Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako na jinsi utakavyo okoa fedha nyingi

Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako na jinsi utakavyo okoa fedha nyingi

Leteni Dodoma hii kitu
Boss yawezekana huko mbeleni serikali ikawaletea gesi na Dodoma pia. Na kama unavyojua hii biashara ya gesi inaangalia maeneo yenye magari mengi.
Ila inawezekana sana tukiwa na tenka la gesi linatoa gesi Dar es Salaam au Mtwara na kuileta huko Dodoma na kuijaza kwenye magari moja kwa moja.
images (6).jpeg
mobile-CNG-filling-station-1024x593.jpg
 
We unahamasisha hivyo waziri anagawa mitungi ya gesi porini wasipokuwepo mawakala .halafu mnaplan kupeleka ges kenyabwakati soko la ndani hamlitendei haki.
Boss gesi ambayo waziri wetu wa nishati aliwagawia watanzania lengo kubwa lilikua ni kuwahamasisha watanzania wa vijijini kutumia gesi kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa vinavyochochea ukataji wa miti yetu na kuharibu misitu yetu. Ni jambo zuri ambalo hata mimi nililipenda.

Lakini pia Tanzania tuna kiasi kikubwa cha gesi ambacho tukitegemea soko la ndani pekee wawekezaji watachelewa kurudisha gharama walizotumia kwenye uwekezaji wao na sisi wenyewe tutachelewa sana kuanza kupata mgao wa faida. Hivyo kuwauzia gesi Kenya hakuwezi punguza kiasi cha gesi tulichonacho.

Gesi yetu mpaka sasa inatumika kuzalisha umeme, asilimia 62 ya umeme wetu huu tunaotumia unazalishwa kwa gesi yetu ya Tanzania. Unaweza kuona jinsi watanzania wanavyofaidika na gesi yetu.

Kiukweli serikali yetu inamipango mingi sana ya kuhakikisha gesi yetu watanzania wanaitumia kwenye magari na kupikia pia. Ila bado serikali inatengeneza mazingira ya kuwezesha hayo. Lazima iweke miundombinu itakayo wezesha hiyo gesi kupatikana maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoani. Kuweka miundombinu hiyo panahitaji fedha za kuwekeza na panahitaji muda.
Kwa hiyo hayo mambo yakikamilika sote tutaweza kuitumia hiyo gesi kwenye magari na kupikia pia.
 
Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako.

1. Ukijaza gesi ya Tsh. 17,000 unaweza kusafiri kilomita zaidi ya 200.
Tsh. 17000 = Km. 200
? = Km. 1
Km. 1 = Tsh. 17000/200 = Tsh. 85

Kikawaida ukijaza lita moja ya petroli unaweza kusafiri kilomita 10 hadi 12. Chukulia lita moja ya petroli ni Tsh. 2886
Tsh. 2886 = Km. 12
? = Km. 1
Km 1 = Tsh. 2886/12 = Tsh. 240.5

Sasa ukitumia gesi kwenye gari yako kwa kila kilometa 1 unaokoa Tsh. ngapi?

Unaokoa = Tsh. 240.5 - Tsh. 85 = Tsh 155.5

Kumbe kwa kila Km. 1 unaokoa Tsh. 155.5

Gharama za kuiongezea mfumo wa gesi gari yako ni Tsh. 1,800,000. Tunazibadili hizi kwenda kwenye Km.

Km 1 = Tsh. 85
? = Tsh 1800,000
Tsh 1800, 000 = Km. 21176.5

Unataka tujue katika Km. hizo tunaokoa Tsh. ngapi?

Km. 1 = unaokoa Tsh. 155.5
Km. 21176.5 = ?

Unaokoa = Tsh. 21176.5 × 155.5 = Tsh. 3,292,941

Sasa unaweza kuona ukiongeza mfumo wa gesi unatumia Tsh. 1,800,000 ambazo zinakuwezesha kutembea Km. 21176.5 kama ukizitumia kununulia gesi. Sasa ukitembea Km. 21176.5 hizo kwa kutumia gesi utaokoa Tsh 3,292,941. Kumbe gharama uliyotumia kubadilisha gari yako itumie gesi itarudi ukisha tembea Km. 21176.5 na faida juu.

2. Kuongeza mfumo wa kutumia gesi kwenye gari inayotumia mafuta inagharimu Tsh. 1,800,000. Gharama hii ni kwa gari zenye cc 400-2000. Na kutakua na ongezeko la Tsh. 80,000 endapo kama spark plugs hazitaruhusu mfumo huo.

3. Ukisafiri kwa kutumia Tsh. 100,000 za mafuta ukitumia gesi utatumia Tsh. 40,000 tu. Umeokoa Tsh. 60,000.

4. Ukiweka mafuta ya Tsh. 45,000, kwa mwezi utatumia Tsh. 1,350,000. Kwa miezi miwili ni Tsh. 2,700,000.
Gesi unaweka ya Tsh. 17,000 na unatumia siku 2 mpaka 3. Inamaana unaongeza gesi kila baada ya siku 2 or 3.
Kama kila baada ya siku 2 unaongeza gesi mara 15 kwa mwezi (Tsh. 17,000 × 15 = Tsh. 255,000). Kwa miezi mwili hii ni Tsh. 510,000.
Gharama za kuongeza mfumo wa gesi ni 1, 800,000 + gesi ya miezi miwili ni Tsh. 510,000 jumla ni Tsh. 2,300,000.

Hivyo ukichukua gharama za mafuta kwa miezi miwili Tsh. 2,700,000 ukatoa gharama ya kufunga mfumo wa gesi na matumizi ya miezi mwili ya Tsh. 2,300,000 unabakia na Tsh. 400,000.

Kwa hiyo kwa mfano huu faida unaanza kuiona baada ya miezi miwili. Kuanzia mwezi wa tatu badala ya kutumia Tsh.1,300,000 kwa mafuta anatumia Tsh.255,000.

Hivyo unaweza kuona jinsi unavyo okoa fedha nyingi ukiongezea mfumo wa gesi kwenye gari yako inayotumia mafuta.

Ukitaka kuongeza mfumo wa gesi kwenye gari yako embu piga namba hii 0747744895
Sawa,
Lakin still 1.8m mko juu sana.
 
Back
Top Bottom