Samahan we unasikiliza na huwa huelewi, jamaa kauliza swali nyimbo 5 za konde zinazohamasisha bangi. Umekuja na essay kubwa kuelezea reggae au country songs, hakuna mziki unafundisha kila kitu kuzidi hip hop hii dunia.
R&b ni mapenz
Hip hop elimu
Reggae uhuru na aman
Kwaya Mungu
Nilizosahau utamalizia
Mkuu zingatia hii point yangu kwanza kwenye maelezo uliyo ni quote. 👇👇
Binafsi nasikiliza HIPHOP kwasana sababu mara nyingi wanaimba vitu positive 🧠.
Chapili mimi kuandika maelezo mengi ni personal desicions, Don't judge me.
Tatu kuhusu Kondeboy kuhamasisha bangi kwenye nyimbo zake ni utani that's why nikaweka kile kikohozi na Emoji ya 😆, Nani asiyejua kwamba Hiphop ndiyo inaongoza kunahamasisha zaidi kuvuta bangi na kuonyesha ni kama sehemu ya kutuliza akili?
Kama unaijua hiphop vizuri, Historia yake, Waanzilishi na nguzo za hiphop basi utakua unaelewa kwanini rappers wengi ni Wavuta bangi.
Problem is yo're not taking things seriously.
Kwa maelezo hayo, Infact hujui genre za mziki, Hebu nikupe mwanga kidogo:
Mziki wa R&B ni mziki ambao hugusa hisia za aina tofauti iwe Mapenzi, Huzuni au Hamu ya mafanikio.
si lazima uhusiane na Mapenzi - Kasikilize Maneno au Bado kidogo zote za Benpol kama utasikia mapenzi humo nicheki nikutumie elfu10.
Tatizo mada zinazopendwa sana ni za Mapenzi na ngono ngono that's why R&B imetawaliwa na Mapenzi na Ngono tupu kwasababu za kiuchumi.
Wahenga walisema fuata nyuki ule asali.
Lakini pia Mziki wa Reggae ni mziki ambao unagusia sehemu nyingi si lazima uhamasishe amani pekee 👇👇
Mapenzi pia yanaweza imbwa kwenye reggae, Fungua link hiyo utakutana na ngoma 50 za mapenzi za reggae ambazo hakuna kuhamasisha amani kama unavyodai bali ni Mapenzi tu.
View: https://open.spotify.com/album/65rNNllspZfeYF2jdylzzf
Ninachokiona hapa unachanganya kati ya Imani ya Rastafatian na Mziki wa Reggae!!
Kwa taharifa yako hata kwaya si lazima ziwe nyimbo za Mungu tu, Tatizo ume claim 👇
Kuhusu HIPHOP pia sio mziki wa kuinspire Positive tu, Kuna ngoma za Hiphop kali beat tu ndani umeimbwa upuuzi tu au mda mwingine matusi tupu tena zipo mpaka Hiphop za Mapenzi huamini;
Kasikilize hizi ngoma:
•Dizasta Vina - Fallen angel. 🎶
•Sugu - Hayakua mapenzi. 🎶
•Chindoman ft Watengwa - Haikupangwa. 🎶
•Godzilla - Milele. 🎶
•Fidq ft Cristian bella - Roho. 🎶
•Joh Makini ft Baraka the prince - Permanent love. 🎶
•Dah remix. 🎶
Infact unaandika usichokijua, Huna uelewa wa kutosha kuhusu Genre za muziki.
CC:
Monetary doctor