Ng'ombe mwenye thamani ya IST

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nilikuwa sijui kama kuna ng'ombe mwenye thamani inayozidi milioni tano.

Lakini hii clip imenifungua macho! Ng'ombe wa maziwa anauzwa Tsh 12,000,000/=

Milioni kumi na mbili si bei ya IST used?

Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa unalipa!
Your browser is not able to display this video.
 
Uzitowake si chini ya kilo 1,000 yaani tani moja.
Umenikumbusha Kikwete alikwenda Zimbabwe akashangaa kuona ng'ombe anauzito unaozidi tani moja, mpaka anaondoka madarakani hakuiwezesha nchi iwe na ng😱mbe wa aina hiyo, hapo ndipo utaona ziara zao huwa kwa manufaa yao tu.
 
Ila nyie motivation speakers huwa mnaongea vitu kiurahisi rahisi sana
 
Kasema lita 60 kwa siku! Rekebisha mahesabu! Na maziwa bei ni 1,500 kwa lita
 
ngombe mwenye uzito karibia tani moja unamtunza kwa 2m kwa mwaka? hyo hela haitoshi mkuu.
 
Kwa maelezo yake yanauzwa almost yote mengine anajiuzia mwenynyewe kwenye miradi mingine ya mbwa..Ng'ombe inakamuliwa mara tatu sio mchezo kwa huku nilipo bei ya lita ni 2000×60=120000 kwa siku kwa ng'ombe mmoja kwa mwezi unaongelea Tsh 3,600,000/= kwa mwaka unaongelea Tsh 43,200,000/= endapo ngombe atakamuliwa mwaka mzima kitu ambacho ni nadra sana maana kuna majira huwa wanakaaaida ya kupunguza utoaji.

Mzee apewe pongezi sana ameamua kwakweli.
 
kwa hyo jk yeye ana ng'ombe kama hao? kuna mwamba alishasema hapa jf kuna kwenye baadhi ya ranch za taifa tuna pure breed ya boran, ambao nao kwenye uzito wanatisha.
 
Mkuu Nadhani Alinunua Binafsi Anafuga Msoga Huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…