New Force/Golden Deer kwanini ajali mnapata nyie tu?

N

Nimewauliza hilo swali.Wamenijibu kwamba kila mmoja hupanda basi moja tu.Haijalishi kampuni Ina mabasi mangapi barabarani.Kama nimewaelewa hivi!
Hizo chuma kwa kukusaidia tu hata zipate ajali hawajawahi kuacha kuzipanda otherwise kama wewe mnazi wa Sauli
 
Upo sahihi kabisa,mchina bado yupo kwenye utafiti na basi zake ili ziweze kuwa compatible na hali yetu huku Africa
 
Upo sahihi kabisa,mchina bado yupo kwenye utafiti na basi zake ili ziweze kuwa compatible na hali yetu huku Africa
Kabla mabasi ya China hayajaja hizo Scania, Isuzu, Volvo, Nissan Diesel na Iveco hazikuwahi kupata ajali?
 
Kabla mabasi ya China hayajaja hizo Scania, Isuzu, Volvo, Nissan Diesel na Iveco hazikuwahi kupata ajali?

Zilikuwa zikipata ajali,ila angalia miundo mbinu wakati huo na sasa,angalia teknolojia ya magari wakati huo na sasa….ukija kwa sasa fanya tafiti njia hyo hyo ya dar-mbeya mabasi mangapi aina ya European na mchina yaliyopata ajali,halafu fuatilia mfumo wa kimakenika wa basi za European na basi za mchina unaweza ukapata kitu
 
Mchina sasa hivi ana brands nyingi za mabasi hapa Tanzania kaiacha Scania kwa mbali sana

So obvious ikitokea ajali hata kama mabasi yako 10 hukosi Chinese brands 8 au zote 10 utakuta ni Chinese brands

Kwa hapo hauna hoja ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…