi?
Mizigo yenye thamani kubwa hata kwenye ndege utatakiwa uikatie bima kwa kipindi cha safari, labda iwe ndege yako mwenyewe.

Mwenye basi atakayekubali basi lake lisafirishe almasi kienyeji kwa kutoza 10% ya value ya mzigo, anajitakia kufilisika


Ninadhani ndiyo sababu ya msafirishaji kujua thamani ya mzigo ili ajue risk kwake kiasi gani anaweza kuikubali na hata kuikabili Ikibidi kulipa fidia Kwa upotevu.
 
Ninadhani ndiyo sababu ya msafirishaji kujua thamani ya mzigo ili ajue risk kwake kiasi gani anaweza kuikubali na hata kuikabili Ikibidi kulipa fidia Kwa upotevu.
Lakini wanatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa muongozo ulioainishwa kwenye leseni yao ya biashara iliyotolewa na TCRA
 
Nimeona una sambaza bandiko hili sehem tofauti tofauti kwenye mitandao mingine ya kijamii, sijui lengo ni nini?

Hayo mambo yanatokea sana kwenye sector ya usafirishaji.
Acheni kutetea huduma za ajabu kwa visingizio vya kitoto sana. Wanasema sio mara ya kwanza wanafanya hivi. Acha aseme ili wanaoweza kusafirisha kwa uaminifu wapewe hayo majukumu. Ndio maana hiyo sector sio monopoly.
 
Golden deer sijui New Force ni wababaishaji. Wanajiamini maana biashara ya nyanda za juu kusini wameishika kasoro Songea maana Superfeo anawapelekea moto balaa na G7 yake wana adabu kidogo, ila Mbeya, Tunduma na Sumbawanga jamaa wanaringa sana manina zao..
Hawa super feo nao upande wa Moshi to songea ni washenzi tu kwakua iyo njia wapo waho tu .wana sumbua sana
 
Makampuni ya bus janja nyingi sana. Ukipeleka mzigo wanauliza thamani ya mzigo ukisema laki 3 wanaomba 30000 wanadai ni 10% ya thamani ya mzigo ndio wanaku charge

Ila ukienda na mzigo wa 30000 au chini ya laki hawapigi tena 10% wanataka uwape 10,000. Changamoto hakuna kigezo rasmi ya kutoza namna yao ya usafirishaji.

Mfano ni allys star

Umuhimu wa pesa unayolipa huwa unaonekana pale mzigo ukipotea, ukitaka kurudishiwa gharama zako.
 
Back
Top Bottom