LURIGA
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 2,436
- 3,723
Washabiki wa CHADEMA wanajidanganya sana kwamba mgombea wao atashinda katika huu uchaguzi. Hoja yao kubwa ni wingi wa watu kwenye mikutano ya Tundu Lisu japo mikutano ya mgombea wa ccm watu ni wengi zaidi. Hao watu wanaokuja kusikiliza hotuba za wagombea siyo wote wanasifa za kupiga kura, wengine bado hawajafikisha umri wa kupiga kura, wengine hawajajiandikisha kupiga kura au kubadili taarifa zao kwenye daftari la wapiga kura kutokana na kuhama sehemu walizojiandiksha mwanzo, wengine ni wanachama wa vyama vingine ila wanakuja tu kusikiliza na hata kuwaona wagombea urais (live) kuliko kusimuliwa.
Na kikubwa zaidi ni kwamba hao watu wanaohudhuria hiyo mikutano ya Tundu Lisu ni sehemu ndogo sana ya population katika jimbo au mkoa husika. Japo watu wanacheka kwamba kwenye mikutano ya magufuli watu wanaletwa kwa malori toka sehemu nyingine za jimbo au mkoa lakini hili linaweza kuwa na positive effect kwa ccm. Tukumbuke kwamba wagombea urais hawawezi kwenda/kufika kwenye kila jimbo kwa ajili ya kunadi sera zao hivyo kwa ccm njia mojawapo ni kuwaleta makada wao kwenye mikutano ya mgombea urais wa chama hicho kwa lengo la kusikia sera na baadae kwenda kuhamasisha wananchi kwenye maeneo wanaokotoka kumpigia kura mgombe awa chama chao. Pia CCM wana matawi hadi mashinani hivyo influence yao huko hasa maeneo ya vijijini ni kubwa wakati chadema hawajawekeza sana maeneo ya vijijini achilia mbali maeneo mengi mijini hawana matawi. Chadema inaendesha siasa za uanaharakati hawana base. Pia Magufuli anarekodi nzuri ya utendaji kazi wake kitaifa na kimataifa tangu aingie madarakani 2015 hadi 2020. Huo pia ni mtaji tosha kwa mgombea wa CCM.
Hivyo washabiki wa CHADEMA wasichukulie hizi kampeni za urais kirahisi hivyo kwa hoja hiyo dhaifu ya mahudhurio ya wananchi kwenye mikutano ya kampeni maana baada ya tarehe 28/10/2020 wanaweza kubaki midomo wazi kwa mshangao maana mgombea wa CHADEMA anaweza akaambulia asilimia ndogo sana ya kura zote. Na kama kawaida ya wapinzani watakimbilia kusema ccm wameiba.