Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leteni Dodoma hii kituKwenye mfumo wa gesi haipo hivyo boss ukijaza gesi inakaa muda mrefu. Ikiisha kama haupo karibu na kituo unaweza kuswichi kutumia mfumo wa mafuta mpaka utakapojaza tena gesi.
Hakuna hasara zozote boss ni faida tu.Tuambie na hasara zake bas.....
Karibu sana bossAhsante kwa muongozo...
Boss yawezekana huko mbeleni serikali ikawaletea gesi na Dodoma pia. Na kama unavyojua hii biashara ya gesi inaangalia maeneo yenye magari mengi.Leteni Dodoma hii kitu
Boss gesi ambayo waziri wetu wa nishati aliwagawia watanzania lengo kubwa lilikua ni kuwahamasisha watanzania wa vijijini kutumia gesi kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa vinavyochochea ukataji wa miti yetu na kuharibu misitu yetu. Ni jambo zuri ambalo hata mimi nililipenda.We unahamasisha hivyo waziri anagawa mitungi ya gesi porini wasipokuwepo mawakala .halafu mnaplan kupeleka ges kenyabwakati soko la ndani hamlitendei haki.
Njoo ufunge mfumo boss, acha uoga.Natamani sana nije nifunge huo mfumo. Ila ule mtungi unachukua nafasi kubwa afu nikiuona naogopa naona kama nafunga bomu.
Sawa,Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako.
1. Ukijaza gesi ya Tsh. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200.
Tsh. 17000 = Km. 200
? = Km. 1
Km. 1 = Tsh. 17000/200 = Tsh. 85
Kikawaida ukijaza lita moja ya petroli unaweza kusafiri kilomita 10 hadi 12. Chukulia lita moja ya petroli ni Tsh. 2886
Tsh. 2886 = Km. 12
? = Km. 1
Km 1 = Tsh. 2886/12 = Tsh. 240.5
Sasa ukitumia gesi kwenye gari yako kwa kila kilometa 1 unaokoa Tsh. ngapi?
Unaokoa = Tsh. 240.5 - Tsh. 85 = Tsh 155.5
Kumbe kwa kila Km. 1 unaokoa Tsh. 155.5
Gharama za kuiongezea mfumo wa gesi gari yako ni Tsh. 1,800,000. Tunazibadili hizi kwenda kwenye Km.
Km 1 = Tsh. 85
? = Tsh 1800,000
Tsh 1800, 000 = Km. 21176.5
Unataka tujue katika Km. hizo tunaokoa Tsh. ngapi?
Km. 1 = unaokoa Tsh. 155.5
Km. 21176.5 = ?
Unaokoa = Tsh. 21176.5 × 155.5 = Tsh. 3,292,941
Sasa unaweza kuona ukiongeza mfumo wa gesi unatumia Tsh. 1,800,000 ambazo zinakuwezesha kutembea Km. 21176.5 kama ukizitumia kununulia gesi. Sasa ukitembea Km. 21176.5 hizo kwa kutumia gesi utaokoa Tsh 3,292,941. Kumbe gharama uliyotumia kubadilisha gari yako itumie gesi itarudi ukisha tembea Km. 21176.5 na faida juu.
2. Kuongeza mfumo wa kutumia gesi kwenye gari inayotumia mafuta inagharimu Tsh. 1,800,000. Gharama hii ni kwa gari zenye cc 400-2000. Na kutakua na ongezeko la Tsh. 80,000 endapo kama spark plugs hazitaruhusu mfumo huo.
3. Ukisafiri kwa kutumia Tsh. 100,000 za mafuta ukitumia gesi utatumia Tsh. 40,000 tu. Umeokoa Tsh. 60,000.
4. Ukiweka mafuta ya Tsh. 45,000, kwa mwezi utatumia Tsh. 1,350,000. Kwa miezi miwili ni Tsh. 2,700,000.
Gesi unaweka ya Tsh. 17,000 na unatumia siku 2 mpaka 3. Inamaana unaongeza gesi kila baada ya siku 2 or 3.
Kama kila baada ya siku 2 unaongeza gesi mara 15 kwa mwezi (Tsh. 17,000 × 15 = Tsh. 255,000). Kwa miezi mwili hii ni Tsh. 510,000.
Gharama za kuongeza mfumo wa gesi ni 1, 800,000 + gesi ya miezi miwili ni Tsh. 510,000 jumla ni Tsh. 2,300,000.
Hivyo ukichukua gharama za mafuta kwa miezi miwili Tsh. 2,700,000 ukatoa gharama ya kufunga mfumo wa gesi na matumizi ya miezi mwili ya Tsh. 2,300,000 unabakia na Tsh. 400,000.
Kwa hiyo kwa mfano huu faida unaanza kuiona baada ya miezi miwili. Kuanzia mwezi wa tatu badala ya kutumia Tsh.1,300,000 kwa mafuta anatumia Tsh.255,000.
Hivyo unaweza kuona jinsi unavyo okoa fedha nyingi ukiongezea mfumo wa gesi kwenye gari yako inayotumia mafuta.
Ukitaka kuongeza mfumo wa gesi kwenye gari yako embu piga namba hii 0747744895
Soma vizuri boss, kwa huu mfumo utaokoa fedha nyingi sana.Sawa,
Lakin still 1.8m mko juu sana.
Boss hizi ni stori za mtaani tu. Huu mfumo una faida nyingi sana. Kwanza ni environmental friendly.Ukitaka gari yako iwe bajaji weka huo mfumo
Environmental friend is stupidity ..waingereza wenyewe wamerudi kwenye Kuni na makaka ya mawe..wewe ni Nani kujali hayo mazingira..who is you?Boss hizi ni stori za mtaani tu. Huu mfumo una faida nyingi sana. Kwanza ni environmental friendly.
Hiyo ilikua ni moja, sikumaliza boss. Mbili, CNG ni economical friendly.Environmental friend is stupidity ..waingereza wenyewe wamerudi kwenye Kuni na makaka ya mawe..wewe ni Nani kujali hayo mazingira..who is you?
Gari inakua kama bajajiHiyo ilikua ni moja, sikumaliza boss. Mbili, CNG ni economical friendly.
Boss hizo ni stori za vijiweni usizisikilize sana. Mfumo huu ukiufunga utaokoa fedha nyingi sana.Gari inakua kama bajaji