Ngongo anatarajiwa kufika mbele ya kikosi kazi wakati wowote kuanzia kesho

Wewe mwenye akili niambie Majaliwa na Mpango nafasi zao haiwezekani ikawa moja.
Inawezekana sana. Zile ofisi zaidi ya kujilimbikizia vyeo na ajira nyingi za wasoozalisha mimi sioni umuhimu wake kivile.
 

Ahsante Kwa kuwa muungwana ndugu yangu, kama binadam inatokea kutofautisha, ila kuziweka kando tofauti zetu na kuendelea na maisha ndio kunaleta thamani ya utu.

Nashukuru pia Kwa kuongeza mfumo wa kupitia mwenendo wa utekelezaji wa huo mpango wa maendeleo. Hata kama Kuna mabadiliko au Kuna dharura, katiba inakua imeweka wazi ni namba Gani Hilo jambo litashughulikiwa.

Hii Kila Rais au awamu kuja na ilani yake haitatufikisha popote, ni upotevu wa rasirimali za taifa.

Lakini muhimu zaidi, itaongeza uwajibikaji Kwa viongozi wetu. Mtu ambae hawezi kuonyesha katika kipindi alichokua kwenye nafasi yake hatoweza kuthubutu kutaka kuendelea Tena. Na anaetaka kjiingiza huko, atajitafakari na kujipima kama anaweza kupelekea mbele utekelezaji wa huo mpango.

Uwe na wakati mwema mkuu
 
Akili huna
Tanganyika na Zanzibar zinakuwa nchi moja au mbili kwenye muungano?

Kwanini usitoe ya moyoni Kwa staha mkuu?
Jamaa ameweka bayana, haya ndio yanamfurukuta hawezi kupata usingizi Wala kutulia Hadi akayatoe mbele ya kikosi kazi. Amesisitiza mengine wataongezea wengine.

Muundo wa Muungano ni miongoni mwa mengine ambayo wewe unaweza kutaelezea. Kumbuka Zanzibar Wana serikali Yao na katiba Yao, kwanini usitoe maoni Yako kuhusu Hilo swali lako badala ya kumshambulia mleta mada?
 
Napendekeza mikataba yote itakayohusu rasilimali za nchi lazima ipite bungeni na wananchi wajulishwe.

Hapo kwenye bunge ndio mushkeli wangu unapoanzia, ukiangalia uwekezaji na fedha inapotea kuhudumia bunge na thamani tunayoipata kama taifa, ni biashara kichaa kama haliwezi kuboreshwa kuisomamia serikali, halina tija. Bora kuwa na kamati za wataalam walioajiriwa na wanapata hizo nafasi Kwa ushindani.

Mikataba itapitiwa na wataalam, wakihusisha mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Kaseme tena Chama kikitoa ahadi za uchaguzi kiitekeleze kwa 90+. Kisipotekeleza kifutwe maana tunadanganywa sana
 
Nchi gani uliwahi kuiona ina mpango wa maendeleo wa miaka 50?
 
Nchi gani uliwahi kuiona ina mpango wa maendeleo wa miaka 50?
Sasa hayo si maoni yangu? Weka Yako hapa. Pia Kuna post inayofuatia nimeeleza kuwa na Chombo Cha kuratibu mwenendo wa utekelezaji na kuona kama mabadiliko yanahitajika kutokana na mahitaji. Hatuwezi kuwa tunachezea rasirimali kisa ilani ya chama au mawazo ya Kiongozi anayeingia madarakani.

Mwisho wa siku sio Kila jambo lazima lifanane nchi zote, ndio maana tumejitumbukiza kwenye gharama zisizo na ulazima kisa tunataka kuwa kama wengine, tunadonoadonoa tunapoona Kuna unafuu wakati huko wanapofanya hivyo ni mfumo kamili unaotegemeana.

Mbona sie kesi ya uchaguzi ya matokeo ya Rais haiendi mahakamani wakati nchi zingine ni jambo la kawaida?

Pia kwanini ukomo wa rais uwe miaka kumi? Kwanini isiwe mitano tu au ikawa zaidi kama anafanya mambo ya kulinufaisha taifa na wananchi Kwa ujumla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…