New York: Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour Tanzania - Starring Samia Suluhu Hassan, President of The United Republic of Tanzania

Unatafuta uteuzi au??unatujazia server humu
 
Daaah Bora asingetumia ngeli kuzungumza, ngeli mbovu au wangemwandikia akawa anasoma tu, Huyu Na Mzee Baba Hawana Tofauti [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sijui hii if ya siku hizi imekuwaje?!. Ingekuwa ni ile JF ya enzi zile, saa hizi ungekuta tuna updates zaidi ya members 10!.
Yaani unamaanisha kati ya hao waalikwa zaidi ya 400, hakuna mwana JF yoyote kutu update!.
P
JF ya sasa hivi imejaa siasa za propaganda za vyama na chuki tu, nothing serious
 
Hata wakiongezeka watalii wengi namna gani, unadhani tutaambulia kitu hapo?
List iliyorudishwa kwenye mfumo ni ile ile iliyokuwepo mpaka mwaka 2015. Ni List hatari kabisa kwa maendeleo ya Nchi.
Kwa issue ya maendeleo, kwa sasa Watanzania tusahau kabisa labda utokee mwujiza wa Mwenyezi Mungu.
 
mangi punguza tamaa ya wizi, utabinuliwa siku moja.

Yaaani unamchukia mtu kwasababu kakudhibiti usiibe
 
Sijaona sababu ya mama kutumia hela za walipa kodi kwenda kuzindua hiyo filamu huko kwa Biden, hayo ni matumizi mabaya ya kodi.

Mbaya zaidi hata Biden mwenyewe kapotezea huo uzinduzi jicho lake lipo kwa putin tu.
 
Mkuu Paskal,usidanganyike na uzalendo katika taifa hili.Trust me hata URUSI akituvamia na kutupiga TZ, bado wa TZ tutamshangilia PUTIN na kufurahia wanajeshi wa SAMIA wanavyopelekewa moto (ambao ni ndugu zetu)
Hisia za uzalendo waliziharibu mboga mboga ikawa ni taifa la wanufaika wachache huo uzalendo utatoka wapi?
 
mangi punguza tamaa ya wizi, utabinuliwa siku moja.

Yaaani unamchukia mtu kwasababu kakudhibiti usiibe
Shida zinaenda liwa wakati chini wakiteseka kukusanya hata kumi awapati.
Uzoefu waliojifanya Kazi kwa3 uaminifu baada ya kustaafu wametupwa jongoo wanajutia bahati
 
CCM bana, mnaitangaza nchi yetu kwa mabeberu ili waje waendelee kutuibia raslimali zetu.
 
Channel ten,imeonyeshwa live
 
Sijaona sababu ya mama kutumia hela za walipa kodi kwenda kuzindua hiyo filamu huko kwa Biden, hayo ni matumizi mabaya ya kodi.

Mbaya zaidi hata Biden mwenyewe kapotezea huo uzinduzi jicho lake lipo kwa putin tu.
Mkuu Kambi ya Fisi , tuna tatizo kidogo kwenye eneo la upashanaji habari. Safari ya Marekani sio tuu ni kuzindua filamu, bali kila mwezi April ya kila mwaka ndio muda wa vikao vya maamuzi vya wakubwa wakubwa wa pesa Duniani, yaani IMF, IFC na WB, hivyo Mawaziri wa fedha wa dunia na Magavana wanakutana kudefend maombi ya mikopo, marais wa nchi wakiwepo wanatia uzito, hivyo Mama Samia yuko huko kwa mikutano hiyo, hivyo hiyo ratiba imefanywa kuoanishwa tuu.

Na kila mwishoni mwa September na Mwanzoni mwa October, ni kikao cha UNGA, New York inafurika marais, Samia ndani.

Hivyo wewe ungelijua hili wala usingeuliza.
P
 
USA siyo bongo, hawana sifa za kujulikana na kufahamiana.
Kwani siku ile hukumuona kavaa t-shirt ya Diaspora akimpokea Mama?
Shughuli hiyo inamhusu mama, itashangaza sana kama 'diaspora' mtegemewa kama Da Mange atakuwa hatambuliki kabisa na mgeni wake mashuhuri wakati huu!
 
Mkuu 'kalunya', nimekusoma mara mbili, lakini bado nashindwa kuelewa hasa lengo lako ni nini na andiko lako hili.

Unataka na hilo libosi liachane na uaminifu, au siyo? Liache 'kudhibiti' watu wale kwa urefu wa kamba zao!

Umekosea sana kuweka haya mawazo yako katiika andiko langu hapo juu.
Hilo 'libosi' kwangu ni jitu linalostahiri pongezi sana, pamoja na matatizo yanayolikabili.

Kwangu mimi, huyo ndiye mTanzania mzalendo, anayelitakia taifa hili mema, bila ya kujali vishawishi vingi vinavyomkabili.

Kama wewe kweli unasimamia mawazo uliyoyaweka hapa, basi wewe ni mmoja wa maadui wa nchi hii mnaostahili kabisa kunyongwa na kufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…