Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana,
Mimi Ngongo Balozi wa kumi natarajia kufika mbele ya kikosi kazi kutoa maoni yangu kuhusu Katiba.
Mosi,naunga mkono katiba mpya kwakuwa hii ya sasa imepitwa na wakati.
Natarajia kuangazia mambo manne tu mengine nawaachia waTanzania wengine.
Katiba lazima ipunguze ukubwa/msururu wa serekali hasa viongozi wakuu wa kitaifa na viongozi ngazi ya Wilaya.
Napendekeza cheo cha Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kiwe kimoja.
Napendekeza Katiba mpya Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Miji kiwe cheo kimoja,Majukumu ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kiunganishwe.
Napendekeza Wabunge na Madiwani wasigombee zaidi ya vipindi viwili.
Napendekeza teuzi za Rais kwa nafasi za Mawaziri,Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Mashirika ya Umma,Mabalozi,Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama lazima kuthibitishwa na Bunge.
Napendekeza mishihara ya wote niliowataja hapo pawepo na bodi ya kupandisha mishahara na stahili nyingine badala ya kuachwa kujipandishia mishahara hovyo hovyo.
Napendekeza kuunganisha NIDA na RITA
Napendekeza idadi ya mawaziri ipo ktk katiba.
Napendekeza iwepo tume\Bodi ya kuajiri,kufukuza na kupandisha cheo majaji.
Napendekeza Rais akitenda matendo ya jinai ashitakiwa mara moja si kungoja mpaka akistaafu.
Napendekeza umiliki wa ardhi urejeshwe kwa wananchi si umma kupitia Rais.
Naomba kuwasilisha.
Ngongo kwa sasa safarini kuelekea kutoa maoni mbele ya kikosi kazi.