Ngoja nikupe mifano ya hesabu inayoeleza faida za kutumia mfumo wa gesi kwenye gari yako na jinsi utakavyo okoa fedha nyingi

Leteni Dodoma hii kitu
Boss yawezekana huko mbeleni serikali ikawaletea gesi na Dodoma pia. Na kama unavyojua hii biashara ya gesi inaangalia maeneo yenye magari mengi.
Ila inawezekana sana tukiwa na tenka la gesi linatoa gesi Dar es Salaam au Mtwara na kuileta huko Dodoma na kuijaza kwenye magari moja kwa moja.
 
We unahamasisha hivyo waziri anagawa mitungi ya gesi porini wasipokuwepo mawakala .halafu mnaplan kupeleka ges kenyabwakati soko la ndani hamlitendei haki.
 
We unahamasisha hivyo waziri anagawa mitungi ya gesi porini wasipokuwepo mawakala .halafu mnaplan kupeleka ges kenyabwakati soko la ndani hamlitendei haki.
Boss gesi ambayo waziri wetu wa nishati aliwagawia watanzania lengo kubwa lilikua ni kuwahamasisha watanzania wa vijijini kutumia gesi kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa vinavyochochea ukataji wa miti yetu na kuharibu misitu yetu. Ni jambo zuri ambalo hata mimi nililipenda.

Lakini pia Tanzania tuna kiasi kikubwa cha gesi ambacho tukitegemea soko la ndani pekee wawekezaji watachelewa kurudisha gharama walizotumia kwenye uwekezaji wao na sisi wenyewe tutachelewa sana kuanza kupata mgao wa faida. Hivyo kuwauzia gesi Kenya hakuwezi punguza kiasi cha gesi tulichonacho.

Gesi yetu mpaka sasa inatumika kuzalisha umeme, asilimia 62 ya umeme wetu huu tunaotumia unazalishwa kwa gesi yetu ya Tanzania. Unaweza kuona jinsi watanzania wanavyofaidika na gesi yetu.

Kiukweli serikali yetu inamipango mingi sana ya kuhakikisha gesi yetu watanzania wanaitumia kwenye magari na kupikia pia. Ila bado serikali inatengeneza mazingira ya kuwezesha hayo. Lazima iweke miundombinu itakayo wezesha hiyo gesi kupatikana maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoani. Kuweka miundombinu hiyo panahitaji fedha za kuwekeza na panahitaji muda.
Kwa hiyo hayo mambo yakikamilika sote tutaweza kuitumia hiyo gesi kwenye magari na kupikia pia.
 
Sawa,
Lakin still 1.8m mko juu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…