Viongozi kama Eltwege, Tale tale? FA, Temba, almanusura hadi Harmonizer apewe jimbo.Hii tabia ya kuokoteza viongozi, hadi kiongozi mkuu kabisa wa nchi ni tabia mbaya na hatari sana kwa nchi yetu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Viongozi kama Eltwege, Tale tale? FA, Temba, almanusura hadi Harmonizer apewe jimbo.Hii tabia ya kuokoteza viongozi, hadi kiongozi mkuu kabisa wa nchi ni tabia mbaya na hatari sana kwa nchi yetu.
Inawezekana sana. Zile ofisi zaidi ya kujilimbikizia vyeo na ajira nyingi za wasoozalisha mimi sioni umuhimu wake kivile.Wewe mwenye akili niambie Majaliwa na Mpango nafasi zao haiwezekani ikawa moja.
Kama kuna jambo la muhimu kuliko hili, sijui jambo hilo ni lipi!
Mkuu 'Monk', ninakukumbuka sana katika mikwaruzano yetu humu JF, lakini hili hapa naondoa kofia na kuonyesha kipara mbele zako. Hongera sana!
Hata kama siyo mipango ya taifa ya miaka hamsini/hamsini; ishirini hadi thelathini inatosha kama kweli serikali zitalazimika na kuwajibika kutimiza mipango hiyo kikamilifu katika muda uliopangwa.
Na kama kuna dharura, basi patakuwepo na utaratibu mahsusi utakaotumika kuchepuka bila kuathiri malengo ya mwanzo.
Akili huna
Tanganyika na Zanzibar zinakuwa nchi moja au mbili kwenye muungano?
Napendekeza mikataba yote itakayohusu rasilimali za nchi lazima ipite bungeni na wananchi wajulishwe.
Nchi gani uliwahi kuiona ina mpango wa maendeleo wa miaka 50?Pendekezo Moja liwasilishe pia, watahakikisha vipi hii katiba mpya haikiukwi/ kusiginwa kama ilivyo ya Sasa?
Kuwa na katiba nzuri ni jambo Moja, utekelezaji ilete tija ni jambo lingine.
Binafsi sioni umuhimu wa bunge kabisa, ni kitu tumerithi tu au tumeiga Kwa wengine. Tunahitaji kamati yenye wabobezi wa mambo ya sheria kusimamia mchakato wa mambo ya kisheria.
Uwaziri uwe ni nafasi ya kitaalam. Unaomba kuwa waziri wa Nishati, vigezo vinaangaliwa, mnashindanishwa na unaeleza kwanini upewe hiyo nafasi. Inakua ni kazi ya mkataba unaongezewa muda Kwa kadri unavyotekeleza Kwa ufanisi majukumu Yako kulingana na matarajio na malengo mliyojiwekea. Kwanza hapa tunaweza kuwa na Wakurugenzi na makaribu wakuu tu. Waziri wanini? Tunaongea gharama tu.
Waruhusu wagonbwa huru wasiokua na chama.
Mwisho, tuwe na mpango wa maendeleo wa miaka hamsini ambao ndio unaongoza jitihada, juhudi na nguvu zetu zote kuutekeleza kama taifa, viongozi wote akiwepo Rais, watapimwa Kwa namna wanavyotekeleza huo mpango. Haitajalisha chama Gani kinashoka Dola, ili kibaki madarakani ni lazima kithibitishe na kuweza kuleta mabadiliko kadri ya mpango wa taifa unavyoongoza.
Sasa hayo si maoni yangu? Weka Yako hapa. Pia Kuna post inayofuatia nimeeleza kuwa na Chombo Cha kuratibu mwenendo wa utekelezaji na kuona kama mabadiliko yanahitajika kutokana na mahitaji. Hatuwezi kuwa tunachezea rasirimali kisa ilani ya chama au mawazo ya Kiongozi anayeingia madarakani.Nchi gani uliwahi kuiona ina mpango wa maendeleo wa miaka 50?