Ngekewa(Capybara): Mnyama pekee apendwae na wanyama wote

Ngekewa(Capybara): Mnyama pekee apendwae na wanyama wote

Nipatie huyu mnyama akiwa hai au ngozi yake ya milioni 5
 
KAMA ULIKUWA HUJUI......

Hii ndio asili ya neno NGEKEWA

1.Mnyama anayefahamika kwa jina la kigeni Capybara ambapo kwa kiswahili huitwa Ngekewa ni mnyama mwenye ukubwa wa sentimita 134 na uzito unaokadiliwa kuwa kilo 66 anapokuwa mkubwa na mnyama huyu asili yake ni nchi ya America ya kusini.

2. Ni mnyama ambaye anapenda kukaa karibu na maji na anapojisi hatari hulazimika kukimbilia ndani ya maji na ana ujuzi mkubwa wa kuogelea.

3. Akiwa ndani ya maji anaweza kutumia dakika tano bila kuibuka ambapo hubana pumzi ndani ya maji anapokwepa hatari ya kushambuliwa na adui yake.

4. Huyu Ngekewa ndio mnyama anayependwa na viumbe vingi vya porini na majumbani.
Wanyama kama mamba, chatu, nyani, paka, kobe na hata ndege wa aina mbali mbali hupenda kukaa karibu naye na kufurahia maisha hivyo mnyama huyu huhesabika kama kiumbe chenye bahati ya kupendwa na viumbe wengine ukiondoa maadui zake.

5. Kwenye kamusi ya lugha ya kiswahili neno Ngekewa mbali na kumzungumza huyu mnyama pia limetafsiliwa kama bahati au yenye bahati na ndio maana hata mtaani
IMG_6181.JPG
mtu mwenye bahati huambiwa ana ngekewa.
Asili ya maana ya neno ngekewa ipo katika kupendwa kwa huyu mnyama na viumbe mbali mbali hata vile vya hatari.
.
Na Joachim mhagama 0713736187
IMG_6180.JPG
IMG_6182.JPG
 

Attachments

  • IMG_6181.JPG
    IMG_6181.JPG
    16.2 KB · Views: 41
Babu Asprin ni mmoja wa viumbe wachache wenye nyota ya huyu mnyama maana kila K-Vant inamshobokea yeye.
Babu na mimi nikikua mkubwa nataka niwe kama wewe.
Hahahaha we jamaa bhana. Ngoja nikukabidhi kwa my dia mjukuu joanah akubatize kwa moto ili haka kanyota ka huyu mdudu kakudondokee...

joanah my dear weekend hii tukamilishe lile zoezi letu tafadhali
 
Hahahaha we jamaa bhana. Ngoja nikukabidhi kwa my dia mjukuu joanah akubatize kwa moto ili haka kanyota ka huyu mdudu kakudondokee...

joanah my dear weekend hii tukamilishe lile zoezi letu tafadhali
Babu Asprin kweli sasa hivi unaanza kuzeeka mpk ushasahau kua joanah ni dadangu hivyo huo ubatizo wa moto haiswihi kabisa yeye kunifanyia.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Khantwe naona umedhamiria kupima kina cha maji kwa kudumu kizalendo miguu yote miwili.
[emoji23][emoji23][emoji23] lakini nipata jibu, nikisombwa na maji hiyo ni ajali kazini
 
Back
Top Bottom